Video: Wakili Boniface Mwambukusi akifafanua kisheria na kikatiba ni kwanini uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu ni uvunjaji wa katiba ya JMT ya 1977

Video: Wakili Boniface Mwambukusi akifafanua kisheria na kikatiba ni kwanini uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu ni uvunjaji wa katiba ya JMT ya 1977

Mbona wakristo wanafanya mambo yao kwa hoja bila ata kuhusisha imani zao? Amini angekuwa ni muislam na doto muislam usingeskia kelele. Ila sisi wakristo ndio dini ya haki, tunakupasua uwe mwenzetu usiwe mwenzetu hatuangalii kabila wala dini ata kama tupo kanisa moja.
 
Kama kweli ni “mjuzi” wa sheria mbona kesi yake ilitupiliwa mbali?
Hilo analolizungumza hapo linahitaji uwe na ujuzi wa sheria kweli?

Mimi ningependa kusoma maoni yako kwenye hilo..

Sina hakika kama itakusaidia lolote kumshambulia yeye na utu wake..

Afer all, kesi hiyo "haikutupiliwa mbali" bali maamuzi yalitolewa na mahakama kuogopa kusema "Rais amekosea" badala yake ikasema "imefungwa mikono..."

Sasa sijui hata kama unaelewa maana ya mtu kusema "nimefungwa mikono".

Kama hujui, nikusaidie tafsiri yake:

Ina maana "naweza kukusaidia ila nimezuiwa".

Na Kwa upande wa mahakama, maana yake ni kuwa; "....nyie kina Boniface Mwambukusi na wenzako, mko sahihi, serikali imekosea lakini tumezuiwa kuwapa haki hiyo!!"

Kama unafikiri vizuri, basi utakuwa umeelewa...
 
Mkuu Mimi sijui Sheria kwasababu sikuisomea, lakini ABC za Katiba nazijua. Mwambukusi haijui Katiba au anapotosha kwa makusudi.
Amepotosha nini?

Parekebishe alipopotosha Kwa kadiri wewe unavyoelewa. Kusema tu ametopotosha halafu hutoi alternative hoja, huo unakuwa ni umbea..

Karibu. Sema amepotosha nini..
Halafu mtoa post kachemka. Dk. Salim aliteuliwa na Rais Mzee Mwinyi sio Mwl. Nyerere.
Hili halina shaka. Nimesharekebisha

Lakini ni kweli pia kuwa Dr Salim A. Salimu alishawahi kushika wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu, au siyo?
 
Ndiyo inawezekana na pia ilikuwepo sikumbuki tu ni nani aliyeiondoa lakini iliwepo
Nadhani unamaanisha nafasi ya Makamu wa pili wa Rais, au siyo?

Nami nakubali pia kuwa ilikuwepo kikatiba na baadaye kuuondolewa Kwa utaratibu wa kikatiba pia....

Na kwa hiyo hawezi kuunda nafasi
 
Huyu kashindwa Mahakamani Hadi Sasa hajakata Rufaa.

Alikuwa anapotosha kwamba Bandari zote kapewa DP World na TPA hairuhusiwi kutoa Tenda kwingine,Tenda imetangazwa badala aombe yupo yupo anatafuta kiki za kijinga.

Sifa zitakuja kumpoteza.
Hakushindwa...!

Mahakama ilisema "imefungwa mikono.."

Unaelewa maana ya hiyo kauli?

Ni sawa na kusema; "....ndugu uko sahihi kabisa ila nimezuiwa nisikupe ninachotakiwa kukupa..!!"

Hata hili yuko sahihi..
 
Hilo analolizungumza hapo linahitaji uwe na ujuzi wa sheria kweli?

Mimi ningependa kusoma maoni yako kwenye hilo..

Sina hakika kama itakusaidia lolote kumshambulia yeye na utu wake..

Afer all, kesi hiyo "haikutupiliwa mbali" bali maamuzi yalitolewa na mahakama kuogopa kusema "Rais amekosea" badala yake ikasema "imefungwa mikono..."

Sasa sijui hata kama unaelewa maana ya mtu kusema "nimefungwa mikono".

Kama hujui, nikusaidie tafsiri yake:

Ina maana "naweza kukusaidia ila nimezuiwa".

Na Kwa upande wa mahakama, maana yake ni kuwa; "....nyie kina Boniface Mwambukusi na wenzako, mko sahihi, serikali imekosea lakini tumezuiwa kuwapa haki hiyo!!"

