Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,086
- 2,823
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano.
Alisema Rais huyu anafanya mambo yaliyokataliwa na waasisi wa nchi hii ya kujali kabila lake kwanza.
Na tumeshuhudia Rais huyu wa sasa akipanda majukwaani na kuweka mbele Kisukuma bila kuzingatia misingi ya kuendeleza Utaifa mmoja, unaoongea lugha ya Taifa moja, lugha ya Kiswahili.
Tundu Lissu, kati ya watu wote, na yeye eti ameangukia mtego huo wa kuongea cha kwao majukwaani. Anatuangusha.
Mwalimu Nyerere anaviringika kaburini.