Video: Wakili Boniface Mwambukusi akifafanua kisheria na kikatiba ni kwanini uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu ni uvunjaji wa katiba ya JMT ya 1977

Video: Wakili Boniface Mwambukusi akifafanua kisheria na kikatiba ni kwanini uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu ni uvunjaji wa katiba ya JMT ya 1977

Vipi kuhusu bajeti ya Ofisi hii mpya kuwa hazikupitishwa na bunge?
Je mamlaka ya Rais kutumia fedha ambazo bunge halijapitisha yanatoka kwenye kifungu kipi cha katiba/sheria?
Hivi kuna bajeti ya ofisi ya Naibu Waziri kumbe? Sio bajeti ya Wizara husika?
 
Why walimnyima mrema kiinua mbongo chake... "....".
Sababu nafasi yake ile haikuwepo kwa mujibu wa katiba hata astahili mafao ya kikatiba..

Ilipoundwa hiyo nafasi, alipata mshahara wa kawaida lakini hawezi kuingia kwenye mafao ya kikatiba kwa sababu katiba haimtambui..

Ndiyo maana tunasema office zilizoanzishwa na katiba, hata appointment, utendaji na utokaji wa watendaji wake unafanyika kwa mujibu wa katiba...

Yeye Rais Samia Suluhu Hassan angeunda ofisi kwa jina jingine lolote Wala kusingekuwa na shida..!

All in all Wakili Boniface Mwambukusi anajaribu tu kuthibitisha matobo yaliyo ktk katiba yetu iliyopitwa na wakati ya mwaka 1977...!!
 
Mkuu katiba inasemaje kuhusu NAIBU JAJI MKUU au KAIMU JAJI MKUU?
 
Mkuu Uzima Tele I beg to differ with my learned senior Counsel. Naendelea na msimamo na maoni yangu kuwa Mhe. Rais yuko sahihi kikatiba kuanzisha na kumteua wa kushika Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu.

Nimeitaja ( na hata Wakili Mwabukusi ameitaja) ibara ya 36 (1). Inatoa mamlaka kwa Rais kuanzisha nafasi/ofisi za kimadaraka.

Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu haipo/haikutajwa kwenye Katiba. Jana ndiyo imeanzishwa. Majukumu yake yataainishwa kwenye Hati ya Kuanzishwa kwake.

Kuanzishwa kwa Ofisi hiyo hakumaanishi kuivunja, kuivuruga, kuiingilia au kuibadili Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni Ofisi mpya inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba (Ibara ya 36(1)).

Hii ndio shida ya watu mliosoma HKL... kwa hiyo kesho rais akianzisha cheo cha Deputy Vice President... napo itakuwa sawa tu.
 
Mkuu katiba inasemaje kuhusu NAIBU JAJI MKUU au KAIMU JAJI MKUU.
Hii haina mgogoro wowote kwa sababu iko kikatiba ibara 109 (10) - (12)👇👇

Lakini kumbuka katiba haisemi "NAIBU JAJI MKUU" Bali inamtaja na kumtambua "KAIMU JAJI". "Kaimu" na "Naibu" ni maneno mawili tofauti yenye maana tofauti kabisa..

Kukaimu ni kushikilia nafasi fulani kwa muda na ajapo au arudipo mwenye nafasi, ukaimu unaishia hapo...

Lakini kuwa "naibu" Kwa kiingereza "deputy", maana yake ni kuwa msaidizi wa............... na utakuwepo pale hadi muda (tenure) yako itakapokwisha..
Screenshot_20230902-015416.png

Hii ya Naibu Waziri Mkuu haipo kokote kwenye katiba. Ni ujanja ujanja tu wa ma - Rais kuumba cheo hiki Kwa manufaa yao
 
Hii haina mgogoro wowote kwa sababu iko kikatiba ibara 109 (10) - (12)[emoji116][emoji116]

Lakini kumbuka katiba haisemi "NAIBU JAJI MKUU" Bali inamtaja na kumtambua "KAIMU JAJI". "Kaimu" na "Naibu" ni maneno mawili tofauti yenye maana tofauti kabisa..

Kukaimu ni kushikilia nafasi fulani kwa muda na ajapo au arudipo mwenye nafasi, ukaimu unaishia hapo...

Lakini kuwa "naibu" Kwa kiingereza "deputy", maana yake ni kuwa msaidizi wa............... na utakuwepo pale hadi muda (tenure) yako itakapokwisha..
View attachment 2736137

Hii ya Naibu Waziri Mkuu haipo kokote kwenye katiba. Ni ujanja ujanja tu wa ma - Rais kuumba cheo hiki Kwa manufaa yao
Wapi wamezuia kikatiba kwamba hapapaswi kuwa na Naibu Waziri Mkuu? Vipi kwenye katiba kuna sehemu inasema Wizara ziwe na manaibu Mawaziri wawili? Na je Naibu Waziri anaingia kwenye Kikao cha Baraza la Mawaziri?
 
Huko kwenye mawizara na office ambazo haziko ring fenced na katiba, ndiko Rais anakoweza kutumia power yake ya ku - consitute na ku - abolish office yoyote Kwa kutumia ibara hiyo ya 36 (1) - (3) lakini sio huko aendako..

