Wakuu,
Kama umepita mitaa ya Mikocheni hivi karibuni utagundua kuna wachina wengi sana.
Pale Ursino Street, wana hospitali kabisa ya wachina, supermarket na restaurant kubwa sana special kwa ajili yao.
Kuna hoteli moja pale Mikocheni ilikuwa inaitwa Regency Park wameichukua wameifanya kuwa ya kwao na pale makao makuu ya zamani ya Bolt there is a whole hotel ambayo bado haijaisha wameichukua. Hata pake Palm Village kuna a restaurant ya kichina.
Huko Masaki , mbele ya Warehouse kuelekea International School of Tanganyika kuna restaurants na sehemu kama 4 kwa ajili ya Wachina tu. Homecity 2 zote ya Mikocheni na Mlimani City ni za kwao
Yaani kuna mtaa wa pale juu karibu na Morocco Square kote kumejaa Wachina tu
Pale kwenye nyumba za TBS, wamechukua nyumba nyingi wameweka garage na indoor small industries.
Ndani ya miaka 5 Masaki na Mikocheni inaenda kuwa ni mji wa kichina. Hata wapiga kura wanaenda kuwa wachina