VIDEO: Sasa kama wanayajua haya kwanini ATCL, TTCL na SGR zinaendelea kutia hasara kila ripoti ya CAG?

Huyu siyo mtaalam. Ni hawa wababaishaji wa Samia wanaojifanya ni wataalam. Kuna mpango mkubwa wa kuwapa wawekezaji kila kitu, ndiyo lengo lao. Hii ni failuire ya CCM na siyo ya watanzania wote.
 
Huo utaalam au wataalam wote kwa nini wasiajiliwe na wapewe management ya kuyafanya hayo yote wanayotaka kuyafanya kwa ppp? kesi example- Mark Carney alipo ajiliwa na UK ili ku-stabilise pound wakati wa covid...

Timu ikifungwa sana - wanachobadili ni kocha basi.. huyo kocha akiimgia atajua cha kufanya- hivyp hivyo huko kwenye mashirika ya umma.

Kama issue ni technokogia- munamuweka mtaalaam wa hiyo kitu na munampa managemenyt yake, hivyo hivyo ktk kila sector.

Issue sio ppp bali ni management - wadokozi ni wengi na serikali imeshindwa kuwadhibiti, kitu ambacho private sector wanaweza maana hakuna mswalia mtume mdokozi akikamatwa huko sector binafsi.
Kila siku mnakimbilia ppp, kubalini kwamba mumeshindwa kuwadhibiti mafisadi ndio maana haya maneno ya CAG
kama hapa chini.
 
CCM wanatawa nchi yetu kwa mazoea - muda mufaka ushafika wapumzike.
Mtu kama wasira ana jipya lipi ndugu zangu kama si yale yale ya toka mwaka 47
 
Napenda sana ubia, lakini sio huu wa PPP ya sheria ya PPP ya kwetu ambayo inaneemesha tu upande mmoja na serikali kuwa kapeti jekundu Kwa tajiri

Hasara za haya mashirika nyingi zinatokana na business model na sio uwezo Mdogo au usimamizi mdogo wa wenye dhamana
1. Reli wao shida ni uwekezaji mkubwa wa miundombinu ambao Bado haujapata full utilization yake… pesa ilo chini
2. ATCL Haina hasara - ni mfumo tu wa umiliki wa ndege, wako Adili leo kesho inasimama faida
3. TTCL Bado Haina uhuru kamili wa maamuzi na usimamizi wa mali zake - wakipewa uhuru huo utasikia faida
 
Unamawazo mazuri lakini hujasema Nini kifanyike?
 
Unamawazo mazuri lakini hujasema Nini kifanyike?
Solutions zote zilo hapo
1. Two walishaambiwa wawe na engines sa kutosha… ilo kuongeza biashara na revenue, rhis year wamepokea mabehewa yq mizigo mengi sana na engines meaning hasara itapungua
2. ATCL ipewe ndege
3. TTCL waachwe na nalo zao
 
Umeongea point sana hii
 
Solutions zote zilo hapo
1. Two walishaambiwa wawe na engines sa kutosha… ilo kuongeza biashara na revenue, rhis year wamepokea mabehewa yq mizigo mengi sana na engines meaning hasara itapungua
2. ATCL ipewe ndege
3. TTCL waachwe na nalo zao
Kwa maana hiyo wewe huoni maana ya PPP
 
Kafulila ameiva sana kwenye uongozi kwa sasa
 
Kwa maana hiyo wewe huoni maana ya PPP
Kwa akili fupi huwezi elewa

Ppp has different models - ila hii ya kuwa off taker Haina maana na ndiyo tunayoitekeleza hapa

And we can see its failure, - a joint venture is a way to go

Ni model ya ppp lakini siyo ile ya kafulila
 
Kwa akili fupi huwezi elewa

Ppp has different models - ila hii ya kuwa off taker Haina maana na ndiyo tunayoitekeleza hapa

And we can see its failure, - a joint venture is a way to go

Ni model ya ppp lakini siyo ile ya kafulila
Ya Kafulila Iko chini Sheria Kafulila hana model yoyote
 
Huyu jamaa amepewa wimbo wa PPP hadi amebadilika kuwa chawa mzowefu..... Kwanini Serikali haitaki kupunguza umiliki wake kwenye mashirika yake yanayozalisha hasara kila mwaka kwa kuyaorodhesha kwenye soko la hisa? Kwa nini mashirika kama ATCL, TRC, Bandari, na mengineyo yasiuze hisa zake kwa wananchi ili wayamiliki wenyewe na kuyasimamia?

Kwa nini makampuni yaliokuwa mahututi kiutendaji miaka ya 90 yalipojiunga na soko la hisa na kuuza asilimia ya hisa zake kwa wawekezaji binafsi na wananchi, kwa nini yanafanya vizuri hadi leo? Makampuni binafsi kama CRDB, NMB Swissport, TCC TOL n.k Yanatumia mbinu gani kufanikiwa ambayo haionekani na huyo chawa Pro-Max wa PPP?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…