Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Huu ndio ukweli wa mambo, tena sio wanahisi tumewaoa, bali huyo mwanamke ndie alijitongozesha, akajibebisha, Mzee Tanganyika akachukua ngoma, akaoa, akatia ndani, analisha, anatunza, anagharimia kila kitu, mke kazi kupendeza tuu, kila kitu bure!.

Niliwahi kuuliza humu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Tanzania itakuwa na wanaume wa ajabu wanao ona wivu na wake zao kwa kutamani wawe sawa kwa sawa!.
Mwacheni mkeo apendeze. Mpe kila anachokitaka!.

P

Umeandika: Niliwahi kuuliza humu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Hii si ndoa huu ni uvamizi unaoitwa muungano na haupo halali kisheria

KAMA NI NDOA hii itakuwa ni ndoa ya mashoga
 
Naunga mkono hoja. Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.

Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.

Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Ta ganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.

Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres, its absurd and weird
Mkuu Stuxnet , kwanza heshima yako, maana watu wa 60s humu tuko countable, tunahesabika. Pili Wazalendo wa aina yako, humu ni wa kutafuta kwa touchi!.

Asante sana, ubarikiwe sana!.

P
 
Umeandika: Niliwahi kuuliza humu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Hii si ndoa huu ni uvamizi unaoitwa muungano na haupo halali kisheria

KAMA NI NDOA hii itakuwa ni ndoa ya mashoga
Yes Muungano japo haukuhalalishwa kisheria kule Zanzibar kwa kufanyika process ya Ratification, Muungano ni halali by performance.

Hata ubakaji ni kosa la jinai, lakini mwanamke akibakwa, akashika, akasaamua kuishi na mbakaji, atahesabika ameridhia!, hivyo hakuna tena kesi ya ubakaji, kilichopo ni maridhiano!. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

The same applies to Muungano

P
 
Naunga mkono hoja. Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.

Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.

Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Ta ganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.

Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres, its absurd and weird

Sasa kama Zanzibar ina 2.045 sq.km inakuwaje mnakuja kutuuwa kila ufikapo uchaguzi , kujaribu kuweka vibaraka vyenu si mtuwache tupumuwe mshughulike na nchi yenu iliyo kubwa ??
 
Yes Muungano japo haukuhalalishwa kisheria kule Zanzibar kwa kufanyika process ya Ratification, Muungano ni halali by performance.

Hata ubakaji ni kosa la jinai, lakini mwanamke akibakwa, akashika, akasaamua kuishi na mbakaji, atahesabika ameridhia!, hivyo hakuna tena kesi ya ubakaji, kilichopo ni maridhiano!. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

The same applies to Muungano

P

Performance ya muungano ndio hii , Pascal labda wewe unaona sawa na nzuri kwa sababu wanaoumia si watu wako

View: https://www.youtube.com/watch?v=gmxrblkDnbc&t=38s&pp=ygVEa2lsaWNob3dhcGF0YSB3YWxpb3dla3dhIGt3ZW55ZSB2aXp1aXppIHZ5YSBtYXRlc28gdWNoYWd1emkgemFuemliYXI%3D ??
 
Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Jibu ni Ndiyo ni Nchi.​

Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Jibu ni Wazanzibar.​

Zanzibar = Pemba + Unguja - Hii bado ipo before and after 1964
Tanganyika = Before 1964
Tanzania = Zanzibar + Tanganyika(After 1964) - Haina Ardhi ipo kwenye makaratasi.

Kwahiyo watu wanaoishi sehemu hizo ni Watanganyika na wazanzibar.

Kwa nje sisi wote ni watanzania ila kwa ndani tunajitambulisha kama mimi mndengereko,mazaramo,mdigo,mtumbnatu ,mkojani etc
 
Ili kukata mzizi wa fitna juu ya muungano kuna haja ya kuitishaa kura ya maoni ili Wazanzibari waamue kama bado wanauhitaji muungano na pia wabara waamue kama bado wanauhitaji muungano. Iwapo pande mojawapo itakataa muungano basi muungano huu utavunjika rasmi.
 
Tanganyika ipatikane hilo ndo la msingi. Huenda hata kupotea kwa Tanganyika tumepata matatizo mengi ya kiroho kama Watanganyika.
 
Wananchi wa Zanzibar wana Katiba yao, Rais wao na Jeshi lao JKU. Wakati wananchi wa Mwanza wana mkuu wa mkoa tu!.
Hapa tumepigwa za uso
Kiusahihi, hakuna Wananchi wa Mwanza au Mbeya. Ni wakazi wa Mwanza au Wakazi wa Mbeya. Unaposema Wananchi unamaanisha wana nchi fulani. Ni sahihi kusema wananchi wa Tanzania, wananchi wa Kenya n.k. Lakini huwezi kusema Wananchi wa Mwanza au Wananchi wa Nairobi bali unatakiwa kusema Wakazi wa Mwanza au wakazi wa Nairobi.

Kwa hiyo kusema Wananchi wa Zanzibar ni kukubaliana kuwa Zanzibar ni nchi ...!!
 
Ili kukata mzizi wa fitna juu ya muungano kuna haja ya kuitishaa kura ya maoni ili Wazanzibari waamue kama bado wanauhitaji muungano na pia wabara waamue kama bado wanauhitaji muungano. Iwapo pande mojawapo itakataa muungano basi muungano huu utavunjika rasmi.

