Video: Ni kama masihara hivi lakini polepole Mikocheni na Masaki zinaenda kutawaliwa na Wachina

Usisahau kuwa hata Marekani,mji wa Manhattan jimbo la Newyork kuna China town,na hii ipo siku nyingi sana,wachina kuwazuia kwenye hii dunia ni sawa na kuzuia mto kuingia baharini utahangaika sana...
 
Unawaona wachina tu,ila husemi kuhusu wahindi kukamata asilimia 80 ya uchumi wenu.mitaa ya katikati ina maghorofa zaidi ya mia na yamejaa wahindi tu.miafrika bana

Hoja imejikita kwenye Wachina, hayo mambo ya Wahindi umeleta wewe. Jikite kwenye mada.

Na it seems hujui kabisa historia ya nchi hii na namna walivyokuwa mstari wa mbele kwenye masuala ya uhuru na ukombozi.

Wahindi walikuwepo hapa Afrika Mashariki kabla hata Nyerere hajazaliwa. Ni Watanzania kuliko hata wewe

Jielimishe historia ya nchi yako uepuke aibu ndogondogo kama hizi
 
Usemayo ni kweli mie mwenyewe nataka JV na mchina aweke 8 floors, Target Yao ni Morocco Square Hadi Mlalakua, Regent washaivamia

Acha walete Fursa ,wazee wa macho macho

Wako wengi sana huko na it raises a lot of questions.

Wale jamaa soon tutaanza kuwaona wanagombea udiwani na Uenyekiti wa vitongoji
 
Usisahau kuwa hata marekani,mji wa Manhattan jimbo la Newyork kuna China town,na hii ipo siku nyingi sana,wachina kuwazuia kwenye hii dunia ni sawa na kuzuia mto kuingia baharini utahangaika sana...

Kuna kipindi walianzisha hadi kituo cha polisi cha wachina huko Manhattan, baadae kikafungwa

Imagine what they would do kwa nchi kama Tanzania ambayo intelligence na usalama tumezidiwa kila kitu na Marekani
 
Usisahau kuwa hata Marekani,mji wa Manhattan jimbo la Newyork kuna China town,na hii ipo siku nyingi sana,wachina kuwazuia kwenye hii dunia ni sawa na kuzuia mto kuingia baharini utahangaika sana...
Mshamba huyo hajatembea nchi za watu achana nae unaweza kubishana na mtu kumbe katoka kwao uchindile kaja Dar juzi kati tu sasa unafikiri ataelewa nini kuhusu utandawazi.
 
Hahahaha, sio wengi ila hizo alizotaja karibu zote ni kweli..

weka statistics basi kwamba wapo wangapi sio unaandika kama mjinga
 
Mshamba huyo hajatembea achana nae unaweza kubishana na mtu kumbe katoka kwao uchindile kaja Dar juzi kati tu sasa unafikiri ataelewa nini kuhusu utandawazi.

Jibu hoja acha matusi na kujikuta unajua sana jiji.

Nimekuuliza maswali huko juu hujajibu hata moja, instead umeanza kuita watu washamba.

Wewe kama sio uvccm sijui maana unafanana nao sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…