Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

..umetoka hoja nzuri sana zenye data.

..sasa kama Tanganyika ni 945,000 sq km, na Zanzibar ni 2,045 sq km, sisi Watanganyika tumekosa nini mpaka tu-sacrifice utaifa na utambulisho wetu ili tuungane na kanchi kadogo hivyo?

..Sisi Watanganyika tumepungukiwa nini, mpaka tuhitaji kuungana na Zanzibar, na kuwaruhusu watutawale, na kutuingilia ktk maamuzi ya nchi yetu? Muungano unatuongezea nini?
 
..Zanzibar ni nchi.

..tena wana Katiba yao inayosema " Zanzibar ni nchi ... "
 
Sasa huoni kuwa hapo Wazanzibari hawautaki? Ni Watanganyika ndio wanaolazimisha chini ya mwamvuli wa muungano ?

..wanaolazimisha ni CCM.

..Na humo wamo baadhi ya Watanganyika, na baadhi ya Wazanzibari.

..Tanganyika ikirejeshwa, italazimisha kuandikwa upya kwa Katiba, na Sheria zetu, kitu ambacho kitakwenda kupunguza madaraka ambayo CCM wanayo.
 
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P
Hapa unakosea, Zanzibar ina Rais, ina bendera yake, ina katiba yake na ina raia wake wanaitwa Wazanzibari, unasemaje Zanzibar siyo nchi, eti ni sehemu ya JMT? Tanzania ilitoka wapi? Zanzibar ipo Tanganyika haipo, ili tuwe sawa Zanzibar ipotee.
 
..Zanzibar ni nchi.
..tena wana Katiba yao inayosema " Zanzibar ni nchi ... "
Mkuu JK JokaKuu , ndio maana nimewashauri humu, elimu ya uraia kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu inahitajika hata kwa watu kama wawe.

1. Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

2. Maneno ya Zanzibar ni nchi, kwenye katiba ya Zanzibar ni mambo ya ndani ya Zanzibar, katiba ya JMT haiitambui katiba ya Zanzibar, kiukweli nchi ni moja tuu ya JMT na uraia ni mmoja tuu, uraia wa Tanzania.

P
 
Wewe umfundishe nani uraia bana acha unafiki wa kupindisha uhalisia kwani nyie waramba asali mkoje..wewe hauna haki ya kutusemea ukweli tunao ujua bana... Tanganyika is Tanganyika and Zanzibar Will remain to be Zanzibar
 
Security transcends all reasons
 
..wanaolazimisha ni CCM.

..Na humo wamo baadhi ya Watanganyika, na baadhi ya Wazanzibari.

..Tanganyika ikirejeshwa, italazimisha kuandikwa upya kwa Katiba, na Sheria zetu, kitu ambacho kitakwenda kupunguza madaraka ambayo CCM wanayo.
Tuungane kwenye EAC unatosha. Kila mtu aende kivyake yaishe maneno na kuuliwa Wazanzibari.
 
Tanganyika ina autonomy ya mambo yake ya ndani?.
 
Security transcends all reasons

..sio kweli kwamba Znz ni tishio la usalama wa Tanganyika, au majirani zake wengine.

..Na kama ni tishio tungeweza kuwasaidia kujilinda kama tulivyosaidia Comoro na Shelisheli, na sio kusalimu amri kwao, na kuua utaifa wetu.
 
Tumesalimu kwao kivipi? Wakati marais wote tunawapangia huku Bara?
 
Kwani ili nchi iitwe nchi ni vigezo gani vinaangaliwa.mkitupa hivi vigezo tutakuwa pamoja.
 
Sasa umeeleweka juu ya zanzibar kiukweli chuki imekujaa juu ya zanzibar na hutamani hata uwepo wa zanzibar lakini ishatokezea tu na huna uwezo wa kuifuta hata nyerere alisema kama angekuwa na uwezo angevitupa mbali sana na tanganyika
w
 
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P
Watu wanakatiba yao bado mnazungumzia ukazi naserikali yao ya mseto ,JMT kuna mseto wa serikali?
 
Ndio maana sisi vijana wa buku mbili tunamtambua pombe kama Baba wa Taifa
 
Ubaya hawapendi tuongelee muungano

Ila ukweli ni kwamba dhoruba ndio usalama wa samaki kutovuliwa
 
Mkuu una shida sana wewe,bora ungebaki Mzilankende kuliko kusumbua Watanganyika wasio na hatia.Mnatukosea sana kwa elimu hizi za kudidimiza haki za upande mmoja wa Muungano na kuinua haki za upande mwingine kisa tu wanazungukwa na bahari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…