VIDEO: Vijana wa JKT wajirekodi na kusema wakikuta mtu akiandamana watamdhuru

VIDEO: Vijana wa JKT wajirekodi na kusema wakikuta mtu akiandamana watamdhuru

Vijana wanaomaliza mafunzo JKT (service persons) wamejirekodi kwenye video na kusema wakikutana na mtu anayeandamana wanamtoa kinyesi, na kuwa ili wawe salama basi wahakikishe wawe na Tsh. 20,000/, lakini pia waombee wakutane na watu wengine ila sio kukutana na wao kutokana na mambo watakayowafanyia!

======

Salamu kwa hii video ya hawa vijana wa jkt nadiriki kusema JKT ya sasa sio ile miaka ya '80s mpaka 90s,

Au wanatoa taswira kwamba vyombo vya dola vya miaka hii ndo hulka yao hii wakiwa makambini?

Wazazi wa hawa vijana wanajua kama vijana wao ndo walichofundishwa hiki?

Hao migambo wanaruka na kukanyagana
 
Haya siyo bahati mbaya . Yamepangwa. Nchi hii ni ya kipuuzi sana
Kwani JKT si kuna kikundi cha sanaa? hawafanyagi maigizo/Drama? Wamezidiwaje kwa Technical Knock -out na yule Shekh ubwabwa wa mbwa mwitu? au wanaweza kuwa ni Vijana wa kijiweni hao.
 
Unamaana kwamba F6 wanaoenda JKT kwa Mujibu wa Sheria nao ni zao la UVCCM? Kama ndo hivyo; logically vijana wanaoingia F one watakuwa lazima wawe ni zao la UVCCM. What a Fallacy!!!

Sio kweli. Kimsingi; Jeshi halitakiwi kufungamana na siasa.

Sema kweli bwashee! :420Pls:
Mkuu ni ngumu kunielewa eeeh na Wala sijamaanisha hao kwa Mujibu hata Mimi licheti lao ninalo ila Mimi namaanisha wale vijana wa kujitolea na hata kupata nafasi ya upolisi tu lazima utokee chini UVCCM au uwe connected na watu wa chama bila hivyo hata miujiza ya Musa kuitenganisha bahari haitakutokea.

Imagine sasa hivi kuzipata tu nafasi za kujitolea kwenda jeshi Hadi uwapigie magoti baadhi ya watu ili wakupitishe sasa unaegemea jeshi Hilo litakuwa na wazalendo au ndiyo watatumika kuwalinda wale waliowapitisha kufika Hadi kuvaa hizo gwanda and it's so sad Green guard ndiyo wapo juu ya hao wote
 
Dah! Si ungelisema hivyo tangu awali ili ueleweke? Hivi Tz. inao vijana idadi yao ni wangapi? Kumbuka Tz. Population ni 70m+ na 60% Ndo vijana. Ni wangapi wanaopenda kujiunga na JKT? OK. Vijana JKT wakujitolea wanaopata nafasi ya kujiunga Jeshini ni wangapi? Mbona zipo nyuzi za malalamiko zinazotrend humu kwamba walidanganywa na wakadanganyika?
Imagine sasa hivi kuzipata tu nafasi za kujitolea kwenda jeshi Hadi uwapigie magoti baadhi ya watu ili wakupitishe sasa unaegemea jeshi Hilo litakuwa na wazalendo au ndiyo watatumika kuwalinda wale waliowapitisha kufika Hadi kuvaa hizo gwanda and it's so sad Green guard ndiyo wapo juu ya hao wote
Ni wale vijana CHOKA-MBAYA tu ndo wanaoweza kupiga magoti. (Kumbuka msemo wa "kupiga magoti" ina maana pana sana) Kijana anayejitambua kamwe, katu hatofanya hilo kwa sababu hakuna faida yoyote kijana ataipata kwa kujiunga na JKT kwa hiari - labda baadaye avizie matangazo ya ulinzi wa majumbani, Bank, kusindikiza magari yakusafirisha bidhaa e.g. bia/sigara n.k.(Private Security). Vinginevyo atakuwa mmojawapo wa kutusubiri "huko rodini" na kuchukua simu zetu bila hiari yetu.
 
Kwa hiyo ukiandamana ukikutana nae ukampa hiyo 20k ndo atakuacha ama? .... Ukiandamana uwe na mav* .... hata mbuyu ulianza ka mchichaa .... watakapokuja kabidhiwa majukumuu takuwa taabu tyupu
Usiwe na wasiwasi. Pamoja na kwamba kama nchi, inasemwa ipo kwenye Mkwamo; lakini kamwe hakuna yeyote atakayediriki kuwakabidhi majukumu vijana kama hawa wabwia unga. Kama wamethubutu kujirekodi na kupost huku mtandaoni watashindwa nini kujirekodi Three some etc na maujinga mengine kama hayo??? Mbona itakuwa ni Aibu kwa Taifa.
 
