Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 829
- 1,564
Mkuu unapoongelea Kamisheni ya utalii inamaanisha ni idara ndani wizara ya utalii na mali kale ambayo iko chini ya SMZ. SMZ ni CEO ambaye ana Directors, Managers nk. ( Nikuulize unawezaje kuitenga wizara yoyote na serikali?)Kitu kimoja nimekuelewa ila, unaposema tourist commission ndiyo inahusika na beach plot sidhani but ni SMZ, kweli lengo ni kuwa na usawa wa matumizi ya fukwe kwa watu wote.
Kunbuka majority kubwa ya ndugu zako wazanzibari ni wavivu na hawana ubunifu, kitu kinachofanya hili unalosema kuwa "Sheria zao nyingi zimetungwa kuwabeba wazanzibar lakini...", so walio nje wameona fulsa lazima waifanyie kazi, siyo kuzuia kwamba hapa 'maasai asifike'
Jambo lingine, faragha ya mtalii kwanza ipo kwenye hoteli aliyofikia baada ya kusoma reviews and hotel environments kabla hajaja, ukitaka commission ndiyo uzuie hicho unachotaka nadhani wewe ndiye utakuwa unaingilia faragha za watu sasa, yaani unawapangia 🤔!.
Point of within; issue ya walinzi na masai kuleteana ugomvi ndipo kuna shida ikisababishwa na eneo huru la ufukweni.
Bahati mbaya sana mmejikita kwenye Uzanzibari na Ubara haliangalii jambo kwa uhalisia wake, mimi sina chembe yoyote ya Uzanzibar ni mdau wa utalii nipo kwa ajili ya kusaka tonge na naongelea uhalisia kwenye field kama siyo ground. Kutoka hapa znz kurudi kwetu si chini ya km 100 na zaidi.
Miongozo ya utalii iko wazi kuwa znz ni Archepalago hivo sheria ya uhifadhi imetoa mwanya kwa mahoteli kujenga mpaka baharini kwa malipo fulani. Pamoja na yote hayo kumbuka beach ni maeneo ambayo yanategemea low na high tides, hivo kuna wakati yale maeneo ya reserve ya hotel yanakuwa almost covered na maji hivo vitanda na miamvuli ya kupumzika wageni inakuwa karibu sana maeneo ya umma, hii haimpi beach boy ama beach girl kuingilia faragha ya mgeni kwa sababu yoyote ile.
Hili ni suala la muda acha waendelee kufanya vurugu ili hii Tourism Police iamke na kufanya kazi manake naona tangu imeundwa ni kama imelala. Na haya yakiendelea SMZ haiwezi kushindana na Investors lazima tu masai ndo watakaoumia.
Nenda hotel zoote zilizoko kwenye fukwe za Dar uangalie kama beach boy na beach girl wanatamba kama znz.