Video: Vijana wakamatwa kwa uchawi

Video: Vijana wakamatwa kwa uchawi

Kwa sababu hakuna uchawi, kinachoitwa uchawi ni umasikini, ujinga, hadaa na vitu kama hivyo.
Uchawi upo mkuu, labda kama tunatofautiana kwenye kutafsiri maana yake, wewe unatafsiri kama ujinga umasikini pengine ni kutokana na mazingira uliyoishi, ila kwa mimi niliyezaliwa kijijini kalema, kwetu tunauona uchawi kama nguvu hasi isiyoonekana
 
uchawi upo mkuu, labda kama tunatofautiana kwenye kutafsiri maana yake, wewe unatafsiri kama ujinga umasikini pengine ni kutokana na mazingira uliyoishi, ila kwa mimi niliyezaliwa kijijini kalema, kwetu tunauona uchawi kama nguvu hasi isiyoonekana
Labda na mimi nijifunze kwako.

Unajuaje huu ni uchawi, na huu si uchawi, labda ni kitu nisichokijua tu?

Kwa mfano.

Nyumbani kwenu kijijini mmegombana na jirani wa karibu yenu, shamba la pili, liko mbali kidogo.

Akasema nitawaua wote nyie.

Wiki moja baadaye ukakuta watu wamekufa ndani ya nyumba.

Hakuna mlango uliovunjwa.

Utajuaje huo ni uchawi au si uchawi?
 
🔹Polisi huwa wanaongizwa Sana mkenge na hao matapeli ambao unakuta wamekwisha kula Dili na waganga tapeli wanajifanya ni wachawi wamenasa halafu anajitokeza tapeli huyo kujifanya yeye ndio kawatega na dawa zake na kuwanasua ili baadaye apate wateja wajinga waliokuwa obsessed na Imani za kishirikina.

🔹 Mkoa wa pwani Kuna kuliko mmoja alikula Dili na mganga feki akazuga akiba mzigo imegoma kushushwa akapelekwa mpaka polisi lakini baadaye ilikuja kugundulika ni magumashi

View: https://youtu.be/mjWCCRqXsis?si=EyH_Ieoycs0bYRS_

🔹 Kule Mwanza wakati zumaridi anaanza mazingaumbwe aliwahi kuwsleta vijana kutoka Kigoma na kuwaweka juu ya paa la kanisa lake na ukijifanya wamedondoka hapo na ungo kutokana na maombi.

View: https://youtu.be/GmpTjDxEF48?si=dftKscnPsT0KHKbi
🔹Iringa ,mbeya na Dar vituko kama hivyo ni vingi. Vyote vipo staged na Kuna mtu yupo nyuma yake ili kutangaza biashara ya kitapeli. Hapo wanakuwa wameshalipana, wsnaespakaa madizi au chokaa , kuvaa kaniki na kubeba ungo ,pembe na vibuyu ila ukimwbia aruke anazuga nguvu zimeisha. Umagumashi mtupu

Umenikimbusha Mombasa Kenya walitokea watu wanacheza ngoma nje, pembeni ya gari, wakiwa uchi.

Madai yao wameiba gari, halafu ile gari ina ulinzi wa uchawi.

Kumbe ilikuwa deal tu la ku boost biashara ya mganga fulani wa kienyeji.

Polisi kija kuchunguza kidogo tu, wakagundua kuwa ile habari yote ilikuwa ni mchezo umepangwa na wale watu walikuwa wamelipwa. Yani watu wameona mambo yalivyopangwa kwenye CCTV footage.

Sasa hapo kwa watu wenye akili za kuamini uchawi wanachotwa kirahisi sana.

Michezo kama hii wajinga wajinga wengi tulio nao hapa unawashikia akili vizuri tu.


View: https://youtu.be/m11yTkKPndk?si=bH8JvGpRRh3aWZZy

 
Labda na mimi nijifunze kwako.

Unajuaje huu ni uchawi, na huu si uchawi, labda ni kitu nisichokijua tu?

Kwa mfano.

Nyumbani kwenu kijijini mmegombana na jirani wa karibu yenu, shamba la pili, liko mbali kidogo.

