tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, afande mmoja kutoka Dawati la Jinsia ameonekana akitoa nasaha kwa wanawake wa Mlandizi huku akiwashangaa kwa vitendo vyao vya ajabu wanavyofanya mbele za watoto wao.
Wanawake hao, ambao ni wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali wilayani humo, wameaswa kuacha kuwa mifano ya ovyo kwa watoto wao, ikiwa ni pamoja na kushare wanaume na mabinti zao.
Sitaki kuwapotezea muda kwa sababu muda ni mchache, hebu msikilze afande wewe mwenyewe hapo chini akitiririka bila kupepesa macho wala kutikisa masikio.
MAONI YANGU
Hawa wazazi kwa kweli wameshindikana kabisa. Ifike wakati serikali ianze kutoa elimu ya unyago kwa wazazi kwa lazima, kama vile inavyowalazimisha wahitimu wa kidato cha sita kwenda JKT. Ikiwa serikali italifumbia macho suala hili, tutarajie kuwa na kizazi cha ovyo sana miaka michache ijayo.