Mkuu umeongea vyema lkn nchi hii ina lack mipango ndio tatizo mama kwa kweli.
Kuna maeneo au mikoa ilitakiwa kusiwepo makazi kabisa maana kuna support kilimo almost mkoa mzima au wilaya nzima.
Yaani sisi kama nchi tuna Dhani maisha yatakuwa hivi milele wakati mabadiliko ni mengi sana.
Kizazi kijacho kitatumia ngivu nyingi sana kuweka mambo sawa.
Kwa kiasi kikubwa nchi hai lack mipango. Tuna mipango mingi tu.
Nchi ina lack utekelezaji wa mipango.
Miaka ya 1980s wakati tulishaanza kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma, Wa Nigeria walikuja kupata idea kama yetu. Walitaka kuhamisha mji mkuu kutoka Lagos kwenda Abuja.
Wakaja kujifunza kwetu, wakachukua makabrasha kuyafanyia kazi.
Wakaenda kuhamisha mji mkuu wao kutoka Lagos kwenda Abuja. Wakamaliza.
Sisi tuliowapa mipango tukawa bado hatujamaliza zoezi kwa miaka mingi, mpaka leo mabalozi karibu wote bado wako Dar. Wanaona hatujawa serious kwenye hili.
Tumepanga mipango miingi, utekelezaji mdogo sana.
Kuna jamaa mmoja alikuwa mwanaharakati wa elimu, jamaa alikuwa well connected kitaa anakijua, halafu kasoma mpaka Harvard mambo ya kimataifa yuko vizuri. Basi alikuwa anafanya activism sana mambo ya elimu.
JK akamuona. Akasema wewe nakitaka uje juwa mshauri wangu mambo ya elimu. Jamaa akasema naam, hapa sasa nimepata sikio la rais, mambo yataenda vizuri, tutabadili mengi.
Basi jamaa kila akimshauri JK, JK anamwambia hilo? Hilo tunalijua tangu miaka 10 nyuma, mtafute Katibu Mkuu wizara ya elimu atakupa makabrasha yote. Jamaa akimshauri JK kitu kingine, anaambiwa, hilo? Hilo tulishafanya utafiti Mzumbe, mtafute Mkuu wa Chuo atakupa makabrasha yote.
Yani jamaa alifikiri yeye anajua mambo mengi, serikali haijui tu, na akipata nafasi ya kushauti serikali, watabadili mengi.
Akaja kugundua kuwa, mambo mengi aliyotaka kushauri, serikali ilikuwa inayajua, tena zaidi ya alivyoyajua yeye.
Tatizo halikuwa kujua, tatizo lilikuwa utekelezaji.
Jamaa alijiuliza, sasa hapa nafanya nini? Ikabidi aache ile kazi, kwa sababu hakuna alichokuwa anafanya.
Makabrasha kibao yanapata vumbi, studies kibao watu wanefanya na kushauri.
Tatizo ni kwenye utekelezaji huko.