VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

Swala la nidhamu jeshini huwa halihitaji majadiliano, unapoelekezwa Jambo na mkuu wako (achilia mbali CDF) unatakiwa kufata Kwanza (hata Kama haliwezekani) ukashindwe ukiwa kwenye juhudi za kulifanya, unaweza ukaamrishwa ukapenye kwenye tundu la sindano na unapaswa kutafuta sindano uanze juhudi za kupenya na sio kuanza kujadili kwamba haiwezekani, like wise kijana uliyepata mafunzo ya kijeshi unaweza ukaahidiwa ajira na kesho ukaambiwa ile ajira haipo Tena unatakiwa utii na kuendelea kusubiri sio uanze kujadili kwamba ahadi ni Deni, kwa kuonesha utii unakujiwekea mazingira ya kuitwa kwenye ajira ya jeshi pindi nafasi ikijitokeza.
 
Inaonekana CDF Mabeyo ama mkuu wa JKT ndiyo wenye tatizo ama mmoja wao au wote juu ya hili jambo la vijana 850 waliotimuliwa baada ya kusaga ardhi vilivyo huko Msata kwa kosa la kuandamana.

Asikwambie mtu, hadi mtumishi wa ndani ya jeshi amefikia kuandamana ujue yamemfika shingoni kweli kweli. Siyo lelemama kama wengine wanavyodhani.

Any way muda utasema ila huenda CDF kwa hili ameficha jambo zito sana na upo uwezekano mkubwa kuwa hawa vijana walichoshwa kupita kiasi tena sana.

Zaidi soma: JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

View attachment 1755335
Mungu ibariki JF
 
Vijana wamepeleka mambo ya balehe na sekondari, kwa JKT??!!

Wacha yawakute yaliyowakuta...
Jeshini ni utiii!
Sir Yes Sir!

Ajira wanalipwa na nani??
Walikuwa wanawaona walimu na manesi wanaohaha mitaani ni mafala.
Warudi maisha yasonge tena washukuru, hawajafungwa kijeshi, huo ni uhaini!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
My point is,before hata hawajaingia kwenye hayo makubaliano ilikuwa sahihi kuwaweka kwenye mtego huo kuwa mfanye kazi kwanza ya kujenga ikulu kisha ndipo niwape ajira?ajira jeshini huwa zinatolewa KWA muktadha huo?,I just want to know
Nimekuelewa sana tena sana. Jiwe aliwapa mkataba huo na akatangaza kuwa wakimaliza tu waajiliwe....Roadside decree kama kawaida yake. Huyu amekuja akaona kuwa, kama unavyosema, kuwa jeshini hakuna mikataba kama hiyo. Lakini as long as waliingia mkataba na Jeshi, basi CDF has an obligation to discharge the terms of contract. Kwa hiyo unasema kuwa mkataba huo ulikuwa na elements zote za coercion, undue influence, fraud, misrepresentation, mistake etc, etc, etc, then ni batili na hawakupashwa kuwaingiza vijana kwenye mtego huo. SO WHAT IS THE WAY FORWARD?
 
Jeshi ni utii

Jeshi ni heshima

Jeshi hakuna kuhoji kabla ujafanya ulichoelekezwa

Jeshi halina siasa chama wala dini

Ni utovu wa nidhamu mkubwa sana wanajeshi kuandamana

Maandamano ni ya wanasiasa NGO's za kiraia makundi mengine but sio majeshi.

Alichokifanya Mabeyo namuunga mkono 100% lazima jeshi Liwe tiifu kwani ndio sifa namba moja ya kuwa mwanajeshi.
Kaka wanajeshi hawali UTII, kuna muda tuangalie hili jambo kwa jicho la KIUCHUMI wa mtu na familia zao.

Hivi mtu anayefanya UASI unamrudisha nyumbani? Something is fishy...
 
Kaka wanajeshi hawali UTII, kuna muda tuangalie hili jambo kwa jicho la KIUCHUMI wa mtu na familia zao.

Hivi mtu anayefanya UASI unamrudisha nyumbani? Something is fishy...
Kasema wangekuwa wameajiliwa na jeshi basi wangehukumiwa kijeshi na yuko sawa katika hili, jeshi lina sheria zake na mahakama za kijeshi. Tuseme hawa vijana walipewa ahadi lakini katika jeshi unafuata amri ya mkuu wako wala uhoji amri hata ukiwa vitani ni amri ndio jeshi sheria zake nidhamu 100%. Hawa vijana wameonesha tu hawafai kuwa wanajeshi maana wameshindwa mtihani ambao ni basic kabisa. Jeshi kukataa amri ya mkuu huo ni uasi, naunga mkono vijana wamechemka vibaya hata kama walipewa na ahadi.
 
Kwa kiapo cha Jeshi, askari wanamtii CDF. Yaani CDF akisema chochote, hawamsikilizi Rais.

Sasa hao wamefukuzwa na CDF mwenyewe, hivyo hata amri ya Rais haina nguvu.
ndio mnavyodanganyanaga hvyo mtaani?
 
Unamlaumu bure maana yeye alisema waajiliwe wakimaliza. Sasa CDF amebadili upepo, nani wa kulaumiwa?
Hao misukule wanyea mdomoni watakuchosha tu.. mzimu wa JPM unawatafuna kila uchao ndo maana wanahara kila wakisikia jinale.
 
Hao madogo wangekuwa wavumilivu kidogo tu wangekula shavu... sasa ujeuri umewaponza
 
Back
Top Bottom