VIDEO: Tundu Lissu, aliyepigwa risasi akipinga ukabila na u-Mobutu, na yeye aiga kuongea vilugha majukwaani

Ni kiongozi wa kitaifa, anafuatiliwa kila pembe ya nchi. Sawa kabisa.

Tundu Lissu sio Chifu wa Wanyaturu.

Wakati Rais Magufuli anaongea kuhusu Corona akiwa kanisani kwake Chato mbona hatukusema aaah bwana eeh, yuko kwao huko, anaongea Wasukuma wenzie! Tulimsikiliza.

Kwa sababu alikuwa anaongea na Taifa, ni kiongozi wa Kitaifa.

Jumamosi, akiwa nyumbani kwake Bedminster, New Jersey, Donald Trump amesaini amri kupitisha mambo ya dharura ya Corona mbali na Washington. Nchi nzima ilimsikiliza. Ni kiongozi wa Kitaifa.

Hatutegemei Tundu Lissu, kati ya watu wote duniani, awe na vitabia tabia vinavyotaka kufanana fanana na Magufuli.

Lissu ni mgombea Urais. Tunategemea awe na hulka, silka na mwenendo wa Urais. Rais wa Tanzania moja.

Julius Nyerere hakuwahi kumsalimia mama yake Kizanaki kama kuna Mnyakyusa mmoja kasimama pembeni.
 
Hawa jamaa wa kijani wakiishiwa hoja wanaenda kukoki bullets ndo upeo wao hapo ujue umeishia
 
Hata Nyerere alizungumza kizanaki kijijini kwake Butiama. Na kwenye hotuba zake kuna moja alisema "wote maniganyanza!" lakini pia alitoa tafsiri ya kiswahili.
Hii siyo hotuba kwa taifa, ni mazungumzo na wanakijiji wenzake. Haijalengwa kwa taifa zima, bado huu siyo mkutano wa kampeni.
Tatizo liko pale mtu mwenye mamlaka na vyombo vya umma vya habari vinavyorusha hotuba yake kwa taifa zima anapoamua kutumia kilugha chake huku akijua audience ni taifa zima kupitia media za taifa zilizoko pale.
 
Tv zenyewe za kuonyesha hazipo zimewekwa mifukoni sibora wanaangalia humu jf
 
Tatizo liko pale mtu mwenye mamlaka na vyombo vya umma vya habari vinavyorusha hotuba yake kwa taifa zima anapoamua kutumia kilugha chake huku akijua audience ni taifa zima kupitia media za taifa zilizoko pale.
hapo unamshusha mgombea wa chama kikubwa cha upinzani, Tundu Lissu, kwamba yeye akiongea Singida hasikilizwi na Taifa zima, unamfanya ni Diwani wa Singida Vijijini!

vyombo vilivyorusha hotuba ya Lissu sio "media za taifa" ?

audience iliyomfuatilia Lissu haikuwa ni audience ya taifa zima?

Lissu anagombea Urais, ajifunze kuenenda kitaifa, na asiige ya JPM.

Vichwa vya habari havipendezi....

 
Mn
Mnajitahidi sana sana kuokoteza maneno ya kijingakijinga.....
 
Anaongea kijijini kwake na wanakijiji wenzake, hata Nyerere alifanya hivyo. Haongei na taifa, hayuko kwenye kampeni, na wala siyo rais ndiyo useme kauli yake ni kauli ya serikali. Chombo kilichurusha hiyo clip siyo cha taifa, siyo TBC hiyo.
Kuna mahali pa kuenenda kitaifa, kinyumbani na kifamilia. Tofautisha hayo.
 
Hapa ndio umeonesha vizuri nani aliehusika kumshambulia Tundu Lissu, hukumu yake ipo, na Mungu ndie hakimu wa kweli.
Lilikuwa tukio la kusikitisha sana.
 
Zilikuwa zama ngumu
 
Zilikuwa zama ngumu
Wanamuomba awape tumehuru. Hivi historia ya wazazi wake nani anaijua? Mwenyekiti yeye katuonyesha Dad wake wamevaa 3-piece suit utotoni, Tundu je? Hata picha hakuna?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…