Akasema nitawaua wote nyie.

Wiki moja baadaye ukakuta watu wamekufa ndani ya nyumba.

Hakuna mlango uliovunjwa.

Utajuaje huo ni uchawi au si uchawi?
Ndio maana nimesema uchawi ni nguvu hasi isiyoonekana kwa macho; kinachoonekana ni matokeo yake,

Kwa mfano mimi nimeshashuhudia kaburi la mtu aliyekufa miaka 7 likifukuliwa na marehemu kumwagiwa madawa akaamka,

Na kuongea kwa zaidi ya masaa ma 4, ktk kikao cha familia,
 
Police wafanye igizo ili iweje sasa
Kwahiyo na wewe unaamini polisi
download.jpeg
hawawezi kufanya igizo?
Police wafanye igizo ili iweje sasa
images (1).jpeg

Hili igizo la Mo umelisahau?
 
Ndio maana nimesema uchawi ni nguvu hasi isiyoonekana kwa macho; kinachoonekana ni matokeo yake,

Kwa mfano mimi nimeshashuhudia kaburi la mtu aliyekufa miaka 7 likifukuliwa na marehemu kumwagiwa madawa akaamka,

Na kuongea kwa zaidi ya masaa ma 4, ktk kikao cha familia,
Kwa hiyo definition yako ya uchawi nuclear fusion nayo ni uchawi?

Ukipuliziea hewa yenye sumu isiyoonekana ya cyanide ukafa, huo nao ni uchawi?

Hiyo story yako unaweza kuithibitisha kuwa ilitokea kwwli na hutufungi kambabtu hapa?

Iliripotiwa wapi?
 
Kwa hiyo nikiwachezea mchezo wa karata tatu nikawaambia huu ni muujiza wangu Mungu muumba vyote, wakaniamini, hapo nitakuwa kweli Mungu muumba vyote?

Unaelewa kuwa kukiamini kitu kuwa ni kweli hakukifanyi kuwa kweli?

Vinginevyo wote tungejiaminisha sisi ni mabilionea wa US dollars, na kujiaminisha hivyo kungetufanya kweli tuwe mabilionea, unaelewa hilo?
Imani upimwa kwa matokeo ya mwili Sasa utaamini vipi we ni bilionea Hali choka mbaya
 
Mkuu,

Tuanze na Halloween.

Nikitunga sikukuu ikakubalika na wengi kama sikukuu, hata watu wanaotaka kusheherekea chochote tu kujiondolea uchovu wa kazi za kila siku, basi hilo linamaanisha sikukuu hiyo inawakilisha jambo la kweli?

Huoni kuwa hapo umefanya logical fallacy ya appeal from popularity ukaiunganisha na logical fallacy ya non sequitur?

Yani umeunganisha logical fallacy angalau mbili kwa pamoja ukapata double decker fallacious argument.

Unaelewa hilo?
Unajua asili ya Halloween ilivyoanza.
Mbona ulaya waliuwa wachawi kupitia operation tokomeza uchawi wengi waliuliwa
 
Umenikimbusha Mombasa Kenya walitokea watu wanacheza ngoma nje, pembeni ya gari, wakiwa uchi.

Madai yao wameiba gari, halafu ile gari ina ulinzi wa uchawi.

Kumbe ilikuwa deal tu la ku boost biashara ya mganga fulani wa kienyeji.

Polisi kija kuchunguza kidogo tu, wakagundua kuwa ile habari yote ilikuwa ni mchezo umepangwa na wale watu walikuwa wamelipwa. Yani watu wameona mambo yalivyopangwa kwenye CCTV footage.

Sasa hapo kwa watu wenye akili za kuamini uchawi wanachotwa kirahisi sana.

Michezo kama hii wajinga wajinga wengi tulio nao hapa unawashikia akili vizuri tu.


View: https://youtu.be/m11yTkKPndk?si=bH8JvGpRRh3aWZZy


Kenya hayo maigizo ni mengi Sana yamiwemo ya nyuki, au kufumaniana kwa kugandana wakifanya mapenzi, watsjifanya ama mganga au dawa kutoka Tanzania au uganda
 
Unajua asili ya Halloween ilivyoanza.
Mbona ulaya waliuwa wachawi kupitia operation tokomeza uchawi wengi waliuliwa
Nakwambia hivi, uchawi ulikuwa ni imani inayokubalika dunia nzima. Hususan kwa sababu ya dini.