Kama unafikiri vizuri, basi utakuwa umeelewa...
Ningemuona wa maana angechambua katiba inayompa mwenyekiti utawala bila kikomo🤣
 
Jaji Warioba hakuwahi kuwa waziri wala PM wakati wa Mwl. Nyerere.
Jamaa inaelekea wamesoma history sasa kachanganya madesa. Manaibu Waziri Wakuu (Salim na Mrema) wote aliteuliwa na Mwinyi. Sijui kwa nini Wazanzibar wanapenda sana wasaidizi wasaidizi au ni Umwinyi...!?
 
1. Kuna mtu humu kaweka thread yake kuhusiana na hilo kwamba baada ya Dk. Salim kuteulia Naibu Waziri Mkuu, waandishi wa habari walimuuliza Mwl. Nyerere kama Rais Mzee Mwinyi hakuvunja Katiba naye alijibu, nanukuu, "...Katiba haisemi chochote kuhusu Naibu Waziri Mkuu. Hivyo, aliteuliwa sawa na asipoteuliwa sawa...!" Mwisho wa kunukuu.

Hoja yangu ni ipi kwamba Mwambukusi aidha haijui Katiba au anapotosha ipo wazi. Yeye mwenyewe anasema Kuna vyeo vilivyotajwa Kikatiba na namna wanavyopatikana kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinaingia kwenye Katiba (36) (1) na (2) kwamba Rais anaweza kuunda nafasi na akamteua mtu kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo. Sijui umenielewa hata kama mimi sio mtaalamu wa Sheria!
 
NB: JF Moderators, naomba hii thread ijitegemee. Najua imeshajadiliwa lakini naona huyu wakili kaja kivingine. Tuwape watu nafasi wajadili hoja yake..

Back to the topic;

✍️Ni kweli Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kuunda ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na kumteua Dr Salim A. Salimu kushika wadhifa huo..

✍️Vivyo hivyo Rais ally Hassan Mwinyi aliwahi kufanya kosa la namna hii na nafasi hiyo kushikwa na Hayati Augustine L. Mrema wakati kikatiba PM akiwa John Malecela..

✍️Sasa Rais Samia Suluhu Hassan naye kafanya makosa hayahaya.

Je, makosa ya mwingine yanaweza kuhalalisha jambo?

✍️Msikilize Wakili Msomi Boniface Mwambukusi akitolea ufafanuzi wa kisheria na kikatiba wa makosa haya..👇👇👇👇
View attachment 2735582

Aliyoyasema kwa ufupi (quotes):

".....Ni kweli Rais kikatiba ana mamlaka na haki (right) ya ku - constitute na ku - abolish any office at anytime. Lakini haki na wajibu huu hau - extend kwenye office ambazo zimeanzishwa na katiba....."

".....Kwa mfano; ofisi ya PM, DPP, AG, Bunge au CAG ni ofisi za umma zilizoundwa na kuwekewa utaratibu na masharti maalumu kikatiba kuanzia katika uteuzi, utendaji na uwajibikaji wa watu wanaoteuliwa na kushika ofisi hizi..."

"....Mfano, Waziri Mkuu anapoteuliwa ni lazima athibitishwe na wananchi kupitia Bunge lao. Kwa maana hiyo, ni makosa na kwa kweli haiwezekani Rais atafute mtu mwingine kwa mlango wa nyuma (au wa uani) na amkasimishe majukumu ya kikatiba ya Waziri Mkuu. Hizo zitakuwa vurugu na ni kukiuka katiba.."

Ndugu Petro E. Mselewa, Pascal Mayalla JokaKuu denooJ Mag3 na wengine mna maoni yoyote?
Katiba ya hii nchi haiendani na mazingira ya sasa, imejaa matobo na viraka tu.
 
Rais anaruhusiwa kuunda na kuvunja wizara na mawaziri wake, kwanini ashindwe kuteua naibu PM?
Ni kwa sababu PM office imeanzishwa na katiba na wajibu au majukumu ya PM yameelezwa bayana na katiba iyo hiyo

Na katiba hiyo hiyo haisemi kutakuwa na Naibu Waziri mkuu na haielezi atakuwa na wajibu gani
Huyu Mwambukusi anawachota akili kiboya.
Sio kweli.

Ila ukweli wake ni huu, kwamba, "maboya" ni wale wasioshughulisha akili zao kuhoji kila kinachofanywa na watawala.

Je, nawe ni miongoni mwa maboya hawa?
 
Mkuu Uzima Tele I beg to differ with my learned senior Counsel. Naendelea na msimamo na maoni yangu kuwa Mhe. Rais yuko sahihi kikatiba kuanzisha na kumteua wa kushika Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu.

Nimeitaja ( na hata Wakili Mwabukusi ameitaja) ibara ya 36 (1). Inatoa mamlaka kwa Rais kuanzisha nafasi/ofisi za kimadaraka.

Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu haipo/haikutajwa kwenye Katiba. Jana ndiyo imeanzishwa. Majukumu yake yataainishwa kwenye Hati ya Kuanzishwa kwake.

