Video: Paul Makonda na harakati za hila za kuulinda mfumo wa serikali tawala ya CCM ulioshindwa. Atafanikiwa au anasukuma anguko lake?

Kinachowatesa nyie siyo hicho unachotaka tukiamini, mnateswa na umati mkubwa unaomwamini Makonda.

Sina mashaka yoyote kwamba wewe ni Mwana CCM uliyejawa na woga tu!!

Huyo Mwamba hakamatiki. Kubalini tusonge mbele
 
Mie namwona maigizo anayofanya ni sawa na akina Senga na Bambo!
Kama kuna anaebisha aende kule alikopita hakuna utekelezaji wowote zaidi ya usanii!
Yeye mwenyewe anajua utekelezaji hauwezekani lengo ni kuwahadaa mafala!
 
Kuna wakati The Legendary anaamua kuwa ndumilakuwili
 
Wewe chawa tumia akili, siyo kila mtu anaehoji na kuikosoa serikali ni mpinzani. Watu wanafanya hivyo ili serikali iwajibike na kuleta ustawi kwa jamii ya Watanzania. Siyo kila mtu kwa mfano, anaepinga mikataba mibovu ni mpinzani wa CCM, hapana ni kwasababu ya ustawi wa taifa.

Kwa wenye uelewa wewe ndiye adui namba moja wa CCM na serikali ya Samia. Unatafuta kuvuna bila jasho. Hushughulishi akili yako kushauri wala kuonyesha panapokosewa. Unajuwa ni kusifia tu hata maamuzi yasiyo sahihi, hausaidii kuonyesha njia Watu wa ina yenu chama kikiwaendekeza kitaangamia. Ni watu mnaopaswa kuwa kwenye chama kama cha Prof. Lipumba na siyo CCM.
 

Watoto wakikusumbua sana unawatafutia dude wahangaike nalo upumue kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachowatesa nyie siyo hicho unachotaka tukiamini, mnateswa na umati mkubwa unaomwamini Makonda.

Sina mashaka yoyote kwamba wewe ni Mwana CCM uliyejawa na woga tu!!

Huyo Mwamba hakamatiki. Kubalini tusonge mbele

Yaani watu wenye akili wateswe na umati wa Makonda kana kwamba hatujui unapatikana vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…