Video: Wakili Boniface Mwambukusi akifafanua kisheria na kikatiba ni kwanini uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu ni uvunjaji wa katiba ya JMT ya 1977

Vipi kuhusu bajeti ya Ofisi hii mpya kuwa hazikupitishwa na bunge?
Je mamlaka ya Rais kutumia fedha ambazo bunge halijapitisha yanatoka kwenye kifungu kipi cha katiba/sheria?
Hivi kuna bajeti ya ofisi ya Naibu Waziri kumbe? Sio bajeti ya Wizara husika?
 
Why walimnyima mrema kiinua mbongo chake... "....".
Sababu nafasi yake ile haikuwepo kwa mujibu wa katiba hata astahili mafao ya kikatiba..

Ilipoundwa hiyo nafasi, alipata mshahara wa kawaida lakini hawezi kuingia kwenye mafao ya kikatiba kwa sababu katiba haimtambui..

Ndiyo maana tunasema office zilizoanzishwa na katiba, hata appointment, utendaji na utokaji wa watendaji wake unafanyika kwa mujibu wa katiba...

Yeye Rais Samia Suluhu Hassan angeunda ofisi kwa jina jingine lolote Wala kusingekuwa na shida..!

All in all Wakili Boniface Mwambukusi anajaribu tu kuthibitisha matobo yaliyo ktk katiba yetu iliyopitwa na wakati ya mwaka 1977...!!
 
Mkuu katiba inasemaje kuhusu NAIBU JAJI MKUU au KAIMU JAJI MKUU?
 

Hii ndio shida ya watu mliosoma HKL... kwa hiyo kesho rais akianzisha cheo cha Deputy Vice President... napo itakuwa sawa tu.
 
Mkuu katiba inasemaje kuhusu NAIBU JAJI MKUU au KAIMU JAJI MKUU.
Hii haina mgogoro wowote kwa sababu iko kikatiba ibara 109 (10) - (12)👇👇

Lakini kumbuka katiba haisemi "NAIBU JAJI MKUU" Bali inamtaja na kumtambua "KAIMU JAJI". "Kaimu" na "Naibu" ni maneno mawili tofauti yenye maana tofauti kabisa..

Kukaimu ni kushikilia nafasi fulani kwa muda na ajapo au arudipo mwenye nafasi, ukaimu unaishia hapo...

Lakini kuwa "naibu" Kwa kiingereza "deputy", maana yake ni kuwa msaidizi wa............... na utakuwepo pale hadi muda (tenure) yako itakapokwisha..


Hii ya Naibu Waziri Mkuu haipo kokote kwenye katiba. Ni ujanja ujanja tu wa ma - Rais kuumba cheo hiki Kwa manufaa yao
 
Wapi wamezuia kikatiba kwamba hapapaswi kuwa na Naibu Waziri Mkuu? Vipi kwenye katiba kuna sehemu inasema Wizara ziwe na manaibu Mawaziri wawili? Na je Naibu Waziri anaingia kwenye Kikao cha Baraza la Mawaziri?
 

Lakini anaweza kuvunja wizara na mawaziri wake sio... nini cha ajabu kuteua vice PM?
 
Halafu ukae uwasikilize hawa, hutofanya chochote mpaka unaondoka madarakani
 
Wapi wamezuia kikatiba kwamba hapapaswi kuwa na Naibu Waziri Mkuu?
Hakuna.

Katiba inaunda na kuitambua office ya Waziri Mkuu.

Kama hiyo haitajwi maana ya haipo na huwezi kuisaidia katiba..
Vipi kwenye katiba kuna sehemu inasema Wizara ziwe na manaibu Mawaziri wawili? Na je Naibu Waziri anaingia kwenye Kikao cha Baraza la Mawaziri?

Jibu la swali lako utalipata ukijibu swali hili 👇👇kwa ufasaha.

KWAMBA; Ni wapi ktk katiba zimeorodheshwa wizara na nafasi za mawaziri na manaibu?

Hilo la Naibu Waziri kuingia kwenye Kikao cha cabinet au la, labda mtafute Naibu Waziri mmoja umuulize maana ni kana kwamba hukusoma hata CIVICS ya form one & two wewe.!
 
Maelezo ya mwakabusi yako wazi na yanaeleweka.Ya hao wengine yanalazimishiwa tu na kuungwa ungwa ilimradi kuficha mapungufu yaliyofanyika.
 
Duh
 
Lakini anaweza kuvunja wizara na mawaziri wake sio... nini cha ajabu kuteua vice PM?
Hakuna ajabu lakini kumbuka kuwa hakuna wizara chini ya Naibu Waziri mkuu

Kikatiba tuna PM mmoja tu na katiba haijampa naibu.

Rais hawezi kuivunja au kuiondoa au kuifanyia amendments yoyote office ya PM unless awe na directives za kikatiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…