Video: Ni kama masihara hivi lakini polepole Mikocheni na Masaki zinaenda kutawaliwa na Wachina

Sasa wewe inakuuma nini? kama vp na wewe nenda china ukatawale mitaa ya Guangzhou. Huu ndio kiashiria cha ubaguzi wenyewe sasa.
Kama unawapenda WACHINA wapeleke kwako au kijijini kwenu. Hao watu ni wabaguzi sana na uwekezaji wao umejikita katika kujinufaisha wao tu.
 
Unawaona wachina tu,ila husemi kuhusu wahindi kukamata asilimia 80 ya uchumi wenu.mitaa ya katikati ina maghorofa zaidi ya mia na yamejaa wahindi tu.miafrika bana
Kwani mwenzetu we si mwafrika? Tu fait pitié lol
 
Wakuu,

Kama umepita mitaa ya Mikocheni hivi karibuni utagundua kuna wachina wengi sana.

Pale Ursino Street, wana hospitali kabisa ya wachina, supermarket na restaurant kubwa sana special kwa ajili yao.

Kuna hoteli moja pale Mikocheni ilikuwa inaitwa Regency Park wameichukua wameifanya kuwa ya kwao na pale makao makuu ya zamani ya Bolt there is a whole hotel ambayo bado haijaisha wameichukua. Hata pake Palm Village kuna a restaurant ya kichina.

Huko Masaki , mbele ya Warehouse kuelekea International School of Tanganyika kuna restaurants na sehemu kama 4 kwa ajili ya Wachina tu. Homecity 2 zote ya Mikocheni na Mlimani City ni za kwao

Yaani kuna mtaa wa pale juu karibu na Morocco Square kote kumejaa Wachina tu

Pale kwenye nyumba za TBS, wamechukua nyumba nyingi wameweka garage na indoor small industries.

Ndani ya miaka 5 Masaki na Mikocheni inaenda kuwa ni mji wa kichina. Hata wapiga kura wanaenda kuwa wachina
Mi5tena
 
Mleta mada nenda VETA hao ni Diaspora.

Watafutaji wamepata fulsa wanakimbizana nazo.

"If you can fight them join them".
 
Kama unawapenda WACHINA wapeleke kwako au kijijini kwenu. Hao watu ni wabaguzi sana na uwekezaji wao umejikita katika kujinufaisha wao tu.
Hukuna muwekezaji yoyote hata wazaww pia mwenye nia kukunufaisha wewe! Hapo sasa ni sera za nchi kuangaliwa upya na kama hufahamu kuna waTz kibao wamenufaika kupitia hao jamaa. Na karne hii mchina ni kama maji ngumu sana kumkataa.
 
WaTanzania wengi hatuna exposure, vitu vidogo kama hivi mtu anajiropokea tu pasipo kutafakari kwa kina.
Naungana na wewe kwa Dunia ya Sasa huwezi kukwepa kitu kama hivyo. USA ile tunayo iona Leo imejengwa na wageni, tumeshuhudia mtu ambaye siyo mzaliwa wa Marekani akawa Rais ndiyo ujiulize ni Kwa namna gani wenzetu wanawatazama wahamiaji kama fursa.

Kigumu hapa Serikari iwatumie hawa wageni kama fursa hasa kwenye swala Zima la Creative and Innovative.
Nani huyo asiyekuwa mzaliwa wa Marekani akawa Rais wao?
 
mtu mweusi hua ni mbaguzi sema ngozi yake inakua kama kinga ikiguswa. kwa marekani wanaita reverse racism.

ulichoandika hapa unaonesha wewe ni mbinafsi na mbaguzi

hiyo mitaa uliyotaja hakuna wachina wengi kias hiko umekuza jambo ili upate attention
Kuna watu hawatembei labda wanadhani hii ni Tanzania tu hata huko majuu iko mitaa mpaka jina China Town, Singapore kuna sehemu Arab street kuna India street wamejaa nenda hapo Dubai tu Deira yote ni wahindi, Afghan na makabila chungu nzima hukuti mwarabu mpaka wa China. Ndani ya Dubai mpaka China Mall sasa hapa la ajabu nini? ndio dunia ilivyo ukiwa wewe umelala fursa zipo wanakuja watu wanafanya biashara. Tuache kuleta mambo ya miaka ya 80 huko. Na uhakika na nchi nyingi tu duniani lazima utakuta hali hii.
 