Kura ya maoni hiyo isimamiwe na CCM , labda kijana unaota usingizi wa mchana.

Huu si muungano ni uvamizi na ujanja ujanja wa Nyerere katika jitihada zake za kuimeza Zanzibar .
Ni kuvunjwa kila mtu akajenga nchi yake katika hali ya ujirani mwema kama tulivyo kwa Kenya , uganda na mataifa jirani. Full stop hakuna haja ya kuwekeana chuki na kuja kutuuwa kila ufikapo uchaguzi
 
Una Miaka Mingapi Kijana?
Hoja ya Muungano Imejadiliwa kila mwaka tangu G55, Mtilila na wengine kibao Kina maalimu Seif Abdu Jumbe na watu wote waliokuwa wakijadili nini Sio Muungano??

Steven Uislam wa mama Samia Sijaona watu wakiuhoji hata mara moja labda wewe ndo uanzishe hiyo Mada..

Kama ilivyo Ukristo wa mkapa Au Ukristi wa Magufuli au Uislamu wa Kikwete au Uislamu wa Mwinyi haukuwahi kujadiliwa Vivo hivyo hata sasa!

Kwanini tusijibu hoja kuliko Kuanzisha Hoja
Mkuu mimi na wewe hatuna tofauti sana ya umri, G55 Nyerere aliitupilia mbali kwani aligundua ilikuwa na chembechembe za chuki dhidi ya urais wa Hayati Ali Mwinyi.

Hoja imezaliwa tena mwaka huu baada ya Samia kuwepo ikulu kwa miaka mitatu, chanzo chake ni hisia potofu za baadhi yetu kudhani kuwa DP World ni ndugu zake Samia kwa hiyo anatengeneza mazingira ya kuiibia Tanzania wanasahau kuwa hawa DP World wapo Ubelgiji, India na Marekani pia, wameshindwa kuiona hoja pana ya kiuchumi na faida za nchi yetu kuwa na waendeshaji wenye umahiri kwa ajili ya bandari zetu wameishia kutengeneza hoja yenye msingi wa kibaguzi nadhani sababu ni elimu zetu kuwa ndogo.

Hayati JPM angekuwa hai mpaka muda huu usingesikia lolote kuhusu masuala ya kuhoji uhalali wa muungano.
 
Sasa kama Zanzibar ina 2.045 sq.km inakuwaje mnakuja kutuuwa kila ufikapo uchaguzi , kujaribu kuweka vibaraka vyenu si mtuwache tupumuwe mshughulike na nchi yenu iliyo kubwa ??
Mbona wewe hujakufa ? Ndiyo maana upo humu unajibu!!
 
Tanzania Ili Cease mwaka 1965..
Mkuu Wewe umesema Umezaliwa mwaka 1960 lakini cha Ajabu Historia umeshindwa Kuielewa?

We kwangu ni kaka maa mimi nimezaliwa Mwaka 1972 kwa hyo unanizidi naomba nitumie Lugha ya Busara kwa kuwa naongea na Kaka Yangu!

Mwaka 1964 Tanganyika na zanzibar ziliungana..
Ila mwaka 1965 ilifanyika Decree ya Kubadili Jina Kutoka Tanganyika kwenda Tanzania pamoja na Wizara zote za Tanganyika Nembo za Tanganyika na hata Viongozi wa Tanganyika na Rasilimali za Tanganyika kuwa za Muungano..

Decree hizo tatu zinapatikana kwenye Vitabu vya Samweli sita Unaweza ukavisoma pia..

Tanganyika Ni Tanzania Ya sasa Iliyojivika Koti la Muungano..

kuna vitu vichache ambavyo ni Vigumu kuvijua kama Ukikumbatia Mapenzi ya Chama au Ya siasa..

Mimi ni Mwana CCM Die hard kabisa..
Ila linapokuja swala la Muungano huwa naweka pembeni hisia nafata Facts..

Umezungumza Kuhusu Hoja za watu..
Ila hujazijibu hata Moja..

Kitu kigumu kinachoiwazisha Serikali Yangu ni kwamba Siku Muungano utakapovunjika Ndio Mwisho wa CCM..

Maana Tukumbuke CCM ni muunganiko wa TANGANYIKA (TANU) NA Zanzibar (ASP)..

Sasa kukitokea Mvunjiko Tutaivunja CCM kurudi kwenye TANU..

Na huu Ndo Muungano wenyewe NA KUUVUNJA NI NGUMU SANA
View attachment 2991515
Siyo kweli. Umesoma vibaya alipoandika Samuel Sitta au Sitta alijielekeza vibaya. Jina Tanzania lilianza kutumika Novemba 1, 1964.

Screenshot_20240516_145221_Facebook.jpg
 
Kama ndivyo Tume ya Uchaguzi ilikuwa wapi? Ama Katiba yetu ina semaje.

Usanii wa Nyerere ndio tatizo , na mzimu wake bado unaogopesha watu kuamua Zanzibar kuwa huru .

Hakuna muungano kuna uvamizi na viroja vya Nyerere tu kujaribu kutaka kuimeza zanzibar kiaina.
 
Back
Top Bottom