Video ya CCTV camera ikionyesha utekaji wa Peter Richard Mushi Kariakoo

Video ya CCTV camera ikionyesha utekaji wa Peter Richard Mushi Kariakoo

Attachments

  • 1000020485.jpg
    1000020485.jpg
    12.1 KB · Views: 8
Mbona hatujawahi kusikia hizo kesi za wanawake matapeli kutekwa kwenda kupewa adhabu za kingono na wanaume waliowatapeli ?
Mwanaume kumkamata mwanamke ahitaji kukodi jeshi la wanaume.
Kwa simu tu unamchukua tapeli aliyekula nauli yako unaenda kumpiga mtungo tofauti na kumkamata mwanaume.
 
Suala si sababu ya kutekwa, suala ni tukio la kutekwa bila watekaji kukamatwa. Kutekana tekana si mambo ya kuhalalisha hata kama wanaotekwa ni matapeli au watembea na wake za watu.
Tupo pamoja! Wewe ndo umewapa serikali lawama wanazostahili kwenye huu uzi.
 
Huyu kwenye video Anaitwa Peter Richard Mushi ni fundi simu Kariakooalipigiwa simu tarehe13/8/2026 na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja anahitaji kutengenezewa simuAlimwelekeza alipo lakini mteja akataka ndugu peter amfuate maeneo ya china plaza alipofika china plaza Alikutana na huyo mteja aliyekuwa anampigia simu kumbe hawakuwa wateja bali ni watekaji walikuja na gari toyota crown rangi nyeupe aina plate namba ndugu wamezunguka vituo vyote vya police hospitali zote mochwari zote bila kupata majibu

Pia soma: Kijana Tosh wa Kariakoo apotea kusikojulikana baada ya kupigiwa simu na mteja wake akampokee
Kuna fundi alichonifanyia kwenye gari yangu, Mungu Tu ndiye anajua lakini matukio mengine unaweza kuwa ni visasi, watu wanakufanyia tukio ambalo kiukweli unatanani ulipize
 
Ujanja ujanja mtu anakuuizia kitu kibovu huku akijua kabisa wenyewe wanasema " Nimempiga Mshamba huyu"

Sasa kuna watu wengine hawamwachii Mungu
Mwisho wa siku wanasingiziwa serikali ndo wameteka.

Wakati hapo serikali wanapaswa kupewa lawama za kwanini hawadhibiti vitendo vya utekaji na ujambazi.
 
Mnapenda kufarijiwa uongo! Ili moyo wako usuuzike basi adui yako atupiwe lawama zote za kweli hadi za uongo.
Sababu zako zote unazoandika hapa hazina maana.

Mtu akijua ana kosa amefanya kwa mwingine hawezi kukubali kuambiwa njoo sehemu fulani unitengenezee simu, lazima angechukua tahadhari ya kujilinda.

Wewe na kichwa chako kinachowaza mapenzi ndio unaamini mwenye kosa anaweza kujipeleka kama kuku sehemu aliyoitwa huku akijua anawindwa.

Unaleta habari za kufarijiwa hapa hatupo kitandani, unawaza sana mapenzi.
 
Back
Top Bottom