Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Hiyo ya Wananchi wa Zanzibar imekaaje .....!!?

Hivi kusema Wananchi wa Mwanza, Wananchi wa Mbeya au Wananchi wa Moshi ni sawa pia....!!?
WaZanzibar wana Katiba yao, Rais wao na Jeshi lao JKU. Wakati watanganyika wote hatuna Rais wala katiba!.
Hapa tumepigwa za uso
 
Mimi nimezaliwa Tanzania, na wengi wetu tumezaliwa Tanzania, waliozaliwa Tanganyika wote by now ni wastaafu, wako over 60 years, na walipopata akili, walikuwa tayari Tanzania, ni Watanganyika gani hao wa kuililia Tanganyika na kujivunia Tanganyika?.

Muungano ni kama ndoa, Zanzibar ni kama mwenza, sasa wewe kama mwenza wako anajipodoa, na wewe utataka kujipodoa ili mlingane?. Hebu acheni hizi kitu!.
P
Naunga mkono hoja. Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.

Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.

Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Ta ganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.

Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres, its absurd and weird
 
View attachment 2991056
Ndugu wana JF - Jukwaa la Siasa;

Mjadala wa muungano tata wa Tanganyika na Zanzibar (1964) unaendelea tena leo....

Na kwa kweli mjadala huu haupaswi kuishia njiani isipokuwa tu wote tumeelewana na kukubali kuwa lipo tatizo ktk muungano huu linalostahili kutatuliwa sasa na sio kesho kama tunataka kuendelea nao...

Leo katika video hiyo☝🏻☝🏻 ni makala ya uchambuzi toka kwa mchambuzi nguli wa maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ndugu Ansbert Ngurumo kupitia YouTube channel yake [SK Media Online TV] anayeishi uhamishoni Uingereza

Katika uchambuzi huu, Ansbert Ngurumo anazimulika kauli za watu watatu juu muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964) ambao ni;

1. Mzee Steven Wassira a.k.a Tyson (CCM)
2. Rais Samia Suluhu Hassan (CCM)

3. Tundu Antipasy Lissu (CHADEMA)

Hawa wote wanajibu maswali mawili muhimu yafuatayo ambayo ndiyo msingi mkuu wa ubishani unaoendelea sasa ktk muungano huu;

1. KWAMBA, Zanzibar ni nchi au sio nchi?

2. KWAMBA, Watu au wananchi wa nchi ya Zanzibar ni Watanzania au Wazanzibari?

Nani mkweli kati ya hawa watu watatu kuhusu muungano wetu? Nini maoni yako? Tatizo liko wapi? Ni kitu gani kinafichwa kupitia muungano huu?

Tazama na sikiliza video hiyo ya dakika 14 tu hadi mwisho kisha tumia akili yako kupima mwenyewe halafu sema kitu.

Na bila shaka kasi ya internet imeboreka kiasi chake na hivyo kila mtu ataifungua video hii bila kuhangaika sana..
==========================================
Tanzania imeingia kwenye matumizi ya Akili Mnembe AI, wakati humu jukwaani bado tunahoji masuala ya muungano!.

Mada nyingi zinaanza na kuishia humu humu jukwaani, huko mtaani hali ni tofauti kabisa.
 
Wana Rais,wimbo wa Taifa,bendera,bunge,baraza la mawaziri,mipaka,ni vile tu hawana kiti UN ila ni nchi kamili
Vyote hivyo ulivyovitaja ni sawa na midoli inayomilikiwa na mwanao wa miaka 4 nyumbani.

Unatishika na midoli?
 
Naunga mkono hoja. Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.

Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.

Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Ta ganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.

Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres, its absurd and weird
Wengi wanaunga mkono Tanganyika kwa sababu ya chuki kwa Samia na haswa uislamu wake. Kuhoji juu ya Tanganyiko ni kificho tu cha chuki zao dhidi ya uislam wa Rais.

Magufuli angekuwa hai mpaka leo usingesikia hoja hizi zikijadiliwa, ni hawa hawa waliomtazama Samia kama mtu anayeleta waarabu pale bandarini wakishindwa kuona kuwa ni suala lililo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM, Chuki zinawapofusha.
 