Daaah ulivyosema mambo ya kujirekodi umenikumbusha lile sakata la mdogo wangu Nyundo sijui rufaa Yao ilienda vipi
 
Vijana wanaomaliza mafunzo JKT (service persons) wamejirekodi kwenye video na kusema wakikutana na mtu anayeandamana wanamtoa kinyesi, na kuwa ili wawe salama basi wahakikishe wawe na Tsh. 20,000/, lakini pia waombee wakutane na watu wengine ila sio kukutana na wao kutokana na mambo watakayowafanyia!
Duh! Service persons (Service men & Service women)Naamini hiyo vid-clip kama sio AI basi hao ni baaditu ya wale vijana wa kujitolea. Hakuna kijana wa Kwa mujibu wa Sheria hata mmoja hapo.
Wamejirekodi na kurusha mtandaoni kwa Idhini ya Nani?
Je; watatoa risiti za EFD kwa makusanyo hayo ya kinyesi na Tsh.20,000/=
Wakiwafanyia watu kitu kibaya na Ikathibitika ni wao; watawajibishwa kwa mujibu wa Sheria za JMT.
======

Salamu kwa hii video ya hawa vijana wa jkt nadiriki kusema JKT ya sasa sio ile miaka ya '80s mpaka 90s,
JKT ya sasa ni ya miezi mitatu tu. Ile JKT ya 80s mpaka 90s ilikuwa ni 1yr. na unapitia mafunzo mengi. Hawa wa leo ni wa-"Kidigitali" ni kufungua na kufunga silaha aina ya SR56, Kwata na Kilimo baaas'. Ona nyuso zao zilivyomeremeta! Jeshi gani hilo?? Sikia lugha na sauti zao pamoja na gestures wanazo-portrait - ni uhuni mtupu. Hao ni maselule wamekusanywa kando ya Hanga walimokutwa na kuamrishwa " Hey! Nyie Mananga; simameni hapa na semeni hivi".....
Au wanatoa taswira kwamba vyombo vya dola vya miaka hii ndo hulka yao hii wakiwa makambini?
Hakuna kitu kama hicho. Wamejifukiza -wakakolea na Akili zao zikawatuma kufanya hilo.
Wazazi wa hawa vijana wanajua kama vijana wao ndo walichofundishwa hiki?

Kinachosikitisha, na pengine ndicho kilichomsukuma mtoa posti, ni kwamba.... Wanaropoka hivyo ndani ya social media, wakiwa ndani ya Kombati rasmi ya jeshi.... Huo SI ni uchochezi? Kuna tofauti Gani kati ya Hawa, na yule aliyesema watakinukisha?.... Labda ndiyo ukweli wa misemo ya kiswahili ya;
  • Mkubwa hakombi mboga
  • Kunya, anye kuku, kwa Bata ni kuharisha
Kina Mwaipopo, wanazidi kuongezeka
 
Vijana wanaomaliza mafunzo JKT (service persons) wamejirekodi kwenye video na kusema wakikutana na mtu anayeandamana wanamtoa kinyesi, na kuwa ili wawe salama basi wahakikishe wawe na Tsh. 20,000/, lakini pia waombee wakutane na watu wengine ila sio kukutana na wao kutokana na mambo watakayowafanyia!

======

Salamu kwa hii video ya hawa vijana wa jkt nadiriki kusema JKT ya sasa sio ile miaka ya '80s mpaka 90s,

Au wanatoa taswira kwamba vyombo vya dola vya miaka hii ndo hulka yao hii wakiwa makambini?

Wazazi wa hawa vijana wanajua kama vijana wao ndo walichofundishwa hiki?

Naada ya kushiba chakula cha bure na kupewa ahadi kibao za uwongo na kweli wanajiona na wao ni walamba asali🤣🤣🤣
 
Waache hisia hawajafundishwa hivyo, kazi ya jeshi ni kulinda raia, hakuna jeshi linalopigana na raia wake milele, watauondoa utawala na kiongozi wake na kuweka mwingine taifa linasonga mbele ni bra afe mmoja kuliko liangamie taifa zima.
 
Hawajafundishwa hivyo ni hisia zao binafsi wana akili za kipolisi.
 
Kinachosikitisha, na pengine ndicho kilichomsukuma mtoa posti, ni kwamba.... Wanaropoka hivyo ndani ya social media, wakiwa ndani ya Kombati rasmi ya jeshi.... Huo SI ni uchochezi? Kuna tofauti Gani kati ya Hawa, na yule aliyesema watakinukisha?.... Labda ndiyo ukweli wa misemo ya kiswahili ya;
  • Mkubwa hakombi mboga
  • Kunya, anye kuku, kwa Bata ni kuharisha
Kina Mwaipopo, wanazidi kuongezeka
Unataka kusema kwamba; kwa sasa kila mtu anapiga ngoma yake sio??
Mwaipopo aliitwa kwa uongozi na kuhojiwa. Hawa vijana wa hii klipu ninaamini ni "Ghosts" kwa maana kwamba hawatapatikana. Jeshi haliwezi kupoteza muda wake adimu kushughulika na vijana wajeuri - sana sana wataikabidhi ishu hii kwa Polisi au wataipotezea tu manake haina mashiko.
Polisi ndo saizi yao kama ilivyokuwa kwa Panya Rodi.
 
Wape muda warudi mtaani, within three month ya kukosa ajira hiyo misimamo watabadilisha
Walivyo mazuzu wameshajiaminisha wao ni wanajeshi.... Ngoja wasambaratike kila mtu arudi kwao.... Mwingine atakamata jembe, mwingine ataendesha boda, mwingine atakuwa saidia fundi na mwingine atafaidi matunda ya ubadhirifu wa mzazi wake.

Kila mtu atajiona mjinga na atapambana kivyake
 
Back
Top Bottom