Video: Paul Makonda na harakati za hila za kuulinda mfumo wa serikali tawala ya CCM ulioshindwa. Atafanikiwa au anasukuma anguko lake?

View attachment 2891582
This video is Courtesy of SK Media Online TV.

=====================================================
KWA UFUPI;

1. Paul Makonda ni Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ndani ya CCM. Yupo barabarani anatembea nchi mzima hata sasa kwa kinachoitwa "ziara ya kuimarisha uhai wa chama..."

2. Ukifuatilia hotuba zake ktk mikutano yake, utaona kwa uwazi kabisa nyuma ya pazia sura ya Mtendaji mkuu wa serikali (Rais Samia Suluhu Hassan) na sio sura ya kiongozi wa idara ndogo tu ndani ya Chama Cha Mapinduzi - CCM yaani Idara ya Itikadi na Uenezi.

Mtu anaweza jiuliza, huyu mtu anafanya hivi kwa makusudi, kwa bahati ya kutojua au ana baraka za boss wake M/kiti CCM taifa na Rais wa JMT?

Ni Kwa sababu maagizo yake ni maigizo tu. Hakuna Mtendaji makini wa serikali atayatilia maanani na kuyatekeleza. Ni kwa sababu hayatoki kwa mtu sahihi kwa mtiririko wa utendaji wa kiserikali..

Mtu anajiuliza Yuko wapi Rais mwenyewe? Yuko wapi VP, Dr Phillip Mpango? Yuko wapi PM, Mwl Kassimu Majaliwa? Wako wapi mawaziri wa kisekta ili kushughulika na matatizo na changamoto za nchi? Je, ya Paul Makonda ni kiashiria cha nchi na taifa kukosa uongozi makini na thabiti? Bila shaka hili la mwisho laweza kuwa jibu..!!

3. Kwa hili kila mtu anajiuiza kuikoni huko CCM kwa maigizo haya? Mifumo sahihi haitendi kazi tena au ndio kuchoka kwenyewe huku? Na kwanini Rais Samia Suluhu Hassan, VP Dr Phillip Mpango na PM Mwl Kassimu Majaliwa wanamtanguliza huyu mtu kupiga kelele ambazo kiuhalisia hazitakuwa na matokeo yoyote kwa wananchi?

4. Fuatilia uchambuzi wa jambo hili toka Kwa mwandishi wa habari mkongwe na nguli Ansbert Ngurumo ktk video ili ujue uongo, hadaa, hila na maigizo ya serikali ya CCM kupitia watu wake wa ajabu ajabu..
Kinachowatesa nyie siyo hicho unachotaka tukiamini, mnateswa na umati mkubwa unaomwamini Makonda.

Sina mashaka yoyote kwamba wewe ni Mwana CCM uliyejawa na woga tu!!

Huyo Mwamba hakamatiki. Kubalini tusonge mbele
 
Mie namwona maigizo anayofanya ni sawa na akina Senga na Bambo!
Kama kuna anaebisha aende kule alikopita hakuna utekelezaji wowote zaidi ya usanii!
Yeye mwenyewe anajua utekelezaji hauwezekani lengo ni kuwahadaa mafala!
 
Nimecheka sana! Eti machawa mazagazaga! Pascal wewe unayo heshima yako, lakini kuna wakati mahaba ya chama kipya yanakufanya uandike jambo linaloshindwa kukutofautisha na hao machawa.
Simamia kweli na haki uone kama kuna mtu anaweza kukuweka kundi moja na hao machawa mazagazaga wasio haya.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Kuna wakati The Legendary anaamua kuwa ndumilakuwili
 
Nashangaa Paschal Mayalla ameingia kwenye mtego wa wapinzani na kuamua kututukana sisi eti ni chawa mazagazaga