United States of Tanzania !!??
Hii Ni ngumu sana!
Labda The United Federation of Tanganyika and Zanzibar...
Au The United Federal Government Of Tanzania..

Ni Vigumu kuwa na United states of Tanzania kwa sababu ya Tulivyorithishana na Imani zetu kuhusu Hizi nchi mbili zanzibar Wanataka Nchi yao na Tanganyika wanataka Nchi yao kamili..

Kama Ilivyokuwa Puerto rico
 
Wengi wanaunga mkono Tanganyika kwa sababu ya chuki kwa Samia na haswa uislamu wake. Kuhoji juu ya Tanganyiko ni kificho tu cha chuki zao dhidi ya uislam wa Rais.

Magufuli angekuwa hai mpaka leo usingesikia hoja hizi zikijadiliwa, ni hawa hawa waliomtazama Samia kama mtu anayeleta waarabu pale bandarini wakishindwa kuona kuwa ni suala lililo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM, Chuki zinawapofusha.
You have hit the jackpot 🎰 🙏 !
 
Naunga mkono hoja. Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.

Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.

Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Ta ganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.

Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres, its absurd and weird
Tanzania Ili Cease mwaka 1965..
Mkuu Wewe umesema Umezaliwa mwaka 1960 lakini cha Ajabu Historia umeshindwa Kuielewa?

We kwangu ni kaka maa mimi nimezaliwa Mwaka 1972 kwa hyo unanizidi naomba nitumie Lugha ya Busara kwa kuwa naongea na Kaka Yangu!

Mwaka 1964 Tanganyika na zanzibar ziliungana..
Ila mwaka 1965 ilifanyika Decree ya Kubadili Jina Kutoka Tanganyika kwenda Tanzania pamoja na Wizara zote za Tanganyika Nembo za Tanganyika na hata Viongozi wa Tanganyika na Rasilimali za Tanganyika kuwa za Muungano..

Decree hizo tatu zinapatikana kwenye Vitabu vya Samweli sita Unaweza ukavisoma pia..

Tanganyika Ni Tanzania Ya sasa Iliyojivika Koti la Muungano..

kuna vitu vichache ambavyo ni Vigumu kuvijua kama Ukikumbatia Mapenzi ya Chama au Ya siasa..

Mimi ni Mwana CCM Die hard kabisa..
Ila linapokuja swala la Muungano huwa naweka pembeni hisia nafata Facts..

Umezungumza Kuhusu Hoja za watu..
Ila hujazijibu hata Moja..

Kitu kigumu kinachoiwazisha Serikali Yangu ni kwamba Siku Muungano utakapovunjika Ndio Mwisho wa CCM..

Maana Tukumbuke CCM ni muunganiko wa TANGANYIKA (TANU) NA Zanzibar (ASP)..

Sasa kukitokea Mvunjiko Tutaivunja CCM kurudi kwenye TANU..

Na huu Ndo Muungano wenyewe NA KUUVUNJA NI NGUMU SANA
20240516_102006.jpg
 
Wengi wanaunga mkono Tanganyika kwa sababu ya chuki kwa Samia na haswa uislamu wake. Kuhoji juu ya Tanganyiko ni kificho tu cha chuki zao dhidi ya uislam wa Rais.

Magufuli angekuwa hai mpaka leo usingesikia hoja hizi zikijadiliwa, ni hawa hawa waliomtazama Samia kama mtu anayeleta waarabu pale bandarini wakishindwa kuona kuwa ni suala lililo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM, Chuki zinawapofusha.
Una Miaka Mingapi Kijana?
Hoja ya Muungano Imejadiliwa kila mwaka tangu G55, Mtilila na wengine kibao Kina maalimu Seif Abdu Jumbe na watu wote waliokuwa wakijadili nini Sio Muungano??

Steven Uislam wa mama Samia Sijaona watu wakiuhoji hata mara moja labda wewe ndo uanzishe hiyo Mada..

Kama ilivyo Ukristo wa mkapa Au Ukristi wa Magufuli au Uislamu wa Kikwete au Uislamu wa Mwinyi haukuwahi kujadiliwa Vivo hivyo hata sasa!

