NB: JF Moderators, naomba hii thread ijitegemee. Najua imeshajadiliwa lakini naona huyu wakili kaja kivingine. Tuwape watu nafasi wajadili hoja yake..
Back to the topic;
✍️Ni kweli Hayati Mwl Julius K. Nyerere aliwahi kuunda ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na kumteua Dr Salim A. Salimu kushika SER=221]JokaKuu[/USER]
denooJ Mag3 na wengine mna maoni yoyote?
Naona kuna watu wanataka kupotosha. Haijawi tokea Nyerere akateua Naibu waziri mkuu. Na Salim Hamed Salim hajawahi kuwa naibu Waziri Mkuu.
Historia inachakachuliwa na watu wamenyamaza tu. Vijana wengi hawajui historia ya hii nchi. hata baadhi ya wanasiasa tulionao leo. Ni wachache tulioweza waona viongozi wote wa nchi hii, ambao tunaweza kutoa historia kidogo.
Mwaka 1984 baada ya Sokoinne kufa Mwalimu Nyerere alimteuwa Salim Hamed Salim kuwa Waziri Mkuu. Na wakati huo Waziri Mkuu alikuwa anakuwa pia Makamu wa pili wa Rais baada ya Rais wa Zanznibar.
Mwaka 1985 Nyerere aliachia madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na uchaguzi ulifanyika chini ya chama kimoja Mwinyi alie kuwa Mgombea pekee alishinda kwa kura za ndiyo na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwinyi alikuwa ni Rais na kule Zanzibar alikuwa Idrisa Abdul Wakil Mwinyi. Hivyo nafasi ya Waziri Mkuu ilibidi ateuliwe mtu kutoka bara ndipo Jaji Joseph sinde Warioba aliteuliwa na kushika hiyo nafasi huku akiwa pia makamu wa kwanza wa Rais.
Salim Hamed Salim aliteuliwa kuwa Waziri wa ulinzi na alifanya mabadiliko na maendeleo makubwa kwa jeshi letu kwa mara ya kwanza wakawa na uniform zaidi ya moja. Akaagiza magari mengi sana kwa ajiri ya jeshi.
Sasa mnao sema Nyerere alimteuwa Jaji Warioba sijui ilikuwa lini? Nyerere kaachia Urais Oct 1985. Tena nakumbuka Mwinyi alipo mteuwa Warioba, kuna uwanja wa Musoma ulikuwa unajengwa. Kulikuwa na tofali. Ule uwanja ulisimama kujengwa na tofali zote zikachukuliwa kupelekwa huko Nyamuswa- Ikizu kujenga nyumba ya Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais ndugu Joseph Sinde Warioba.
Wakati huo mimi nilikuwa mdogo tu, na chipukizi wa kudumu katika kupokea viongozi. Hivyo nilihoji kwa nini walichukua tofali za kujengea uwanja wa musoma na kuzipeleka zikajenge nyumba kwao waziri mkuu, tulijibiwa wameazima tofali hivyo watazirudisha kumalizia uwanja.
Walisema ni aibu waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais nyumbani kwao kutokuwa na nyumba ya maana hivyo wamefanya vile hili kumhifadhi waziri mkuu wetu.
Niseme tu hadi leo zile tofali hazijarudishwa na uwanja wa Musoma umebaki kama ulivyo. Ulitakiwa jukwaa zijengwe kwa kuzungushwa. Uwanja huu jukwaa kubwa na lile dogo zilijengwa mwaka 1984-1985 wakati wa kufanyika sherehe za kuzaliwa chama cha mapinduzi.
Tafadhali mzee Warioba mzee wetu rejesha tofali Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Musoma umaliziwe kujengwa. Ahadi ni deni!
Nakumbuka sana kwani nilikuwa kamanda wa kikosi. (Pratoni kamanda) sherehe hizi zilifana sana kwani kwa mara ya kwanza vijana tulifundishwa mbinu za kivita. Jeshi ndo lilikuwa likitoa mafunzo pia tulikuwa na mwalimu wa Haraiki yeye alisomea China na Urusi ya zamani huyu mwalimu aliagizwa kutoka Comoro.
Na wakati wa mafunzo yalikuja magari ya maziwa na tulikunywa sana maziwa tukipumzika kabla ya kuendelea tena na mazoezi.
Kuna watu tumeonja raha za utawala wa Nyerere japo kuna wapinzani leo wanamtukana, nachojua hawamjui vema Nyerere na wazee wenzake akina Mkwawa. Walijitahidi kwa kiasi chao.
Viongozi wote wa Taifa walikuwepo kuanzia Rais Nyerere, Rais Mwinyi toka Zanzibar, Waziri Kiongozi wa Zanzibar Maalim Seif, waziri Mkuu Salim Hamed Salim, Mzee Mfaume Rashid Kawawa. Akina Bibi Titi Mohamed na wengineo wengi.
Sifa zilimwagika kwa ile haraiki, bila kumsahau mkaguzi alie kuwa anakuja kutuona tumeiva kiasi gani, Major General Mwita Marwa.
Baada ya sherehe hizi kuna baadhi vijana tuliteuliwa kwenda Urusi.
Baadae miaka ya 90 na ushee, wakati huo Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani. Kwa kazi alizokuwa anafanya. Mawaziri wenzake wakata mzingua asiwaingilie kwani Mrema aliwabana hadi mawaziri.
Ndipo Rais Mwinyi akamteuwa Mrema kuwa Naibu waziri Mkuu. Lakini uteuzi huu ulileta gumzo kiasi kwamba haukuwa unatambulika rasmi. Ulifanywa kisiasa zaidi. Ndo maana Mrema hakuwai kulipwa mafao, wala kutambulika rasmi kwani hata ofisi ya naibu wa rais hakuwa nayo.
Hivyo niseme tusipotoshe historia ya hii nchi. Kutaka kutetea mambo ambayo siyo. Warioba hakuwa waziri Mkuu wakati wa Nyerere bali Mwinyi na alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais pia.
Salim Hamed Salim hakuwai kuwa naibu Waziri Mkuu bali alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa pili wa Rais.
Nafasi ya Naibu Waziri Mkuu ilitolewa mara moja tu, nayo ilikuwa ya kisiasa zaidi. Ilikuwa kwa Mrema pekee. Ndo maana hata Mrema mwenyewe alikuwa akiongea atajitambulisha rasmi kama waziri wa mambo ya ndani mstaafu. Akisema naibu waziri mkuu alikuwa akicheka yeye mwenyewe kwani alijua cheo hiko hakikuwepo kikatiba.
Waziri mkuu ni anatakiwa athibitishwe na Bunge. Hivyo hata naibu wake maana yake anauwezo wa kutenda sawa na waziri Mkuu, na bahati mbaya Katiba haijatamka juu ya naibu waziri mkuu.