FREEMAN MBOWE VS OCD MPINA HAI
Imeonekana Video Fupi inayozunguka ikionyesha Mabishano kati ya Freeman Mbowe na OCD wilaya ya Hai.
Ili Kutenda Haki tujiulize na Kujibu maswali machache
1.Je?Freeman Mbowe alipaswa kuwepo pale kwa mujibu wa ratiba ya Tume?bila shaka hakupaswa ndio maana anaonekana akisema hata Rais akipita anaweza kusimamishwa, kwa maana hyo aliingilia Ratiba na Alivunja kanunu
2.Mbowe anasikika akimuambia OCD" huyo mnayembeba habebeki' Je? Kwa kiongozi mature na mwenyekiti wa Chama aliyesaini hati ya maadili alipaswa ku-provoke mamlaka inayolinda na Kusimamia mikutano yake?
3.Kitendo cha Mgombea ubunge mbowe kujilinganisha na Rais badala ya kutii ratiba ambayo polisi wanaisimamia ili kuzuia uvunjifu wa amani ni sahihi?
Kwa vyovyote vile busara ilipaswa na inapaswa kuwa Reciprocal, sio sawa kujadili matamshi ya OCD huku tukijifanya hatuoni muenendo wa matukio yaliyopelekea kauli hiyo na Kupishana huki kutokea.
Kama ambavyo Jeshi la Polisi lina wajibu wake lakini vyama vya siasa vina wajibu mkubwa zaidi wa kutii na kuheshimu Ratiba,kanuni na makubaliano waliyoyaweka hasa katika kipindi hiki cha mpito,na Freeman Mbowe hukwepi lawama katika hili.
Nimalizie kwa kusema Hai Vita haitakuwa Lelemama, inaonekana vita Sio nyepesi hata kidogo, Mbowe awekeze kurudisha imani ya Wapiga kura wake na sio controtation zinazofanya aonekane mwepesi siasani.