Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,086
- 2,823
- Thread starter
- #41
Ni kiongozi wa kitaifa, anafuatiliwa kila pembe ya nchi. Sawa kabisa...kweli.
..pamoja na kuchombeza kilugha, TL alitakiwa atafsiri ktk lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
..nayasema hayo kwa kuzingatia kwamba wako watu[wageni wake] waliomsindikiza kama Salum Mwalimu, Susan Kiwanga, etc ambao hawazungumzi Kinyaturu.
..pia tukio zima lilikuwa linafuatiliwa kila pembe za Tanzania hivyo ni vizuri wafuatiliaje waelewe kila lililozungumzwa.
Tundu Lissu sio Chifu wa Wanyaturu.
Wakati Rais Magufuli anaongea kuhusu Corona akiwa kanisani kwake Chato mbona hatukusema aaah bwana eeh, yuko kwao huko, anaongea Wasukuma wenzie! Tulimsikiliza.
Kwa sababu alikuwa anaongea na Taifa, ni kiongozi wa Kitaifa.
Jumamosi, akiwa nyumbani kwake Bedminster, New Jersey, Donald Trump amesaini amri kupitisha mambo ya dharura ya Corona mbali na Washington. Nchi nzima ilimsikiliza. Ni kiongozi wa Kitaifa.
Hatutegemei Tundu Lissu, kati ya watu wote duniani, awe na vitabia tabia vinavyotaka kufanana fanana na Magufuli.
Lissu ni mgombea Urais. Tunategemea awe na hulka, silka na mwenendo wa Urais. Rais wa Tanzania moja.
Julius Nyerere hakuwahi kumsalimia mama yake Kizanaki kama kuna Mnyakyusa mmoja kasimama pembeni.