Vifo Katesh; Je, Tanzania kuna milima mingine kama mlima Hanang?. Serikali imechukua hadhari gani?

Yeah. Kulingana na kitabu cha Ufunuo, milima yote ina 'uwezo wa kuwaangukia na kuwafunika binadamu'.


 
Hujajibu swali, je, waendelee kujenga na kuishi hapohapo na vilevile pamoja na wenzao wenye mazingira kama haya? haitatokea tena, itatokea baada ya muda gani tena?
 
Kwa kuongezea,

Ili nchi iendelee inahitaji vitu vifuatavyo; WATU, ARDHI, SIASA SAFI, NA UONGOZI BORA. Kwa sasa Tanzania imebaki vitu viwili tu...
Kuna visiwa vya kwenye bahari ya Pacific vinaelekea kuzama chini ya bahari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na usawa wa bahari kupanda.

Kwa hiyo, vinapanga kuendelea kama nchi mtandaoni tu baada ya kuzama baharini.

Usije kushangaa visiwa hivi vikapata maendeleo kama nchi za mtandaoni, bila ya kuwa na ardhi, wakati sisi tuna ardhi lakini hatuna maendeleo.
 
Sio kweli, unampotosha mwenzako, watu wengi ndio uchumi wenyewe. Hakuna nchi ambayo haipendi masoko ya China na India kwa bidhaa zao kutokana na idadi yao kubwa ya watu (consumers). Nchi za magharibi zina uchumi mkubwa kwasabu ya dhambi inazozifanyia nchi nyingine kwenye masoko (WTO) lakini na uporaji kutoka nchi nyingine. Kwanini viwanda vingi vya Marekani viko Asia?
 
Hujajibu swali, je, waendelee kujenga na kuishi hapohapo na vilevile pamoja na wenzao wenye mazingira kama haya? haitatokea tena, itatokea baada ya muda gani tena?
Hapo waendelee kujenga tu kwa sababu baada ya maporomoko hayo ardhi haitakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji tena. Sehemu ya ardhi iliyobaki itachuruzisha maji na kubaki kiasi cha kawaida na hivyo haitatokea tena.
 
Sawa.

Endeleeni kuzaana bila mpango halafu muone kama kuzaana ndiyo utatuzi wa matatizo yenu.

Hawa watu ulionao unapata shida kuwalisha, kuwasomesha, etc.

Huna mipango mizuri ya kutumia nguvukazi. Watu hawa wachache hujui kuwatumia.

Halafu unasema, hapa tatizo langu ni watu wachache, ngoja niongeze watu wawe wengi.

Sasa kama hawa wachache hujui kuwatumia, hao wengi utawezaje kuwatumia?

Kwenye habari za mataifa ya magharibi na chumi zao, nimetoa mfano wa Japan. Japan si nchi ya magharibi.

Tujikite Africa kuondoa habari za magharibi.

Nchi zenye chumi tajiri kabisa kwa per capita income ni pamoja na Seychelles na Mauritius. Hizi nchi zina watu wachache lakini GDP per capita kubwa.

Ingekuwa wingi wa watu ndio unaoketa maendeleo, Nigeria ingezipita Mauritius na Seychelles kwa GDP per capita.

Tuangalie mifano kwa data.

Kwa hesabu za mwaka 2021:

Nigeria ina takriban watu milioni 215 na GDP per capita ya US $2066.

Seychelles ina watu 99,258 na GDP per capita ya US $14,653.

Kipato cha mtu mmoja wa Seychelles, kwa wastani, kwa hesabu za mwaka 2022, kilikuwa takriban mara saba ya kipato cha wastani cha mtu wa Nigeria kwa mwaka huo huo, licha ya Nigeria kuwa na watu mara 2166 zaidi ya Seychelles.

Sasa, mnaosisitiza kuwa wingi wa watu ndio uchumi bora, hamuoni kuwa Nigeria kuna watu wengi sana wanaogawana umasikini, wakati Seychelles kuna watu wachache wana uchumi mzuri tu, mara saba ya uchumi wa Nigeria kwa GDP per capita?
 
Hata maeneo yanayofaa kilimo na ufugaji wanakwenda kupima viwanja vya makazi kana kwamba watu hawahitaji chakula wala nyama na maziwa tena na ardhi sehemu nyingine hakuna. Watu wanakwenda kujenga kwenye njia za maji bila kuwa na mipango ya kuzuia mvua kubwa zisinyeshe. Mipango mibovu.
 
Sidhani kama unajua Hanang' wewe acha lawama zisizo na msingi...Hakuna kitu kama hicho
 
Kuna mlima unaitwa Mkindu au Mguluwandege. Mwaka jana mwezi wa nne kuliporomoka majabali usiku fulani. Majabali hayo hayakufika chini na wananchi pale wanafahamu. Mlima upo Morogoro eneo la Mkindu.

