Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Naona akataka kugonga na wananchi wakati anaondoka
 
Huyu polis alipaswa kuvuliwa madaraka Mara moja. Jeshi La polis limeshaharibiwa sana na siasa.Nawashangaa chadema na wapinzani kutochukua hatua stahiki Mara moja
Mimi nafikiri ujumbe utakuwa ulishawafikia Wahusika ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hapo kuna mtego kwao.
 
Huyo askari lafudhi yake tu sio mtanzania..hawa polisi kwani hawana familia tugawane nao vitengo tu..
 
Mwambieni sisi wananchi wa Hai tutamchagua kaka Mbowe yeye aendelee kubisha hivyohivyo ili aendelee kulinda kibarua chake kwa kujipendekeza kwa mabosi wake.)
 
Afukuzwe cheo huyo askari.
Hana maadili ya KAZI
Umefuatilia vizuri clip? Au...! Kwa nini Mbowe aseme kumbe na wewe unajua!! Mimi nilitegemea Mbowe aseme nitamshinda! sijasikia neno hilo kutoka kwa Mbowe! Acheni manipulation!!! Vyombo vya dola viko kazini!
 
Afukuzwe cheo huyo askari.
Hana maadili ya KAZI
Umefuatilia vizuri clip? Au...! Kwa nini Mbowe aseme kumbe na wewe unajua!! Mimi nilitegemea Mbowe aseme nitamshinda! sijasikia neno hilo kutoka kwa Mbowe! Acheni manipulation!!! Vyombo vya dola viko kazini!
 
Katika hali ya kushangaza OCD wa Hai ameonekana akimwambia Mbowe hadharani kuwa hawezi kushinda uchaguzi katika jimbo la Hai.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la polisi ni miongoni mwa taasisi ambazo zinapaswa kutokuegemea upande wowote katika uchaguzi huu....
Sisi Watanzania ni waoga mno, huyo OCD uchwara alipaswa kushikishwa adabu ila kwa kuwa uogaaa umezidi wananchi tunaangalia tu.
 
"Kunya anye kuku akinya bata kaharisha" Mbowe amebanwa kila kona tusubiri tarehe 28 kuna jambo pale Hai
 
Alicho kosea Afisa wa polisi ni kusema ukweli, Ata wenyewe CHADEMA wanajua kuna majimbo machachesana ambayo wanaweza wakashinda ndiomaana hata kwenye kura za urais waneshakata tamaa kabisa.
Umetoka usingizini, Akili ndogo inapoamini ni akili kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…