Video: Vijana wakamatwa kwa uchawi

Video: Vijana wakamatwa kwa uchawi

Umasikini, ujinga na pengine maradhi.

Jamii zetu zina tamaduni za kutafuta majibu rahisirahisi kwenye maswali yanayotaka uchambuzi wa kina wa kutumia mantiki.

Mtu ataumwa kwa sababu jamii ni masikini, inakunywa maji machafu, watu wanaumwa na mbu wanaoambukiza magonjwa, jamii hazina vyoo safi na salama, haina chakula bora kinacholiwa kwa mpango.

Hapo utaona sababu za kuumwa nyingi sana, na ukipima watu utakuta minyoo, virusi, bacteria na madudu mengine kibao.

Halafu mtu akiumwa, kirahisi kabisa tunakimbilia kwa waganga wa kienyeji watuague kwa ramli. Tunajazwa ujinga kuwa hapa kuna ndugu yako kakutupia uchawi.

Badala ya kufanya blood tests, X-Rays etc tujue tatizo kisayansi, tunakimbilia habari za uchawi.

Huo mfano mmoja tu, kwingine kote hivyo hivyo. Ukishindwa maisha kwa sababu huna strategy, unakimbilia kusema umelogwa. Ukishindwa kwenye ndoa kwa sababu za umasikini na ujinga, unakimbilia kusema umezimiwa nyota.

Ni ujinga fulani hivi tumejazana na umekaa kiutamaduni kiasi kwamba unaweza kukuta mtu kasoma degree mbili au tatu za chuo kikuu, tena za sayansi, anajua medicine, anajua bacteria, anajua virusi, halafu bado anaenda kwenye uchawi, kwa waganga, kwa babu wa kikombe.

Ni ujinga na umasikini wa kiutamaduni. Huu kuuondoa vigumu sana maana ujinga dawa yake elimu. Lakini kwenye utamaduni hata elimu inapata shida sana.
Noted
 
Kwani Whitecraft ni nini kama sio uchawi.
Sikuku za Halloween ni nini,wakutishe na kitu kisichokuwepo kwenye society iweje sasa,hayo makanisa ya wachawi yakiwemo freemasoni,hivyo vyuo na vitabu vya uchawi ulaya vina maana Gani.
kama Fbi,CIA,KGB nk kwenye operation zao ngumu wanatumia uchawi mfano kuingia sehemu na kupotea,nk.
Sema ulaya zaidi ni white magic,na Africa zaidi ni black magic uchawi WA level ya chini.
Mkuu una uhakika humo kichwani zimo kweli?
 
Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote, cha uongo au ukweli.

Hiyo ni haki yako ya kikatiba na kiutu. Ni sehemu ya uhuru wa kuabudu na uhuru wa kujiamulia mambo.

Tatizo kuthibitisha.

Mkuu,

Unaijua story ya "Romeo and Juliet" ya Shakespeare?

Ina movies kibao, inafundishwa vyuoni, imekuwa kama dini fulani jinsi ilivyo kila sehemu.

Sasa, je, kwa kuwa story hiyo ya "Romeo and Juliet" imepata kiki hivyo, hilo linamaanisha hao "Romeo and Juliet" wapo au walikuwepo kweli?

Hapana.

Story inatuonesha tu kwamba William Shakespeare alikuwa mtunzi mahiri ambaye ameandika story inayofuatiliwa na watu mpaka leo. Story ime capture imaginations za watu.

Watu wana uwezo mkubwa sana wa kujitungia hadithi zika capture imagination.

God. The value of paper money. The corporation as an entity. The country. Uchawi.

That does not mean all these things are real.

That just means that we have a high abikity if crwating what Yuval Noah Harari calls "manufactured reality".

Uchawi haupo, ni stories watu wameungaunga tu.

Ukitaka kuamini kitu kwa sababu kipo kwenye movies sana na kinafundishwa kanisani utaamini uongo mwingi sana.
Hawawezi movie vitu ambavyo havipo kwenye society.imagation ni kuufunua ulimwengu wa kiroho katika ulimwengu halisi.
Mfano uvionavyo vyote kwenye cartoon vile ni viumbe halisi vipo kwenye ulimwengu roho ni mwanadamu pekee na malaika ndio walioumbwa kwa uzuri mfano wa Mungu
 
Mkuu bongo dili sio kila linalosemwa na kila mzungu ni jambo sahihi.
Majengo ya freemason,alama za illuminat,church of Satan ujaviona ulaya.
Ni nini kama sio uchawi.
Africa wanafanya uchawi WA level ya chini sana black magic,ulaya wanafanya whitemagic na red magic zaidi
 
Majengo ya freemason,alama za illuminat,church of Satan ujaviona ulaya.
Ni nini kama sio uchawi.
Africa wanafanya uchawi WA level ya chini sana black magic,ulaya wanafanya whitemagic zaidi
Umejuaje ni uchawi kwel? Thibitisha apa .
 
