Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Umasikini, ujinga na pengine maradhi.So what is it?
Jamii zetu zina tamaduni za kutafuta majibu rahisirahisi kwenye maswali yanayotaka uchambuzi wa kina wa kutumia mantiki.
Mtu ataumwa kwa sababu jamii ni masikini, inakunywa maji machafu, watu wanaumwa na mbu wanaoambukiza magonjwa, jamii hazina vyoo safi na salama, haina chakula bora kinacholiwa kwa mpango.
Hapo utaona sababu za kuumwa nyingi sana, na ukipima watu utakuta minyoo, virusi, bacteria na madudu mengine kibao.
Halafu mtu akiumwa, kirahisi kabisa tunakimbilia kwa waganga wa kienyeji watuague kwa ramli. Tunajazwa ujinga kuwa hapa kuna ndugu yako kakutupia uchawi.
Badala ya kufanya blood tests, X-Rays etc tujue tatizo kisayansi, tunakimbilia habari za uchawi.
Huo mfano mmoja tu, kwingine kote hivyo hivyo. Ukishindwa maisha kwa sababu huna strategy, unakimbilia kusema umelogwa. Ukishindwa kwenye ndoa kwa sababu za umasikini na ujinga, unakimbilia kusema umezimiwa nyota.
Ni ujinga fulani hivi tumejazana na umekaa kiutamaduni kiasi kwamba unaweza kukuta mtu kasoma degree mbili au tatu za chuo kikuu, tena za sayansi, anajua medicine, anajua bacteria, anajua virusi, halafu bado anaenda kwenye uchawi, kwa waganga, kwa babu wa kikombe.
Ni ujinga na umasikini wa kiutamaduni. Huu kuuondoa vigumu sana maana ujinga dawa yake elimu. Lakini kwenye utamaduni hata elimu inapata shida sana.