Video: Ubarikio wa mtoto wa Bilionea Mosha

Video: Ubarikio wa mtoto wa Bilionea Mosha

Sio kweli sema hujui tu hata huku katoliki mambo haya yapo. Tena kwa wakatoliki huo ubatizo unaweza ukafanyikia nyumbani kwa hiyo familia!
Kwa wachache saaana, tena kwa mapadre ambao nafikiri wameanza kukengeuka, ubatizo huwa unatangazwa kwa utaratibu wa pamoja kama ni msamaha, kama ni kwa mafunzo wanaandikishwa wanabatizwa kwa siku moja wote uwe tajiri, uwe masikini unabatizwa na wenzio labda hayo masherehe ndo myafanyie nyumbani.
Ubatizo wa nyumbani labda wa wagonjwa na mpako wa wagonjwa.
 
Japo sio sawa kulinganisha madhehebu tofauti yenye historia tofauti, misingi na taratib tofauti hivyo kila kitu lazima kitakuwa tofauti, labda usharika mmoja na mwingine ndani ya dayosisi hiyohiyo au dayosisi moja na nyingine ndani ya nchi moja hapo unaweza kusema hawa wanazingatia taratib "zetu" wale wanakiuka, hata hivyo kwenye mambo ya kutoa huduma hizi, makanisa yetu haya makubwa (rc na kkkt) huwa yako flexible sana, kuna kitu kinaitwa "busara za kichungaji" wanakitumia kuangalia mazingira yanayofaa kutoa huduma flani za kiroho bila kukinzana na mafundisho ya kanisa wala ya kijamii, kwa hili ya kubatiza, ndoa, kipaimara, hakuna kosa lolote limefanywa na mchungaji kiongozi wala wazazi wa mtoto wala viongozi wa usharika, huduma iliyotolewa kwa mtoto wa tajiri inaweza kutolewa vilevile kwa mtoto wa fukara, tofauti ni kuwa ya mtoto wa tajiri tutajua, ya masikini itafanyika kimyakmya, lakini huduma ni ileile, masikini tuache chuki kwa matajiri, na matajiri waache dharau kwa masikini, mbingu ni yetu sote, na moto pia.
 
Nina abudu kkkt, hawa jamaa ukiwa na hela unapata special treatment kuanzia ubatizo/kipaimara/Ndoa/hadi Ibada yako ya mazishi

Najitahidi kwenda nao sawa ili tusitengwe tukifa

Kwahiyo michango ya Ujenzi/kutunza watumishi n.k unachomoa kibunda unawapa
Popote pale ukiwa na hela treatment yako inakua tofauti na asiye na pesa, si hata ww ulionaa mwili wa Mzee Mengi ulipelekwa Lugalo lakini wa Ulomi ulipelekwa Mwananyamala

🦾🦾Nimefurahi kujua we ni mshirika mwenzangu
 
Jana nimeshangaa kuona ubarikio wa mtoto wa Bilionea Knyama KKKT peke yake tofauti na wenzetu huko Katoliki ambako ratiba ya komunio/kipaimara ni kwa wote (bila kujali kipato cha mzazi/mlezi) na sio mmoja mmoja. Shkamoo Mangi

View attachment 3182057
Kanisa Moja Katoliki la Mitume hawawezi kufanya ujinga kama huo.
 
Back
Top Bottom