Majengo ya freemason,alama za illuminat,church of Satan ujaviona ulaya.
Ni nini kama sio uchawi.
Africa wanafanya uchawi WA level ya chini sana black magic,ulaya wanafanya whitemagic na red magic zaidi
Hamna kitu hapo

Ova
 
Umejuaje ni uchawi kwel? Thibitisha apa .
Wanatoa kafara mbalimbali mfano za damu,za humiliation ritual mwanaume kuingiliwa ushoga nk,Ibada zao ni za Siri tena usiku na only members.wachawi ndio usali usiku
 
Tueleze kwa kifupi hicho kwenye video ni nini?? Ukiachana na haya maelezo yote chief
Ni umasikini na ujinga, nieleze mara ngapi chief?

Na ukiona hiki ki post tu kuwa ni "maelezo yote" nikitaka tujadili kwa undani kabisa mambo ya matatizo ya saikolojia na utamaduni Afrika, kwa kuzama mpaka kwa John Mbiti na Jean-Paul Sartre tutaweza?

Huoni kuwa na wewe unarudi kule kule nilikokulalamikia kwenye utamaduni wa kutaka majibu mafupi, rahisi, ya mkato, kwenye maswali yanayotaka mazungunzo ya kina, ya kimantiki na yenye kuangalia mambo kwa muktadha mpana?

Naogopa kuzama kwenye maongezi ya kina kwa maana naona tayari kama ushanipa tahadhari ya "comments ziwe fupifupi".

Na hata hizo "comment fupi fupi" nilizoanza nazo kwa kusema hili ni tatizo la ujinga na umasikini, hazieleweki, zinahitaji maelezo zaidi.

Kwa hivyo comment zikiwa fupi hazieleweki, kwa sababu ni fupi zinahitaji maelezo marefu.

Comment zikiwa ndefu, naambiwa nielezee bila maelezo marefu.

Tutaelewana kweli hapa?
 
Majengo ya freemason,alama za illuminat,church of Satan ujaviona ulaya.
Ni nini kama sio uchawi.
Africa wanafanya uchawi WA level ya chini sana black magic,ulaya wanafanya whitemagic na red , ata smartphone tulisema ni free Mason sasa ivi unaonaje

Majengo ya freemason,alama za illuminat,church of Satan ujaviona ulaya.
Ni nini kama sio uchawi.
Africa wanafanya uchawi WA level ya chini sana black magic,ulaya wanafanya whitemagic na red magic zaidi

Kwel mmedanganywa sana , sioni nikitoboa kukuelimisha.
 
Hawa wanafanya uchawi WA level ya kimasikini ujinga na upumbavu huu unaitwa black magic,pana red magic,whitemagic.
Mitume na manabii wanafanya uchawi aina ya white magic,wanasayansi wanatumja white magic kufanya unthinkcable projects au ideas
 
Wanatoa kafara mbalimbali mfano za damu,za humiliation ritual mwanaume kuingiliwa ushoga nk,Ibada zao ni za Siri tena usiku na only members.wachawi ndio usali usiku
Unaamini hao watu, wanafanikiwa kuliko wewe na Mungu muweza wa yote wanaomwamini wanaishi kwenye lindi la umaskini?
 
Tueleze kwa kifupi hicho kwenye video ni nini?? Ukiachana na haya maelezo yote chief
Uchawi unavunja kanuni za kisayansi, hauelezeki

sijaona kitu hapo ambacho hakielezeki, hapo ni aidha wana matatizo ya akili ama video hiyo ni maigizo
 
Majengo ya freemason,alama za illuminat,church of Satan ujaviona ulaya.
Ni nini kama sio uchawi.
Africa wanafanya uchawi WA level ya chini sana black magic,ulaya wanafanya whitemagic na red magic zaidi
Mkuu,

Nikianzisha dini yangu na kujenga majengo ya hiyo dini, nikasema mimi ndiye Mungu muumba vyote, nikapata wafuasi, hayo majengo na kuwapo kwa wafuasi wa hiyo dini yangu vitanifanya mimi niwe kweli Mungu muumba vyote?
 
Back
Top Bottom