Hakuna mtu mbaguzi kama mtanganyika, mpemba na muunguja, acheni wenye fedha zoo waishi wapendapo alimradi wamepanunua na wamelipa fedha stahili Bila lawama, utapiga kelele za kuumilia mpaka unaweza kata roho, pambana kijana, dunia ya wote hii.
 
Hukuna muwekezaji yoyote hata wazaww pia mwenye nia kukunufaisha wewe! Hapo sasa ni sera za nchi kuangaliwa upya na kama hufahamu kuna waTz kibao wamenufaika kupitia hao jamaa. Na karne hii mchina ni kama maji ngumu sana kumkataa.
Ukitaka kufunga biashara yako mwaka tu wewe ajiri wa Tanzania utakuja kuniambia hapa, uaminifu zerooooooo na hawa wanapewa intelligence ya kibiashara kabla ya kufungua biashara zao.
 
Kuna watu hawatembei labda wanadhani hii ni Tanzania tu hata huko majuu iko mitaa mpaka jina China Town, Singapore kuna sehemu Arab street kuna India street wamejaa nenda hapo Dubai tu Deira yote ni wahindi, Afghan na makabila chungu nzima hukuti mwarabu mpaka wa China. Ndani ya Dubai mpaka China Mall sasa hapa la ajabu nini? ndio dunia ilivyo ukiwa wewe umelala fursa zipo wanakuja watu wanafanya biashara. Tuache kuleta mambo ya miaka ya 80 huko. Na uhakika na nchi nyingi tu duniani lazima utakuta hali hii.
Mkuu Heijah umeliweka vizuri sana. Wachina ni kama maji usipoyanywa utayaoga. Na yanayotokea hapa siyo mageni duniani, China effect ipo dunia nzima.

Watanzania wanapaswa wajifunze anachofanya Mchina, wakiige ili wafanikiwe. Ila kumpiga vita Mchina ni kupoteza muda
 
Wakuu,

Kama umepita mitaa ya Mikocheni hivi karibuni utagundua kuna wachina wengi sana.

Pale Ursino Street, wana hospitali kabisa ya wachina, supermarket na restaurant kubwa sana special kwa ajili yao.

Kuna hoteli moja pale Mikocheni ilikuwa inaitwa Regency Park wameichukua wameifanya kuwa ya kwao na pale makao makuu ya zamani ya Bolt there is a whole hotel ambayo bado haijaisha wameichukua. Hata pake Palm Village kuna a restaurant ya kichina.

Huko Masaki , mbele ya Warehouse kuelekea International School of Tanganyika kuna restaurants na sehemu kama 4 kwa ajili ya Wachina tu. Homecity 2 zote ya Mikocheni na Mlimani City ni za kwao

Yaani kuna mtaa wa pale juu karibu na Morocco Square kote kumejaa Wachina tu

Pale kwenye nyumba za TBS, wamechukua nyumba nyingi wameweka garage na indoor small industries.

Ndani ya miaka 5 Masaki na Mikocheni inaenda kuwa ni mji wa kichina. Hata wapiga kura wanaenda kuwa wachina
Kwani tatizo nini mkuu. Tuache akili za kijamaa jamaa ulimwengu ni kijiji mkuu. Mbona husemi wahindi na wakenya ambao.kila mwaka wanadabo
 
Wakenya machimbo yao ni wapi?, wahindi tunafahamu sana?
 
wanalipa kodi au hawalipi? kama wanalipa, shida yako nini? wakati hata wasingekuja wewe au yule msingekuja kuishi masaki au mikocheni maisha yenu yote.
Acha hizo dharau wewe au uliteta na Mungu akakuhakikishia kuwa hatawapa frusa ya kuishi Masaki au Mikocheni mpaka wanaingia kaburini.🥲
 
Back
Top Bottom