Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Hakuna kitu kama hicho mkuu, kigoma kwenyewe kila mtu anasema "nasikia kuna mtu alikuwa hivi au vile"
Kuna mambo yako hivi au vile, cha ajabu huyo anayeongea, unakuta nayeye alisikia tu.

Kuna eneo fulani pale kijijini kwetu, ilikuwa inasemekana huwa inapita treni nyakati za usiku wa saa saba mpaka saa tisa.
Na wakawa wanasema hiyo treni huwa inatoa misukule burundi na kongo.
kijijini kwetu hakuna reli ya kupitisha treni, nikajisemea, "mimi nitaenda hilo eneo kuiangalia hiyo treni yenye misukule"
Kwakweli nilifululiza kama wiki hivi eneo lile nyakati za usiku wa manane na sikuiona hiyo treni.

Story karibu zote za mambo ya ushirikina zipo hivyo- hearsay. Kila mtu anayekwambia naye kasimuliwa. Zingine kama hii ya CCTV ukifanya tafakuri kidogo tu unagundua hamna kitu hapa.

Hawa watu walishindwa kutoa jina kabisa including mleta uzi mwenyewe ila karibu watu wote kwenye ule uzi, kama ilivyo kawaida ya mitanganyika, iliamini.
 
Mkuu kama nakumbuka wewe ndo ukiwahi hadi kulala makaburini lakini wapi 🤣🤣 ukawa unaenda yale maeneo watu wanayoyaogopa kwa stori za kutisha lakini bado hukupata unachokitaka au si wewe?
Watu wote husema hivyo!
Watu wote husema, "nenda sehemu fulani kuna wataalamu wa hayo mambo"
Cha ajabu unaweza kwenda sehemu husika, na aliyekwambia uende hiyo sehemu,
asikuonyeshe hao wachawi.
Sana sana ataishia kukuletea janja janja ambazo hazina msingi.
 
Back
Top Bottom