Kwanini tusijibu hoja kuliko Kuanzisha Hoja
 
Wengi wanaunga mkono Tanganyika kwa sababu ya chuki kwa Samia na haswa uislamu wake. Kuhoji juu ya Tanganyiko ni kificho tu cha chuki zao dhidi ya uislam wa Rais.

Magufuli angekuwa hai mpaka leo usingesikia hoja hizi zikijadiliwa, ni hawa hawa waliomtazama Samia kama mtu anayeleta waarabu pale bandarini wakishindwa kuona kuwa ni suala lililo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM, Chuki zinawapofusha.
Unazingua kuingiza udini bora useme uzanzibari wake,hakuna mwenye shida ya uislam au ukristo wa mtu,JPM alikuwa gaidi usingethubutu kuongea ongea angekuua
 
Kwa hiyo shida ya "kutojitambua" iko upande wetu wa pili yaani Tanganyika..

Tanganyika na Watanganyika wako wapi?

Jina halisi la nchi hii kumbe linapaswa kuwa ni

"Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar"

na siyo

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Hili jina la "Tanzania" ilitoka wapi? Shida iko kweye jina hili. Uchawi uko humu ndani ya jina hili. Inawezekana vipi kiongozi mmoja anayeitwa "Julius Kambarage Nyerere" abadili jina la nchi na uraia wetu bila ya ridhaa ya wananchi wenyewe??

Huu ni wakati wa kuhoji maamuzi ya huyu aitwaye baba wa taifa hili Mwl Julius K. Nyerere..

Kuna maamuzi yake mengine mengi yalikuwa very fatal na ya hovyo sana na yanahitaji kurekebishwa sasa au kuachana nayo kabisa maana ni mitego ya mauti na kikwazo cha ustawi wetu kama taifa na nchi..

Huu wote ni udanganyifu wa Nyerere katika jitihada zake za kuhalalaisha UVAMIZI wake kwa Zanzibar
 
Wana Rais,wimbo wa Taifa,bendera,bunge,baraza la mawaziri,mipaka,ni vile tu hawana kiti UN ila ni nchi kamili

Imetokea hivyo kwa sababu wale Waliowekwa na Nyerere wakati wa Uvamizi walikuwa kilinda ulaji wao wa madaraka na upande wapili walikuwa wakimtegemea Nyerere kulinda madaraka yao.

Ni unafiki mtupu hata hakuna kinachoeleweka nchi, si nci ni mkoa si mkoa , LAANA TUPU YA MAPINDUZI NA UVAMIZI
 
Katiba ya Zanzibar ibara ya kwanza inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi, halafu wewe unasema Zanzibar siyo nchi !!!
Kwa maana halisi ya katiba, katiba ni katiba ya JMT inayosema Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT. Aliyesema Zanzibar sio nchi sio mimi, ni katiba ya JMT.
Hivi kati ya wewe na Katiba ya nchi ya Zanzibar nani mkweli? Nani asikilizwe?
Katiba ya JMT haitambui katiba ya Zanzibar, hivyo mimi ndie mkweli, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani!.

Kwa vile Zanzibar ina uhuru na utawala wake wa ndani, katiba ya Zanzibar na kujiita ni nchi, ni mambo yao ya ndani, sisi hayatuhusu!, ukiwa ndani kwako, uko huru kufanya chochote, hata kujiita vyovyote as long as ni mwisho Chumbe!.
P
 
Kwa maana halisi ya katiba, katiba ni katiba ya JMT inayosema Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT. Aliyesema Zanzibar sio nchi sio mimi, ni katiba ya JMT.

Katiba ya JMT haitambui katiba ya Zanzibar, hivyo mimi ndie mkweli, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani!.

Kwa vile Zanzibar ina uhuru na utawala wake wa ndani, katiba ya Zanzibar na kujiita ni nchi, ni mambo yao ya ndani, sisi hayatuhusu!, ukiwa ndani kwako, uko huru kufanya chochote, hata kujiita vyovyote as long as ni mwisho Chumbe!.
P

Mkataba wa muungano / uvamizi unasemaje ??
 
Back
Top Bottom