Naunga mkono hoja. Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.
Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.
Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Ta ganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.
Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres, its absurd and weird
..umetoka hoja nzuri sana zenye data.
..sasa kama Tanganyika ni 945,000 sq km, na Zanzibar ni 2,045 sq km, sisi Watanganyika tumekosa nini mpaka tu-sacrifice utaifa na utambulisho wetu ili tuungane na kanchi kadogo hivyo?
..Sisi Watanganyika tumepungukiwa nini, mpaka tuhitaji kuungana na Zanzibar, na kuwaruhusu watutawale, na kutuingilia ktk maamuzi ya nchi yetu? Muungano unatuongezea nini?