Acha niwe chawa mazagazaga lakini nitaendelea kuisemea serikali yangu na Rais wangu Mama Samia na chama changu. nimehiyari kutukanwa matusi yote yanayoandikika na yasiyoandikika .nimeamua kuyaoga matusi ya kila aina kwa ajili ya kuyasema mazuri yanayofanywa na Rais Samia kwa ajili ya Taifa letu. Nimeamua kubeba gharama ya kudhalilishwa kwa kila aina ya jina baya na kila aina ya udhalilishaji lakini sitayumba.
Wewe chawa tumia akili, siyo kila mtu anaehoji na kuikosoa serikali ni mpinzani. Watu wanafanya hivyo ili serikali iwajibike na kuleta ustawi kwa jamii ya Watanzania. Siyo kila mtu kwa mfano, anaepinga mikataba mibovu ni mpinzani wa CCM, hapana ni kwasababu ya ustawi wa taifa.

Kwa wenye uelewa wewe ndiye adui namba moja wa CCM na serikali ya Samia. Unatafuta kuvuna bila jasho. Hushughulishi akili yako kushauri wala kuonyesha panapokosewa. Unajuwa ni kusifia tu hata maamuzi yasiyo sahihi, hausaidii kuonyesha njia Watu wa ina yenu chama kikiwaendekeza kitaangamia. Ni watu mnaopaswa kuwa kwenye chama kama cha Prof. Lipumba na siyo CCM.
 
View attachment 2891582
This video is Courtesy of SK Media Online TV.

=====================================================
KWA UFUPI;

1. Paul Makonda ni Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ndani ya CCM. Yupo barabarani anatembea nchi mzima hata sasa kwa kinachoitwa "ziara ya kuimarisha uhai wa chama..."

2. Ukifuatilia hotuba zake ktk mikutano yake, utaona kwa uwazi kabisa nyuma ya pazia sura ya Mtendaji mkuu wa serikali (Rais Samia Suluhu Hassan) na sio sura ya kiongozi wa idara ndogo tu ndani ya Chama Cha Mapinduzi - CCM yaani Idara ya Itikadi na Uenezi.

Mtu anaweza jiuliza, huyu mtu anafanya hivi kwa makusudi, kwa bahati ya kutojua au ana baraka za boss wake M/kiti CCM taifa na Rais wa JMT?

Ni Kwa sababu maagizo yake ni maigizo tu. Hakuna Mtendaji makini wa serikali atayatilia maanani na kuyatekeleza. Ni kwa sababu hayatoki kwa mtu sahihi kwa mtiririko wa utendaji wa kiserikali..

Mtu anajiuliza Yuko wapi Rais mwenyewe? Yuko wapi VP, Dr Phillip Mpango? Yuko wapi PM, Mwl Kassimu Majaliwa? Wako wapi mawaziri wa kisekta ili kushughulika na matatizo na changamoto za nchi? Je, ya Paul Makonda ni kiashiria cha nchi na taifa kukosa uongozi makini na thabiti? Bila shaka hili la mwisho laweza kuwa jibu..!!

3. Kwa hili kila mtu anajiuiza kuikoni huko CCM kwa maigizo haya? Mifumo sahihi haitendi kazi tena au ndio kuchoka kwenyewe huku? Na kwanini Rais Samia Suluhu Hassan, VP Dr Phillip Mpango na PM Mwl Kassimu Majaliwa wanamtanguliza huyu mtu kupiga kelele ambazo kiuhalisia hazitakuwa na matokeo yoyote kwa wananchi?

4. Fuatilia uchambuzi wa jambo hili toka Kwa mwandishi wa habari mkongwe na nguli Ansbert Ngurumo ktk video ili ujue uongo, hadaa, hila na maigizo ya serikali ya CCM kupitia watu wake wa ajabu ajabu..

Watoto wakikusumbua sana unawatafutia dude wahangaike nalo upumue kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachowatesa nyie siyo hicho unachotaka tukiamini, mnateswa na umati mkubwa unaomwamini Makonda.

Sina mashaka yoyote kwamba wewe ni Mwana CCM uliyejawa na woga tu!!

Huyo Mwamba hakamatiki. Kubalini tusonge mbele

Yaani watu wenye akili wateswe na umati wa Makonda kana kwamba hatujui unapatikana vipi?
 
Back
Top Bottom