Uchaguzi 2020 VIDEO: Wachambuzi wa siasa Kenya washangazwa na muundo wa uchaguzi wa Tanzania, wasema walitoka huko kitambo sana

Acha maneno mengi, alichokisema huyo jamaa ni sahihi au sio sahihi? Shame
Ni nafuu na sisi Tanzania wenyechangamoto ndogo ya tume huru kuliko Kenya wenye siasa za ukabila.
Nasema kukosa tumehuru kwa Tanzania ni changamoto ndogo kwa sababu hata wenye kudai tume huru hawaonyeshi nia yadhati kuitaja.ndo maana wanakubali kushiriki uchaguzi bila tume huru.haya ni madhaifu ya vyama pinzani kwenye kutia maznani tume huru.
 
Unafahamu kuwa hata mamba anaweza kuuliwa ndani ya mto ijapokuwa nguvu ya mamba ni maji?

Picha ni mfano halisi wa kitu. Mandhari ya tawala yetu inafahamika ipoje na mifano ya wazi ipo wazi.

Katiba ni suala zuri! Lakini ilitamkwa haikuwa katika ilani yao. Athari ya waliyotunisha msuli inafahamika marejeo kwao yalikuwa ni nini!

Uchaguzi ni wakati maalumu! Ni sawa sawa ubora wa daraja la mto usubiri wakati wa masika. Wao ni ndege wajanja lakini uchaguzi ni tundu bovu!

Ndivyo wanavyofanya wapinzani.
 
Pale Kenya sasa hivi ni kama hamna mkubwa! Kila mtu ni kambare! Wamejaa ukabila, hayo ndio waliyoendelea hakuna kingine.

Fikiria uchaguzi bado miaka 2 lakini ofisi ya rais Kenyata ina mgogoro wa kugombea madaraka ya 2022

Lazima nasi tufikirie namna bora ya kufanya chaguzi huru na za haki ... hatuhitaji ku copy na ku paste kila jambo kutoka kwa wengine.

Ili kuondokana na hofu za kitawala ni vema viongozi walioko madarakani na wale watarajiao kuchukua madaraka wakajifunza kwamba njia nyepesi ya kupewa dhamana na wananchi kuwaongoza ni kuwatendea haki hao wapiga kura, mara nyingi ukiona mtu anatafuta mbinu chafu ku win ushindi basi tambua kuwa kuna mabaya amefanya anatafuta huruma ya kujinusuru
 
Wakenya wana matatizo mengi na Magufuli kawanyoosha ni vema wakachambua uchaguzi wa marekani maana wao ndio vibaraka wao afrika ya Tanzania hayawahusu
Magufuli anatukana tu wale wenye tume yao maana wamepigwa chenga ya mwili na walimuhakikishia mwamba atanasa kwenye mtego. Sa sijui itakuwaje! Patamu hapo!
 
Unakaa Tanzania gani hiyo usiyoyaona hayo.au kwavile hayazungumzwi wazi wazi.
Sio kweli kaka yangu Tanzania hakuna ukabila huo ni uwongo unatungwa kuchafua viongozi

Mimi sina chama
 
Yupo sahihi kabisa,japo kila nchi mabadiliko huwa yanakuja gradually na ningumu kufananisha kinachofanyika Kenya au Uganda kiwe sawa na Tz.

Ila nawao wapambane na huu ubaguzi kama ule wa pale Mlang'a pale wafuasi wa Uhuru walipowazuia wafuasi wa Ruto na ugomvi mkubwa kupelekea watu wawili kufariki.......sasa mkienda kwa Wakelenjin nawao watalipiza.......
 
Huyo jamaa ni wa karne hii lakini fikra zake ni za karne ya nyumba. Si akili wala maarifa wala ufahamu kwake hivyo havijakuwa. Vimegotea hukoo! Ashakum si matusi! Hoja zake, kauli zake na vitendo vyake vimeshamiri ujinga kwa sababu vitatu kwake viligote nyuma (akili, maarifa na ufahamu). Matokeo yake anafanya mambo ya kishamba.