Mimi.nimefika.mpaka Salem Massachusetts huko walikokuwa wanauliwa watu waliodaiwa kuwa wachawi.

Ila, wenzetu walivyofika kwenye miaka ya 1500, wakaanza kuhoji vitu vingi sana kuhusu imani za dini, Mungu na uchawi.

Ulaya walikufa sana katika kitu kinaitwa "The Black Death". Wakajiuliza maswali mengi magumu sana, huu uchawi gani unaotuua? Tufanye nini tuepukane nao? Tumepewa laana ya nini?

Wakaja kugundua sababu za magonjwa si uchawi, ni uchafu, ni vijidudu kama bacteria, virusi, ni kukosa maji safi, ni kulala na wanyama hususan panya, ni kula vitu vichafu, ni watu kulundikana pamoja mijini bila kuwa na hewa safi.

London wakafanya uchunguzi kipindupindu kinaeneaje? Wakaja kugundua mpaka bomba la maji la Broad Street ambapo watu walikuwa wanakutana na kuambukizana kipindupindu. Huo mwaka 1954.

Yani watu walikuwa wanaambukizana kipindipindu kwa kugusa kike kifungua bomba, walivyokiondoa na kuelimisha watu, kipindupindu kikaisha.

Soma hapa John Snow, Cholera, the Broad Street Pump; Waterborne Diseases Then and Now

Watu wakasoma medicine, wakagundua madawa, mpaka dawa za kuua bacteria wakagundua penicillin 1928.

Hizo habari za uchawi zikakosa nguvu, zikabaki sanasana kwenye movies na hadithi.Kila unavyozidi kugundua sababu za kisayansi za kuelezea mambo, habari za uchawi zinazidi kukosa sababu ya kuwapo.

Jamii zetu zinaamini sana uchawi kwa sababu hazielewi au kukubali sayansi. Na ulimwengu hautaki vacuum ya sababu. Nature abhors a vacuum. Kama kitu watu hawakielewi, watakitungia sababu tu hata kusema "mapenzi ya Mungu tu hayo" au "Uchawi huo".

Watu wamegundua mpaka kucheza na genes kisayansi.Kuzibadikisha. Yani wenzetu wametoka kuamini jini, mpaka kwenda kuifungua code gene. Ukiangalia hapo mzizi wa neno jini na gene ni huo huo mmoja kwa sisi tunaofuatilia etymology. Ila, wenzetu wamechukua zile habari za uchawi, wakasema, hivi tunafanyaje hizi hadithi za uongo ziwe kweli? Yani habari ya magic potion inayoponya magonjwa kwa kuisomea abracadabra tunapataje dawa ya kweli inayoweza kuponya magonjwa? Wamefanya kazi, wamepata dawa.

Sisi bado hatujatoka kwenye abracadabra kwa kiasi kikubwa sana. Yani sehemu nyingi Africa imani za watu ni sawa na imani za Ulaya za mwaka 1500-1900. Na hapo tushukuru watu wameletewa vitabu, smartphones, internet na movies.

Yani mtu kakaa kwenye internet mpaka leo anaamini uchawi jamani?
 
Kwani Whitecraft ni nini kama sio uchawi.
Sikuku za Halloween ni nini,wakutishe na kitu kisichokuwepo kwenye society iweje sasa,hayo makanisa ya wachawi yakiwemo freemasoni,hivyo vyuo na vitabu vya uchawi ulaya vina maana Gani.
kama Fbi,CIA,KGB nk kwenye operation zao ngumu wanatumia uchawi mfano kuingia sehemu na kupotea,nk.
Sema ulaya zaidi ni white magic,na Africa zaidi ni black magic uchawi WA level ya chini.

Man, how can you be this dumb? Kiwango chako cha ujinga hata chizi atakucheka. Huu ujinga umesomea wapi?
 
Back
Top Bottom