Video: Wamasai wazichapa tena na Walinzi (Wajeruhi)

Video: Wamasai wazichapa tena na Walinzi (Wajeruhi)

kwani hawa wamasai wameanza kuuza shanga hapo zenj tarehe ngapi,mwezi wa ngapi na mwaka upi shekh??? mbona siku za nyuma kulikuwa hamna kelele kama izi!!! iko ivi, vijana wa kizanzbar wengi ni wavivu,kazi yao ni kusikiliza taarab na kuuza ngada huko beach,wengine wana imani kali za kiislam kiasi kumuudumia mtalii mwenye bikini wanaona ni kharam,then wakipewa shoo na madem wa kitasha bao moja tuutaskia YALAAAA!!then anajitupa pembeni kama bata,tofauti na wamasai!!!
Ungeharibu kujikita kwenye hoja yangu ungetoka na kitu, mimi napingana na sheria nzima ya beach ni public, unajua gharama kumconvice mgeni mpaka afanye booking na hoteli yako, alafu akishafika wanajitokeza wapuuzi Wachache wanaojiita Beach boy na kuanza kuwaghasi wageni, mgeni anakuplain kwa uongozi wa hotel, hotel itawaeleza walinzi wake kuhahakikisha wageni hawasumbuliwi. Wajibu wa mlinzi nikumweleza masai asiwaghasi wageni, masai haelewi, mlinzi afanye nini? Lakini wakifika TP masai huondoka. Wageni wananunua fukwe na si kitanda wala chakula
 
Na nyie huku bara mmejaa mnauza simu mbovu kkoo mmejaa na vihotel vyenu ila hamuoni kwamba mnatubana sisi tukiamua tuwakimbize bongo mtakuja kutulamba miguu.Kama kuna wabara wanatafuta maisha huko waacheni km tulivo waacha mtuuzie vifaa used mbofu mbofu huku bara
Huelewa wako umeishia hapo. Yawezekana hata kariakoo unaiona mtandaoni tu
 
Ungeharibu kujikita kwenye hoja yangu ungetoka na kitu, mimi napingana na sheria nzima ya beach ni public, unajua gharama kumconvice mgeni mpaka afanye booking na hoteli yako, alafu akishafika wanajitokeza wapuuzi Wachache wanaojiita Beach boy na kuanza kuwaghasi wageni, mgeni anakuplain kwa uongozi wa hotel, hotel itawaeleza walinzi wake kuhahakikisha wageni hawasumbuliwi. Wajibu wa mlinzi nikumweleza masai asiwaghasi wageni, masai haelewi, mlinzi afanye nini? Lakini wakifika TP masai huondoka. Wageni wananunua fukwe na si kitanda wala chakula
ok!!!!,kwani hamna wachuuzi wa kizanzibar???? au ni wamasai tu?? mbona video haionyeshi wamasai wakiwa na shanga??
 
Mnawachokoza, hao jamaa ni wastarabu ichuliwe kama watu wengine.. How comes fights daily ila watu hawatajwi kwa makabila yao ila akigombana mmasai anatajwa kwa kabila lake..

Wamasai kwani wameanza kuingia juzi hapo Zanzibar!? Wapo miaka kwa miaka ishu ndogo basi anahusisha kabila zima.

Tubadilike kabisa hili suala halina mantiki kwa watanzania wenzetu, mpaka sasa kama vile wametengwa kwa nasaba yao, kila tukio lao linapewa shtuma kwa wote.. kakae kariakoo kutwa watu wanaopigana wanajulikana makabila ya mbona hawatajwi...
Masai wastaarabu wanapatikana wapi? Me mkulima nawajua, ni watu washenzi sana.

Hawa masai hata waliopo huku bara inabidi warudishwe kwao Arusha tu wakaishi na wanyama huko, waache kutusumbua.
 
Wana Vitu vingi sana wanavyitusaidia Sema Kuvisema hadharani ni kuhatarisha usalama wa Nchi yetu"

Alisikika mlevi mmoja akisema baada ya kushiba Kitimoto na Wine yake
Huo ni uongo.
ZANZIBAR NI MNUFAIKA MKUBWA WA MUUNGANO KULIKO TANGANYIKA.
WAPO WANAOFANYA KAZI SERIKALINI NA WAMELITHIBITISHA HILO NA NAWAJUA.
KAMA UNATAKA NAKUTAJIA.
 
Mi nikajua wanapigana maeneo ya mjini, hapo ni sawa kupigwa kwa sababu sizani kama ni suala la ubaguzi, hapo viongozi wengi wa hotel hawapendi mabichi boi sababu wanasumbua wageni, walinzi wanapewa order ya kuzuia zuia hao Masai pamoja na bichi boi wasisumbue wageni, lakini nao wanatafuta riziki lazima wawasumbue wageni ili wapate ela.

