Video: Wakili Boniface Mwambukusi akifafanua kisheria na kikatiba ni kwanini uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu ni uvunjaji wa katiba ya JMT ya 1977

Ya IGA yamemshinda anatafuta kiki kwengine?

Aandamane.
 
Mwabukusi ni mwanasheria kanjanja tu, ambaye anatumia nguvu nyingi kujenga hoja. Angekuwa amefuta cheo cha PM au kuweka PM wawe 2 ingekuwa ni makosa.

Ila ameunda nafasi ya Naibu ambayo haizuiliwi na Katiba
 
Huyu kashindwa Mahakamani Hadi Sasa hajakata Rufaa.

Alikuwa anapotosha kwamba Bandari zote kapewa DP World na TPA hairuhusiwi kutoa Tenda kwingine,Tenda imetangazwa badala aombe yupo yupo anatafuta kiki za kijinga.

Sifa zitakuja kumpoteza.
 
Huyu kashindwa Mahakamani Hadi Sasa hajakata Rufaa.

Alikuwa anapotosha kwamba Bandari zote kapewa DP World na TPA hairuhusiwi kutoa Tenda kwingine,Tenda imetangazwa badala aombe yupo yupo anatafuta kiki za kijinga.

Sifa zitakuja kumpoteza.
Shut up, mhaini kwanini mkampa dhamana?!

Amewashinda mahakamani, akawashinda na kituo cha polisi, hamumuwezi huyo.

Mpaka bunge na serikali wote wameamua kuacha kubadilisha ile sheria.
 
Kitu cha msingi hapa hicho cheo ni Sawa na ceremonial title, Kwa sababu , hata kuwa Hana hayo Mamlaka Waziri Mkuu. Kwa hiyo sio Jambo la kuliongelea Sana.
 
Point yako nambari wani ni batili Kwani moja ni Waziri Mkuu na mwingine ni naibu Waziri Mkuu, Kwa hiyo sio Kwa Jina lile na sio Kwa cheo kile kile moja ni Makubwa Kwa mwenzake na cheo chake kipo gazetted
 
Kuanzishwa kwa Ofisi hiyo hakumaanishi kuivunja, kuivuruga, kuiingilia au kuibadili Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni Ofisi mpya inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba (Ibara ya 36(1)).
Vipi kuhusu bajeti ya Ofisi hii mpya kuwa hazikupitishwa na bunge?
Je mamlaka ya Rais kutumia fedha ambazo bunge halijapitisha yanatoka kwenye kifungu kipi cha katiba/sheria?
 
2. Kama Rais ameona kuwa PM anahitaji mtu wa kumsaidia, na aitwe "Naibu Waziri Mkuu", apeleke amendment ya katiba..
Sikubaliani na point #2. Ukifanya ammendment ya kisheria itabidi iwe ya kudumu. Kwa hiyo hata akija Rais mwingine itabidi amuweke Naibu WM.

Hawa manaibu wanawekwa kukidhi mambo fulani tu. Kwa mfano Salim Ahmed Salim alipewa unaibu mwaka 1985 ili kumtunzia hadhi kwa kuwa alikuwa na profile kubwa baada ya kuwa mtarajiwa wa Urais wa Tanzania Nyerere alipokuwa anatoka.

Mrema alipewa kama shukrani tu kwa namna alivyo kuwa anashughukikia masuala ya ufisadi wa akina Chavda, wizi wa dhahabu etc.

Mwabukusi ni boksi tupu halina kitu zaidi ya kelele na kufoka. Msimpe umaarufu asiokuwa nao
 
Mwabukusi amevurugwa
 

I couldn't agree more.
 
Rais anaruhusiwa kuunda na kuvunja wizara na mawaziri wake, kwanini ashindwe kuteua naibu PM?
Mawaziri hawathibitishwi na Bunge ilhali PM anathibitishwa na Bunge. Hiyo ndiyo tofauti.
 
I subscribe your position Msomi, kuna mahali Seniour Mwambukusi amejichanganya sitaki kabisa kuamini kuwa hafahamu hii tafsiri.
 
Mawaziri hawathibitishwi na Bunge ilhali PM anathibitishwa na Bunge. Hiyo ndiyo tofauti.

Huyu ni naibu PM sio PM na hiyo ndo tofauti. Naibu PM is a temporary post
 
Huyo ni PM sio naibu wake.
Sasa shida ni kwamba kazi anazofanya PM ndo zilifanya kikatiba awe na Sifa ya kupelekwa Bungeni jina lake...Kama na huyu DPM atafanya kzi kama za PM kwanini kusiwe na haja ya kupeleka bungeni pia
 
Haya sasa n huyu Wa Sasa hivi kapewa kwa sababu gani unawez kuniambia 🤔🤔🤔🤔 maana mmmh Doubtfull
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…