Kuanzishwa kwa Ofisi hiyo hakumaanishi kuivunja, kuivuruga, kuiingilia au kuibadili Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni Ofisi mpya inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba (Ibara ya 36(1)).
Huyu Mwakubisi inabidi apate ushauri maana anapo elekea atakua kama bongo flavor. Mambo mengi aache kuyasemea kama ana uhakika nayo.
 
Mkuu Uzima Tele I beg to differ with my learned senior Counsel. Naendelea na msimamo na maoni yangu kuwa Mhe. Rais yuko sahihi kikatiba kuanzisha na kumteua wa kushika Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu.

Nimeitaja ( na hata Wakili Mwabukusi ameitaja) ibara ya 36 (1). Inatoa mamlaka kwa Rais kuanzisha nafasi/ofisi za kimadaraka.

Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu haipo/haikutajwa kwenye Katiba. Jana ndiyo imeanzishwa. Majukumu yake yataainishwa kwenye Hati ya Kuanzishwa kwake.

Kuanzishwa kwa Ofisi hiyo hakumaanishi kuivunja, kuivuruga, kuiingilia au kuibadili Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni Ofisi mpya inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba (Ibara ya 36(1)).
Huyu Mwakubisi inabidi apate ushauri maana anapo elekea atakua kama bongo flavor. Mambo mengi aache kuyasemea kama ana uhakika nayo.
 
1. Kuna mtu humu kaweka thread yake kuhusiana na hilo kwamba baada ya Dk. Salim kuteulia Naibu Waziri Mkuu, waandishi wa habari walimuuliza Mwl. Nyerere kama Rais Mzee Mwinyi hakuvunja Katiba naye alijibu, nanukuu, "...Katiba haisemi chochote kuhusu Naibu Waziri Mkuu. Hivyo, aliteuliwa sawa na asipoteuliwa sawa...!" Mwisho wa kunukuu.
Kama katiba haisemi lolote kuhusu jambo fulani maana yake kinabaki kuwa hivyo. Kuongeza au kupunguza yote yataharibu
Hoja yangu ni ipi kwamba Mwambukusi aidha haijui Katiba au anapotosha ipo wazi.
Hapotoshi bali anatumia akili yake vyema kuibua maswali ya matendo ya ajabu ya watawala Kwa kisingizio cha "katiba haisemi chochote"
Yeye mwenyewe anasema Kuna vyeo vilivyotajwa Kikatiba na namna wanavyopatikana kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Ndiyo.
Cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinaingia kwenye Katiba (36) (1) na (2) kwamba Rais anaweza kuunda nafasi na akamteua mtu kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo.
Ulikuwa na bundle kweli ukaifungua hiyo video na kuisikiliza mwanzo hadi mwisho? Yes, Rais ana power ya ku - consitute na ku - abolish office yoyote. Lakini that power is limited na kamwe hai - extend hadi kwenye nafasi za kikatiba.

Mfano Rais huyo hawezi leo hii akaamka na kuunda office ya Malkia wa nchi na kimteua mama yake awe Malkia!

Hayati Baba wa taifa hili Mwl J.K. Nyerere pamoja na ubabe wake hakuwahi ku abuse power yake Kwa kiwango hiki wanachifanya hawa sasa!
Sijui umenielewa hata kama mimi sio mtaalamu wa Sheria!
Sidhani kama Uzima Tele atakuelewa kama ambavyo hata sisi wengine hatujakuelewa
 
Ni kwa sababu PM office imeanzishwa na katiba na wajibu au majukumu ya PM yameelezwa bayana na katiba iyo hiyo

Na katiba hiyo hiyo haisemi kutakuwa na Naibu Waziri mkuu na haielezi atakuwa na wajibu gani

Sio kweli.

Ila ukweli wake ni huu, kwamba, "maboya" ni wale wasioshughulisha akili zao kuhoji kila kinachofanywa na watawala.

Je, nawe ni miongoni mwa maboya hawa?

Katiba inasemaje kuhusu Raisi kuvunja au kuunganisha wizara? Inasemaje kuhusu majukumu yao as well?
 
Mkuu Uzima Tele I beg to differ with my learned senior Counsel. Naendelea na msimamo na maoni yangu kuwa Mhe. Rais yuko sahihi kikatiba kuanzisha na kumteua wa kushika Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu.

Nimeitaja ( na hata Wakili Mwabukusi ameitaja) ibara ya 36 (1). Inatoa mamlaka kwa Rais kuanzisha nafasi/ofisi za kimadaraka.

Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu haipo/haikutajwa kwenye Katiba. Jana ndiyo imeanzishwa. Majukumu yake yataainishwa kwenye Hati ya Kuanzishwa kwake.