Hapo itakuwa Kuna shida ya kupishana lugha tu, ila Ili suala alihusiani na uzanzibar na ubara.
Sababu hata mabichi boi wa kizanzibar wapo hapo, nao wanazuiliwa pia, na ngumi Huwa zinatakankuchapwa nawengine wanapambana, mleta Uzi ni mzindiki anawakandia wamasai
 
Nini kifanyike kuepusha matukio kama haya kwenye jamii yetu?
Mbele ya wageni
Screenshot_20240207_120246_Samsung Internet.jpg
 
Wamechoka kunyanyaswa na kunyanyapaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshana issue hapa si kunyanyapaliwa tatizo la wamsai znz ni suala la muda tu, hawa Jamaa wamekosa ustaraabu kabisa huku znz, wanaghasi sana wageni wakiamini kupata wanawake wa kizungu, hawajali kabisa privacy za wageni. Kumfuata mgeni mpaka kwenye sunbed kwao si issue tena. Siyo wageni wote wanafurahia hizo tabia, kinachofuata mgeni akiondoka wakati wa kujaza comment card halicomend hotel kwa sababu tu ya kughasiwa na masai. Biashara kwa sasa imebadilia iko kimtandao zaidi, mgeni akishaenda TripAdvisor na kucoment usumbufu wa beach boys. Tayari hotel inakuwa imedrop. Then what next??
 
Na hii ndo ishu inayoleta ugomvi, ila mjinga mmoja analeta Uzi kwa kusema shida ni uzanzibar na ubara,
 
wamasai wamekuwa wanagasi sana wageni, siyo kila mgeni anataka kununua shanga, lakini masai wakielezwa hawaelewi
Ina maana wageni wanaòkuja Zanzibar ni tofauti na wanaoenda Ngorongoro kwa wamasai?

Halafu hii kauli yako inatofautiana ns ya msemaji wa serikali ya huko, yeye alisema kubeba silaha (rungu na sime) ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.
Haya ya kuwaghasi watalii ni mengine.
Hizi chuki mnazopanda mtavuna muda sio mrefu ujao...na mlivyojazana huku bara malipizi yatakuwa rahisi sana.
 
Ungeharibu kujikita kwenye hoja yangu ungetoka na kitu, mimi napingana na sheria nzima ya beach ni public, unajua gharama kumconvice mgeni mpaka afanye booking na hoteli yako, alafu akishafika wanajitokeza wapuuzi Wachache wanaojiita Beach boy na kuanza kuwaghasi wageni, mgeni anakuplain kwa uongozi wa hotel, hotel itawaeleza walinzi wake kuhahakikisha wageni hawasumbuliwi. Wajibu wa mlinzi nikumweleza masai asiwaghasi wageni, masai haelewi, mlinzi afanye nini? Lakini wakifika TP masai huondoka. Wageni wananunua fukwe na si kitanda wala chakula
Una point nzuri. Bahati mbaya chuki ya muungano imeshaota mizizi. Imefunika uhuru wa fikra na mitazamo isiyo na chembe ya prejudice.

Sheria inapaswa kuwa kali kuweka katazo la watanzania wa jamii zote kuwasumbua watalii wanapokua ndani ya fukwe binafsi. Kwa zile fukwe public ni jukumu la mtalii mwenyewe na wenyeji wake kuangalia usalama wao.

Kinachotokea sasa si tu watanzania wa jamii ya kimasai bali na wazawa wa hapo kupenya katika hizi fukwe zilizohodhiwa na kuwasumbua na kuwahadaa watalii.
 
Hii Kitu nimeenza kuiona Sio Ishu ya Domestic tena ukiangalia kwa jicho la kiinteligensia utagundua mambo machache..

Kwanini Hii kitu itokee sasa?
Wakati sheria ya Kuzuia silaha ni ya Muda Mrefu?
Kwanini wamasai Ghafla wamekuwa A bit more Causative wa Violence?
Kwanini wanaopigwa Ni walinzi au Askari?
Kwanini hawapigani wao kwa wao?

Kuna kitu nakihisi si kizuri kinafanyika kwa Ajili ya Muungano..

Kuna kitu kinatengenezwa sio kizuri Nikisema maneno kama SOWING DISCORD au FOMENTING DISCORD.. Kwa waliosoma Diplomasy au Political Science...Watanielewa Zaidi..

Hii ni conflict ya kutengeneza Ili baadaye iwe kubwa na ilete Hisia baina ya Watanganyika na Wazanzibar Mwisho wa siku Tuharibu Muungano..

Kuna kiti kinasukwa matokeo yake yanaweza yasionekane sasa hivi ila Trust me Yatakuwa makubwa sana..

Wanaweza Wakafukuza wamasai wote kwa kufanya Resolution (Cause and effects)..
Lakini inasikitisha sana kufanya sowing kwa kutumia Watu wenye Roho zao.bila kujali kama watapoteza Roho zao..

Kuna Ajenda kubwa sana "A sowing Discord" Imatengenezwa
Umejielekeza vibaya tukio dogo kabisa hilo.
 
Wamasai ukiwaanza ni wabaya sana. Kuna Muingereza mmoja alindika kitabu kinachowahusu hao jamaa "The silent barbarians of East Africa" anawaelezea vizuri.

Ni wapole ila wanaweza kukula nyama ukizingua 😅
 
Huyu aliye record hii video alikuwa na njaa au maana muda wote Ana zungusha tuu simu hatuoni video vizuri. Next time record vizuri ili tuone mtu akichapika kisawasawa maana tumechoka uonevu kwenye hii nchi.
 
Back
Top Bottom