Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?


Umeandika: Niliwahi kuuliza humu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Hii si ndoa huu ni uvamizi unaoitwa muungano na haupo halali kisheria

KAMA NI NDOA hii itakuwa ni ndoa ya mashoga
 
Mkuu Stuxnet , kwanza heshima yako, maana watu wa 60s humu tuko countable, tunahesabika. Pili Wazalendo wa aina yako, humu ni wa kutafuta kwa touchi!.

Asante sana, ubarikiwe sana!.

P
 
Umeandika: Niliwahi kuuliza humu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Hii si ndoa huu ni uvamizi unaoitwa muungano na haupo halali kisheria

KAMA NI NDOA hii itakuwa ni ndoa ya mashoga
Yes Muungano japo haukuhalalishwa kisheria kule Zanzibar kwa kufanyika process ya Ratification, Muungano ni halali by performance.

Hata ubakaji ni kosa la jinai, lakini mwanamke akibakwa, akashika, akasaamua kuishi na mbakaji, atahesabika ameridhia!, hivyo hakuna tena kesi ya ubakaji, kilichopo ni maridhiano!. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

The same applies to Muungano

P
 

Sasa kama Zanzibar ina 2.045 sq.km inakuwaje mnakuja kutuuwa kila ufikapo uchaguzi , kujaribu kuweka vibaraka vyenu si mtuwache tupumuwe mshughulike na nchi yenu iliyo kubwa ??
 


Performance ya muungano ndio hii , Pascal labda wewe unaona sawa na nzuri kwa sababu wanaoumia si watu wako


View: https://www.youtube.com/watch?v=gmxrblkDnbc&t=38s&pp=ygVEa2lsaWNob3dhcGF0YSB3YWxpb3dla3dhIGt3ZW55ZSB2aXp1aXppIHZ5YSBtYXRlc28gdWNoYWd1emkgemFuemliYXI%3D ??
 

Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Jibu ni Ndiyo ni Nchi.​

Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Jibu ni Wazanzibar.​

Zanzibar = Pemba + Unguja - Hii bado ipo before and after 1964
Tanganyika = Before 1964
Tanzania = Zanzibar + Tanganyika(After 1964) - Haina Ardhi ipo kwenye makaratasi.

Kwahiyo watu wanaoishi sehemu hizo ni Watanganyika na wazanzibar.

Kwa nje sisi wote ni watanzania ila kwa ndani tunajitambulisha kama mimi mndengereko,mazaramo,mdigo,mtumbnatu ,mkojani etc
 
Ili kukata mzizi wa fitna juu ya muungano kuna haja ya kuitishaa kura ya maoni ili Wazanzibari waamue kama bado wanauhitaji muungano na pia wabara waamue kama bado wanauhitaji muungano. Iwapo pande mojawapo itakataa muungano basi muungano huu utavunjika rasmi.
 
Tanganyika ipatikane hilo ndo la msingi. Huenda hata kupotea kwa Tanganyika tumepata matatizo mengi ya kiroho kama Watanganyika.
 
Wananchi wa Zanzibar wana Katiba yao, Rais wao na Jeshi lao JKU. Wakati wananchi wa Mwanza wana mkuu wa mkoa tu!.
Hapa tumepigwa za uso
Kiusahihi, hakuna Wananchi wa Mwanza au Mbeya. Ni wakazi wa Mwanza au Wakazi wa Mbeya. Unaposema Wananchi unamaanisha wana nchi fulani. Ni sahihi kusema wananchi wa Tanzania, wananchi wa Kenya n.k. Lakini huwezi kusema Wananchi wa Mwanza au Wananchi wa Nairobi bali unatakiwa kusema Wakazi wa Mwanza au wakazi wa Nairobi.

Kwa hiyo kusema Wananchi wa Zanzibar ni kukubaliana kuwa Zanzibar ni nchi ...!!
 

Kura ya maoni hiyo isimamiwe na CCM , labda kijana unaota usingizi wa mchana.

Huu si muungano ni uvamizi na ujanja ujanja wa Nyerere katika jitihada zake za kuimeza Zanzibar .
Ni kuvunjwa kila mtu akajenga nchi yake katika hali ya ujirani mwema kama tulivyo kwa Kenya , uganda na mataifa jirani. Full stop hakuna haja ya kuwekeana chuki na kuja kutuuwa kila ufikapo uchaguzi
 
Mkuu mimi na wewe hatuna tofauti sana ya umri, G55 Nyerere aliitupilia mbali kwani aligundua ilikuwa na chembechembe za chuki dhidi ya urais wa Hayati Ali Mwinyi.

Hoja imezaliwa tena mwaka huu baada ya Samia kuwepo ikulu kwa miaka mitatu, chanzo chake ni hisia potofu za baadhi yetu kudhani kuwa DP World ni ndugu zake Samia kwa hiyo anatengeneza mazingira ya kuiibia Tanzania wanasahau kuwa hawa DP World wapo Ubelgiji, India na Marekani pia, wameshindwa kuiona hoja pana ya kiuchumi na faida za nchi yetu kuwa na waendeshaji wenye umahiri kwa ajili ya bandari zetu wameishia kutengeneza hoja yenye msingi wa kibaguzi nadhani sababu ni elimu zetu kuwa ndogo.

Hayati JPM angekuwa hai mpaka muda huu usingesikia lolote kuhusu masuala ya kuhoji uhalali wa muungano.
 
Sasa kama Zanzibar ina 2.045 sq.km inakuwaje mnakuja kutuuwa kila ufikapo uchaguzi , kujaribu kuweka vibaraka vyenu si mtuwache tupumuwe mshughulike na nchi yenu iliyo kubwa ??
Mbona wewe hujakufa ? Ndiyo maana upo humu unajibu!!
 
Siyo kweli. Umesoma vibaya alipoandika Samuel Sitta au Sitta alijielekeza vibaya. Jina Tanzania lilianza kutumika Novemba 1, 1964.

 
Kama ndivyo Tume ya Uchaguzi ilikuwa wapi? Ama Katiba yetu ina semaje.

Usanii wa Nyerere ndio tatizo , na mzimu wake bado unaogopesha watu kuamua Zanzibar kuwa huru .

Hakuna muungano kuna uvamizi na viroja vya Nyerere tu kujaribu kutaka kuimeza zanzibar kiaina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…