Video ya Rais wa Sudan Kusini akitokwa na haja ndogo yazua maswali kuhusu afya za viongozi

Video ya Rais wa Sudan Kusini akitokwa na haja ndogo yazua maswali kuhusu afya za viongozi

Wewe unasema hali ya huyo Rais kitokwa na mkojo hadharani kwamba kadhalilika, mimi nasema hivi; kudhalilika kunategemea na mazingira, huyo Rais ni mgonjwa na ugonjwa huo ni maarufu sana hivyo jambo likimtokea mgonjwa kwa Sababu ya huo ugonjwa hapo hakuna udhalilifu kwasababu ni Ugonjwa ndio umesababisha jambo hilo, udhalilifu unakuja katika mazingira yasiyokuwa ya Ugonjwa mfano nikakupa kwamba kama huyo Raisi angekuwa kanywa pombe na mkojo ukamtoka kwa bahati mbaya au kwa kusudi au akajiharishia hapo ndipo lugha ya udhalilifu inaingia, chukua mfano huu; kama badala ya kujikojolea aangeanguka kifafa na kutokwa povu mdomoni je hapo ungesema kadhalilika??

Usichanganye kati ya kudhalilika kwa kutokwa na haja (uchafu) hadharani kwa sababu ya kujitakia na hali hiyo itokee kwa bahati mbaya kutokana na ugonjwa ambao kila mtu anaweza kuupata.
Sijui unatetea nini? Mbona nyeusi unataka kuilazimisha iwe nyeupe? Hapo kadhalilika na ni aibu kwa taifa zima
 
Uzee una shida nyingi muda mwingine, mi naomba nipumzishwe mapema 😅😅, tulienda kwenye msiba mmoja tukawa tumekaa chumbani watu kibao, tukatolewa wote kuna bibi alikuwa anabadilishwa diapers nikawaza cjui anajisikiaje maskini maana sio kama hajitambui ni mtu ana akili timamu anaogea watu wanacheka lkn ndo hivyo nguvu zimeisha 🥴
 
Katika tukio lisilo la kawaida, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mwenye miaka 71 ameonekana akitokwa na haja ndogo wakati wa hafla ya Kitaifa na wimbo wa Taifa ukipigwa. Kitendo hicho kinaibua maswali kuhusu hali za kiafya za viongozi wengi duniani kuendelea kukaa madarakani hata baada ya umri wao kuwa mkubwa na wengine wakiwa na afya zisizoridhisha.

Mwaka huu 2022, pia mgombea wa Urais nchini Nigeria Bola Ahmed Adekunle Tinubu mwenye miaka 70 alionekana akiwa na mfuko maalumu wa kuhifadhia mkojo wakati wa mchakato wa kuanza kampeni hali iliyopelekea wananchi kuhoji kuhusu afya yake na majukumu anayotaka kugombea.

Awe anavaa diaper!
 
Bado ile haja nyingine, wasaidizi wake watampeleka mtoni akajioshee huko[emoji16] badala yakutulia na wajukuu nyumbani kutwa kwenye majukwaa.
 
Last week nilisoma mahali Putin nae Hali yake kiafya sio nzuri sina uhakika sana. Alidondoka bahati mbaya haja kubwa ikamtoka ana kansa inamsumbua!
Ila Hawa viongozi wetu sijui wanatafuta nini ushajichokea pesa unayo ya kushato nini kingine wataka!!
 
Mpiga video mshenzi sana akaonesha tukio kwa umakini kwa nini hakutoa kamera? Ili auze? Kama angekuwa baba yake angefanya vile?
 
Ki protocal hata hii footage haikutakiwa itoke lkn kwakua ma beberu yanapenda kutudhalilisha ndio mana imetoka na kuzagaa ndio mana kwetu ilkua footage zote znahaririwa na mawasiliano ikulu ndio media zngne znapata content
Wazungu ndo watakuwa walitoa clip hiyo
 
Huyo ana afadhali maana kutozuia mkojo kunaweza kusiathiri akili na ufanyaji wa maamuzi. Kuna huyu Bola Asiwaji Tinubu (BAT) mgombea wa chama tawala cha APC pale Nigeria...
Mwamba kajipunguzia miaka kumi 😅😆😆🤣
 
Hata Biden huwa anapotea sana Jengo Jeupe
Na kuna wakati alimkanyaga paka akasema aah paka mwenyewe mweusi

Hawa wazee wafukuzwe tu
Oh maskini kwani ana shida ya macho ndo maana hakumuona huyo paka?
 
Haja ndogo imemtoka Raisi wa Sudani kusini, Salva Kiir (71), akiwa mbele ya viongozi mbalimbali kwenye mkutano wa kimataifa. Wadau wengi wamedai kuwa ifike wakati viongozi wa Afrika wakubali kuachia madaraka pale umri unapowatupa mikono.


 
Kwa wanaojua presidential directives za mamlaka kama hapa Tz, ni Nini kinapaswa kifanyike hapo baada ya AIBU hio?

Atabadirishwa Nguo na kuendelea ama zoezi lilokua linaendelea litakomea hapo? Kivyovyote vile hawezi kuachwa hivyo.
Nimeona kwenye misafara ya Viongozi wetu wakuu, hata wakiwa vijijini sehemu ambayo atahutubia kwenye jukwaa wanaandaa choo temporary
 
Back
Top Bottom