Vifaa vya Tronic vinaharibika vyenyewe baada ya muda mfupi. Ni dhahiri baada ya kuaminiwa wameanza kuchakachua

Vifaa vya Tronic vinaharibika vyenyewe baada ya muda mfupi. Ni dhahiri baada ya kuaminiwa wameanza kuchakachua

w0rM

Member
Joined
May 3, 2011
Posts
81
Reaction score
192
Salam Wanajamvi,

Nisiwapotezee muda niende moja kwa moja tu kwenye mada. Yaani nimenunua vifaa vya umeme na kuweka kwenye nyumba zikiwemo sockets, taa na nyaya. Ila ikiwa ni miezi 9 tu tangu kuweka vifaa hivyo yaani baadhi vimeanza kuharibika vyenyewe.

Taa zinaungua sana choke lakini kubwa zaidi, socket zinapasuka zenyewe yaani nishangaa tu tayari zimepasuka na inabidi kubadili. Nimeshabadili sockets 3 na sasa tayari nyingine 3 zimekuwa na nyufa.

3.jpg
2.jpg

1.jpg

Sijajua shida ni nini kwenye hivi vifaa ya Tronic. Je, hali hii ni kwangu tu au vifaa vyao vimeanza kuwa vya ovyo baada ya kujua wameshaliteka soko la Tanzania na watu wanawaamini?
 
Mkuu kwenye hili ni ukweli kabisa bidhaa za tronic ubora umeshuka sana, Taa za tronic kama nlio attach hapo chini zinaungua haraka sana
LE4022-DL_740x.jpg
 
Umejichakachua mwenyewe alafu unalaumu vifaa.Ata hivyo hakuna kifaa duniani ambacho hakiharibiki kabisa.
Unajichanganya kwa namna gani ikiwa unanunua kwa duka lao kabisa na wao wakisifia ni original?

Wao ndio wanaofanya mchezo basi wa kuweka vifaa feki na kudai ni original ili kupata faida maradufu
 
Hizo ni feki umeuziwa
Mkuu hizo zimenunulia kwenye moja ya duka lao kubwa kabisa. Kama ni mwenyeji wa Dar es Salaam basi utakuwa unalifahamu lile duka lao la Kisutu pale
 
Weka Hippo acha kujidanganya mkuu tutawapiga Sana Bei had mkome
 
Salam Wanajamvi,

Nisiwapotezee muda niende moja kwa moja tu kwenye mada. Yaani nimenunua vifaa vya umeme na kuweka kwenye nyumba zikiwemo sockets, taa na nyaya. Ila ikiwa ni miezi 9 tu tangu kuweka vifaa hivyo yaani baadhi vimeanza kuharibika vyenyewe.

Taa zinaungua sana choke lakini kubwa zaidi, socket zinapasuka zenyewe yaani nishangaa tu tayari zimepasuka na inabidi kubadili. Nimeshabadili sockets 3 na sasa tayari nyingine 3 zimekuwa na nyufa.

View attachment 2762131 View attachment 2762132
View attachment 2762133

Sijajua shida ni nini kwenye hivi vifaa ya Tronic. Je, hali hii ni kwangu tu au vifaa vyao vimeanza kuwa vya ovyo baada ya kujua wameshaliteka soko la Tanzania na watu wanawaamini?
Hata kwa muonekano tu hizo SIYO Tronic. Umepigwa
 
Watu mnaosema hizo sio tronic mnatumia kigezo gani ?
 
Back
Top Bottom