Video: Wanawake wa Mlandizi wanachangia wanaume na mabinti zao

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, afande mmoja kutoka Dawati la Jinsia ameonekana akitoa nasaha kwa wanawake wa Mlandizi huku akiwashangaa kwa vitendo vyao vya ajabu wanavyofanya mbele za watoto wao.

Wanawake hao, ambao ni wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali wilayani humo, wameaswa kuacha kuwa mifano ya ovyo kwa watoto wao, ikiwa ni pamoja na kushare wanaume na mabinti zao.

Sitaki kuwapotezea muda kwa sababu muda ni mchache, hebu msikilze afande wewe mwenyewe hapo chini akitiririka bila kupepesa macho wala kutikisa masikio.


Your browser is not able to display this video.

MAONI YANGU
Hawa wazazi kwa kweli wameshindikana kabisa. Ifike wakati serikali ianze kutoa elimu ya unyago kwa wazazi kwa lazima, kama vile inavyowalazimisha wahitimu wa kidato cha sita kwenda JKT. Ikiwa serikali italifumbia macho suala hili, tutarajie kuwa na kizazi cha ovyo sana miaka michache ijayo.
​
 
Mungu anawaona hawa wanawake. Haya matendo wanayofanya ni chukizo duniani na mbinguni.
 
WAZAZI WENYEWE NAO NI VISICHANA!....
 
Kama mtu ambae nishawahi kuishi Mkoa wa Pwani, eneo la mlandizi pamoja na Bagamoyo, mtaa wa mji mwema, Afande yuko sahihi kabisa. Hizo sehemu zina laana usiku. Na ni moja ya sehemu zinaongoza kwa maambukizi ya UKIMWI nadhani. Taarifa za TACAIDS zinaweza ku backup taarifa yangu.
 
Aisee
 
Hapo Mlandizi ni Uzaramoni, hayo mambo siyo mageni labda Afande ndiyo mgeni na mambo haya
 
Hapo Mlandizi ni Uzaramoni, hayo mambo siyo mageni labda Afande ndiyo mgeni na mambo haya
Afande naye anaonekana ni mweneji wa eneo hilo. Mbona mambo ya huko anayajua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…