Kuanzishwa kwa Ofisi hiyo hakumaanishi kuivunja, kuivuruga, kuiingilia au kuibadili Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni Ofisi mpya inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba (Ibara ya 36(1)).
Hiyo office maana yake nini?

Kwamba baadhi ya majukumu ya kikatiba ya PM yatagawiwa kwa Naibu Waziri Mkuu?

Unajua pamoja na kuwa katiba yetu ya 1977 ni mbovu kwa kiasi cha kutisha, lakini wakati mwingine maamuzi yanapaswa kubebwa na hekima na busara. Ikikosekana hekima, viongozi wanaweza kuingiza nchi ktk shida kubwa sana.

Na unajua watu wengine wanaweza kusema mbona Mwinyi alifanya haya haya hakukukuwa na malalamiko kama haya?

Ni kweli, lakini hicho kilikywa kizazi kile. Kizazi hiki ni cha kuchunguza na kuhoji!

Hayati Mwl. Nyerere pamoja na nguvu na ushawishi wake aliokuwa nao wakati ule, hakuwahi kutumia madaraka yake kufanya maamuzi ya namna hii kama wafanyavyo Marais wa leo!
 
Katiba inasemaje kuhusu Raisi kuvunja au kuunganisha wizara? Inasemaje kuhusu majukumu yao as well?
Huko kwenye mawizara na office ambazo haziko ring fenced na katiba, ndiko Rais anakoweza kutumia power yake ya ku - consitute na ku - abolish office yoyote Kwa kutumia ibara hiyo ya 36 (1) - (3) lakini sio huko aendako..

Mfano hawezi kuifuta office ya CAG au AG au ya DPP ambazo ziwekwa na katiba kwa sababu na matakwa yake tu eti Kwa kuwa ana mamlaka ya ibara ya 36 (1) - (3) na kisha kuanzisha kitu kingine anachoona mwenyewe kinamfaa!
 
Wapo watakuja tu na nimemwita Kwa makusudi ndugu Petro E. Mselewa na Pascal Mayalla kwa sababu ni wanasheria ingalau Kwa sbb pia hujitambilisha hivyo hapa jukwaani..

Lakini kikubwa zaidi ni kwa sababu Wakili Boniface Mwambukusi katika wote waliolisemea jambo hili (niliowasikia mimi), jamaa huyu yeye kaja kitofauti kidogo na kufungua koki moja ya ufahamu wangu ambayo ilikuwa imefunga na ndiyo maana nikaleta hoja hii hapa jukwaani..

Hapa na mimi najiuliza ndiyo maana EL aliwekwa kwenye mtego wa kujiuzulu mwenyewe?
 
Kama katiba haisemi lolote kuhusu jambo fulani maana yake kinabaki kuwa hivyo. Kuongeza au kupunguza yote yataharibu

Hapotoshi bali anatumia akili yake vyema kuibua maswali ya matendo ya ajabu ya watawala Kwa kisingizio cha "katiba haisemi chochote"

Ndiyo.

Ulikuwa na bundle kweli ukaifungua hiyo video na kuisikiliza mwanzo hadi mwisho? Yes, Rais ana power ya ku - consitute na ku - abolish office yoyote. Lakini that power is limited na kamwe hai - extend hadi kwenye nafasi za kikatiba.

Mfano Rais huyo hawezi leo hii akaamka na kuunda office ya Malkia wa nchi na kimteua mama yake awe Malkia!

Hayati Baba wa taifa hili Mwl J.K. Nyerere pamoja na ubabe wake hakuwahi ku abuse power yake Kwa kiwango hiki wanachifanya hawa sasa!

Sidhani kama Uzima Tele atakuelewa kama ambavyo hata sisi wengine hatujakuelewa
Unaendeleza tu mjadala bila mantiki. Kwani hiyo 36 (1) na (2) inazungumzia nafasi zipi? Mbona mnakuwa wagumu wa kuelewa?
 
Unaendeleza tu mjadala bila mantiki. Kwani hiyo 36 (1) na (2) inazungumzia nafasi zipi? Mbona mnakuwa wagumu wa kuelewa?
Kwani wewe unaelewa nini boss?

Kuna kusoma na kuelewa bila kujua tafsiri yake. Lakini Kuna kusoma na kuichakata mantiki..!

Wewe bila shaka umesoma na kuelewa hivyo hivyo bila tafsiri ya kimantiki, au siyo?

Ndiyo maana kukitokea mikanganyiko kama huu watu huenda mahakamani. Huko mahakamani hawaendi kusoma na kuelewa tu kama ulivyoelewa wewe na Samia bali kupata tafsiri na maana pana ya kimantiki ya kitu hiyo..

Mjadala na uendelee..................
 
Back
Top Bottom