VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Inaonekana CDF Mabeyo ama mkuu wa JKT ndiyo wenye tatizo ama mmoja wao au wote juu ya hili jambo la vijana 850 waliotimuliwa baada ya kusaga ardhi vilivyo huko Msata kwa kosa la kuandamana.

Asikwambie mtu, hadi mtumishi wa ndani ya jeshi amefikia kuandamana ujue yamemfika shingoni kweli kweli. Siyo lelemama kama wengine wanavyodhani.

Any way muda utasema ila huenda CDF kwa hili ameficha jambo zito sana na upo uwezekano mkubwa kuwa hawa vijana walichoshwa kupita kiasi tena sana.

Zaidi soma: JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Inaonekana CDF Mabeyo ama mkuu wa JKT ndiyo wenye tatizo ama mmoja wao au wote juu ya hili jambo la vijana 850 waliotimuliwa baada ya kusaga ardhi vilivyo huko Msata kwa kosa la kuandamana.

Asikwambie mtu, hadi mtumishi wa ndani ya jeshi amefikia kuandamana ujue yamemfika shingoni kweli kweli. Siyo lelemama kama wengine wanavyodhani.

Any way muda utasema ila huenda CDF kwa hili ameficha jambo zito sana na upo uwezekano mkubwa kuwa hawa vijana walichoshwa kupita kiasi tena sana.

View attachment 1755335
Kwa kiapo cha Jeshi, askari wanamtii CDF. Yaani CDF akisema chochote, hawamsikilizi Rais.

Sasa hao wamefukuzwa na CDF mwenyewe, hivyo hata amri ya Rais haina nguvu.
 
Usiamini sana alichokuwa anakisema jiwe muda mwingine alikuwa anajiropokea tu maneno yanayomjia akilini ili watu wampigie makofi na kumshangilia lakini sio kwamba alivyokuwa anavihaidi alikuwa amevikusudia hata kwenye elimu alisema ataajiri walimu 13 elfu kilichofuata baada ya hapo ni ajira elfu 8 tu ndizo zilitoka zingine zikapotea katika mazingira ya kutatanisha
 
Jeshi ni utii

Jeshi ni heshima

Jeshi hakuna kuhoji kabla ujafanya ulichoelekezwa

Jeshi halina siasa chama wala dini

Ni utovu wa nidhamu mkubwa sana wanajeshi kuandamana

Maandamano ni ya wanasiasa NGO's za kiraia makundi mengine but sio majeshi.

Alichokifanya Mabeyo namuunga mkono 100% lazima jeshi Liwe tiifu kwani ndio sifa namba moja ya kuwa mwanajeshi.
 
Mzee walio jenga kuta mbalimbali wapo walio nufaika na kuta hizo kupelekea kupata ajira na wapo ambao haikuwa bahati yao...

Kuta za melelani, ukonga magereza kama sikosei, ikulu chamwino etc watu wamepata ajira vizuri tu... Na wapo walio kosa...

Nafahamu wapo pia walio pata ajira za utumishi wa umma kama watendaji, walimu, madaktari etc...

Na wapo walio kosa... Hao hawakuwa wa kwanza kurejea nyumbani au kufanya mgomo, kuna wale waligomaga ikazua taflani kiongozi wao ikasemekana hakuonekana kwa muda, nazani ilikuwa ni kipindi cha mzee wa msoga

Baada ya hapo mgomo wao ulijbu waka pelekwa kwata msata kambi mpya...

Hawa waligoma na wala haikuwa ahadi bali saikolojia yao ya kurejea nyumbani ndio iliwapa hali ya kufanya maamuzi magumu ya mgomo...

Nidhamu jeshini na uti ni sehemu ya uzalendo kwa nchi na vyombo vilivyo kupa dhamana ya kulitumikia taifa (wananchi)
 
Mkuu hilo suala ni kwa mujibu wa wanajeshi wenyewe.

Kwamba wao wanamtii na kumsikiliza CDF.
Nadhani katika day to day activites/duties of wanajeshi. Linapokuja suala kuwa kuna mtanziko fulani, AJM na CDF .......anyway sijui
 
Kwa kiapo cha Jeshi, askari wanamtii CDF. Yaani CDF akisema chochote, hawamsikilizi Rais.

Sasa hao wamefukuzwa na CDF mwenyewe, hivyo hata amri ya Rais haina nguvu.
Kumbuka Rais ni Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama so husimlinganishe kabisa na huyu bwana mdogo CDF ambae boss wake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi
 
Back
Top Bottom