- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwa na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Instagram, ikiambatanishwa na madai kwamba leo nchini Zambia, siku ya uchaguzi mkuu, polisi wametumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya wapiga kura katika vituo kadhaa vya kupigia kura kwa tuhuma za uvunjifu wa amani.
Hata hivyo, ufuatiliaji wa video hiyo umebaini kuwa matukio yanayoonekana katika video hayakutokea wakati wa uchaguzi mkuu wa sasa nchini Zambia. Badala yake, video hiyo inaonesha tukio lililotokea kabla ya uchaguzi na sasa limehusishwa kimakosa na matukio ya uchaguzi wa sasa.
Uchunguzi zaidi kupitia vyombo rasmi vya habari nchini Zambia umebaini kuwa chombo cha habari cha Mwebantu kilichapisha video hiyo mwezi Agosti ikiwa na maelezo kwamba wafuasi wa chaam cha National Reconciliation Party for Unity and Prosperity (NRPUP) na United Party for National Development (UPND) walikabiliana katika Mkoa wa Western wakati wa ziara ya kampeni ya mgombea urais wa NRPUP, Brian Mundubile. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wafuasi wa vyama hivyo walirushiana mawe wakati wa mkutano wa kampeni.
Taarifa hiyo inathibitisha kwamba video inayosambazwa sasa ni ya zamani na imechukuliwa kutoka katika tukio lililotokea kabla ya uchaguzi, kisha kutumika kuwasilisha picha kwamba tukio hilo limetokea wakati wa uchaguzi wa sasa nchini Zambia.
Ikumbukwe kuwa Zambia inafanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali, wakiwemo Rais, wabunge na madiwani. Uchaguzi huo umekumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo matukio ya vurugu yaliyoripotiwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha kusitishwa kwa muda kwa zoezi la kuhesabu kura.
Hata hivyo, video hiyo inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii haihusiani na matukio hayo ya sasa, bali ni video ya tukio la awali lililotokea wakati wa kampeni za uchaguzi.