Mfano hawezi kuifuta office ya CAG au AG au ya DPP ambazo ziwekwa na katiba kwa sababu na matakwa yake tu eti Kwa kuwa ana mamlaka ya ibara ya 36 (1) - (3) na kisha kuanzisha kitu kingine anachoona mwenyewe kinamfaa!

Lakini anaweza kuvunja wizara na mawaziri wake sio... nini cha ajabu kuteua vice PM?
 
Halafu ukae uwasikilize hawa, hutofanya chochote mpaka unaondoka madarakani
 
Wapi wamezuia kikatiba kwamba hapapaswi kuwa na Naibu Waziri Mkuu?
Hakuna.

Katiba inaunda na kuitambua office ya Waziri Mkuu.

Kama hiyo haitajwi maana ya haipo na huwezi kuisaidia katiba..
Vipi kwenye katiba kuna sehemu inasema Wizara ziwe na manaibu Mawaziri wawili? Na je Naibu Waziri anaingia kwenye Kikao cha Baraza la Mawaziri?

Jibu la swali lako utalipata ukijibu swali hili 👇👇kwa ufasaha.

KWAMBA; Ni wapi ktk katiba zimeorodheshwa wizara na nafasi za mawaziri na manaibu?

Hilo la Naibu Waziri kuingia kwenye Kikao cha cabinet au la, labda mtafute Naibu Waziri mmoja umuulize maana ni kana kwamba hukusoma hata CIVICS ya form one & two wewe.!
 
Sawa, lakini mimi bado naendelea kukubaliana na mwanasheria mwenzako huyu based on the fact kwamba;

1. Ofisi zilizoanzishwa kikatiba zinapaswa kuwa intact vilevile. Haipaswi Rais kuitumia ibara ya 36 kimakosa kwa kuingiza mtu mwingine kwa mlango wa nyuma Kwa nafasi ileile na Kwa jina la cheo kilekile. Hizi ni vurugu..!

2. Kama Rais ameona kuwa PM anahitaji mtu wa kumsaidia, na aitwe "Naibu Waziri Mkuu", apeleke amendment ya katiba..

3. La anaona shida, na ameona ktk serikali yake kuna mambo yanahitaji kuundiwa wizara, hilo liko ndani ya mamlaka yake kikatiba kuanzisha wizara na kumteua waziri ashughulikie hayo LAKINI SIO KUM - SABOTAGE PM ambaye yupo pale kikatiba...!!

Nakubaliana na Boniface Mwambukusi..
Maelezo ya mwakabusi yako wazi na yanaeleweka.Ya hao wengine yanalazimishiwa tu na kuungwa ungwa ilimradi kuficha mapungufu yaliyofanyika.
 
NB: JF Moderators, naomba hii thread ijitegemee. Najua imeshajadiliwa lakini naona huyu wakili kaja kivingine. Tuwape watu nafasi wajadili hoja yake..

Back to the topic;

✍️Ni kweli Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kuunda ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na kumteua Dr Salim A. Salimu kushika wadhifa huo..

✍️Vivyo hivyo Rais ally Hassan Mwinyi aliwahi kufanya kosa la namna hii na nafasi hiyo kushikwa na Hayati Augustine L. Mrema wakati kikatiba PM akiwa John Malecela..

✍️Sasa Rais Samia Suluhu Hassan naye kafanya makosa hayahaya.

Je, makosa ya mwingine yanaweza kuhalalisha jambo?

✍️Msikilize Wakili Msomi Boniface Mwambukusi akitolea ufafanuzi wa kisheria na kikatiba wa makosa haya..👇👇👇👇
View attachment 2735582

Aliyoyasema kwa ufupi (quotes):

".....Ni kweli Rais kikatiba ana mamlaka na haki (right) ya ku - constitute na ku - abolish any office at anytime. Lakini haki na wajibu huu hau - extend kwenye office ambazo zimeanzishwa na katiba....."

".....Kwa mfano; ofisi ya PM, DPP, AG, Bunge au CAG ni ofisi za umma zilizoundwa na kuwekewa utaratibu na masharti maalumu kikatiba kuanzia katika uteuzi, utendaji na uwajibikaji wa watu wanaoteuliwa na kushika ofisi hizi..."

"....Mfano, Waziri Mkuu anapoteuliwa ni lazima athibitishwe na wananchi kupitia Bunge lao. Kwa maana hiyo, ni makosa na kwa kweli haiwezekani Rais atafute mtu mwingine kwa mlango wa nyuma (au wa uani) na amkasimishe majukumu ya kikatiba ya Waziri Mkuu. Hizo zitakuwa vurugu na ni kukiuka katiba.."

Ndugu Petro E. Mselewa, Pascal Mayalla JokaKuu denooJ Mag3 na wengine mna maoni yoyote?
Duh
 
Lakini anaweza kuvunja wizara na mawaziri wake sio... nini cha ajabu kuteua vice PM?
Hakuna ajabu lakini kumbuka kuwa hakuna wizara chini ya Naibu Waziri mkuu

Kikatiba tuna PM mmoja tu na katiba haijampa naibu.

Rais hawezi kuivunja au kuiondoa au kuifanyia amendments yoyote office ya PM unless awe na directives za kikatiba.
 
Back
Top Bottom