Kuna kauli inasema "..ujinga unaporomosha jengo kwa muda mfupi tu lilijengwa kwa karne.."

Sasa ujinga umeongezekewa na ushamba athari yake ni maafa tu.
 
Tanzania ya sasa aliyekula trilion 1.5 akamtoa kafara CAG, aliyetafuna pesa cash madini yote yaliyokamatwa airport Bandarini mipakani pia akachukua pesa zote za wamiliki wa maduka ya kubadili pesa za kigeni akajimilikisha kienyeji kwa njia haramu za kishetani huitwa Mzalendo, uzalendo Tanzania ni kupora vya wengine na kutafuna pesa za umma kama kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge, neno uzalendo kwa Tanzania linatumika tofauti na sehemu Nchi zingine Duniani.
 

Najiuliza mara mia lakini bado sipati jibu, hivi kweli hivi vyama vya upinzani wamejiridhisha na nini hasa kuamini kuwa watashinda kutokea ndani ya Tume isiyo huru? kwanini kwanza wasidai katiba na tume huru ndipo uchaguzi ufuate hapo uwanja utakapokuwa na level sawa? kule Zanzibar kuna mtu alishasema hawawezi kuachia madaraka kwa kutumia makaratasi naona dalili zote kuwa usemi ule tayari ulishaleta kivuli chake huko bara yetu macho
 
Wapo CCM wenye akili timamu hawapendi tabia ya mtukufu mwenyekiti wa CCM na polepole lakini wanaogopa kumkosoa kwa hofu ya kuvuliwa uanachama wa CCM kisha kubambikiwa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Nadhani baada ya matokeo haya tunanafasi kubwa sana ya kulazimisha mabadiliko ya namna tume inavyopatikani.
 
Nadhani baada ya matokeo haya tunanafasi kubwa sana ya kulazimisha mabadiliko ya namna tume inavyopatikani.
Siyo baada ya matokeo kwani tayari Tumeccm wanayo matokeo mifukoni wanatembea nayo saa 24, watanzania wapige kura wasipige kura Tumeccm wanayo matokeo ya kumtangaza mshindi ni mtukufu mwenyekiti wa CCM ni bora kuikataa hii Tume ya kishetani sasa kabla hawajaleta machafuko na ikibidi mkurugenziccm wa Tumeccm afikishwe ICC kwa kuonyesha upendeleo kwa CCM kuashiria uvunjifu wa Amani tarehe 28 October
 
Siasa za Kenya ni za ubaguzi wa kikabila.

Kenya wapambane kwanza waondoe hili kabla ya wao kukosoa wengine.
Tusidanganyane, ukabila uko popote hata Marekani, kinachotofautiana ni viwango tu. Angalia hii awamu ilivyojaa ukabila.

Kuwasema wakenya saana ni kuwaonea tu na ni unafiki tu.
 
Pale Kenya sasa hivi ni kama hamna mkubwa! Kila mtu ni kambare! Wamejaa ukabila, hayo ndio waliyoendelea hakuna kingine.

Fikiria uchaguzi bado miaka 2 lakini ofisi ya rais Kenyata ina mgogoro wa kugombea madaraka ya 2022
"Hoja hapa ni tume ya uchaguzi. Kwamba watendaji wanateuliwa na Rais ambaye pia ni Mgombea wa nafasi hiyo. JADILI. Is it fair or not?!"
 
Katibu imempa mamlaka ya uteuzi JPM.
unalingine bwashee?
Katiba ipi? Katiba mbovu au katiba ile ile inayolalamikiwa? Mbona Tume za mwinyi mkapa Kikwete hazikuwahi lalamikiwa kama hiyo Tumeccm ya mtukufu magufuli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…