Watu wanaendelea kujenga kuufuata mlima huo. Na umekaa kimtego haswaa
 
Tamaa za fedha na ujinga wa kutoiona kesho vinasababisha maafa siku za usoni
 
Kwa mujibu wa Samico Tanzania Mlima Hanang' una kitambi.

Sasa unashauri watu wa Moshi wahame?
Watu wanajisemesha tu bila kujali context. Kwa land scape ya Tanzania ni sehemu gani ambapo Kuna makazi hakuna milima, vijilima au milima mikubwa? Hizi natural disaster ni sehemu ya maisha yanapotokea tukubali kwamba it's because of nature. Katesh ni mji wa zamani sana na haijawahi tokea kitu kama hicho na watu wa Ile jamii wanajua kutunza mazingira Yao sana sana. Palipotokea tukio kulikuwa well conserved Kuna miti na uoto wa asili na nyumba zilijengwa strategically kufuata landscape...Tuache lawamazisizo na msingi
 
Mimi nimefanya utafiti mwingi sana kwenye maswala mbalimbali nchini, lakini nakwambia shida kubwa ya nchi yetu hii ni siasa za chama kushika hatamu na kiendelee kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile. Kila maamuzi mtaalamu atayoishauri serikali lazima yahakikishe kuwa hayaigombanishi CCM na wapiga kura. Huu ndio mtaji mkuu wa CCM kuendelea kubaki madarakani. Ndio maana leo hii huwezi kupanga wala kusafisha miji, huwezi kuwaondoa watu mabondeni au chini ya milima hatarishi.

Wazo la kuhamishia makao yetu makuu kwenda Dodoma lilikuwa na maana na manufaa kwenye miaka ya 1970s, lakini liliendelea kupoteza maana baada ya maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano. leo hii njia za kupashana habari na kupata taarifa hazihitaji kwenda Dodoma tena kutoka Dar au Mtwara, gharama za kuhamia dodoma kwenye miaka hii 2020s zingeweza kuepukika kama tungejikita zaidi kwenye kukuza njia za habari na mawasiliano ili kila mtanzania apate huduma zote za wizara husika kwenye ngazi ya makao makuu ya wilaya yake. Unanda Dodoma kufanya nini?
 
Ukishaishi kwa kuamini kudra za Mwenyezi Mungu utajenga popote pale.

After all, unaweza kuacha kujenga milimani ukajenga sehemu tambarare, lakini kwa kudra tu ukapigwa radi vilevile.

Hii mentality ya kuishi kwa kudra ndiyo inatugharimu.
 
Hapo waendelee kujenga tu kwa sababu baada ya maporomoko hayo ardhi haitakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji tena. Sehemu ya ardhi iliyobaki itachuruzisha maji na kubaki kiasi cha kawaida na hivyo haitatokea tena.
Hiyo theory yako ni theory kama ya embe, kwamba ukila sehemu ya juu ndani utaakutana na kokwa. hakuna kitu kama hiko, leo utakutana na land slide kesho utakutana na lava ya moto kama ya nyiragongo, kesho utafunikwa na jivu na kesho kutakumbana na moshi mbaya tu. Huwezi kutoa majibu mepesi ya kiasi hicho mkuu. Nyumba moja baada ya kujengwa ukatokea mpasuko kwenye ukuta na msingi, mwenye nyumba akasema msiogope wapangaji hapo ndio mwisho wa mpasuko kwakuwa ardhi ilikuwa inajiweka sawa tu, imeshamaliza. Lakini ile nyumba ikawa ya kwanza kuanguka siku lilipotokea tetemeko dogo tu lililozibakisha nyumba nyingine.
 
Kule kwetu tulizaliwa wengi, watoto 20 kwa wanawake 3 wa baba, lakini wote tulikwenda shule kwakuwa watoto wote tulikuwa na kazi za kufanya kule shambani, kwenye mifugo, kwenye mizinga ya baba na dukani. Tulikuwa tunalima sana, kuchunga sana, kukamua sana, kulisha kuku sana, kulinda tumbili sana, kurina asali sana na kulisha kuku sana kiasi kwamba hatukuwa na shida ya chakula wala ada ya shule na chuo. Bro, ni sera tu mbovu.
 
Ulisha wahi lini kuona Tz tuko vizuri kwenye disaster preparedness and mitigation? Never ever! Sina maana mbaya.
 
Ukishaishi kwa kuamini kudra za Mwenyezi Mungu utajenga popote pale.

After all, unaweza kuacha kujenga milimani ukajenga sehemu tambarare, lakini kwa kudra tu ukapigwa radi vilevile.

Hii mentality ya kuishi kwa kudra ndiyo inatugharimu.
Umecompare na kuContas😅
 
Hiyo argument yako siyo ya kisayansi! Kuna uhusiano gani wa kisayansi kati ya landslide ya Hanang na lava ya moto au jivu na moshi mbaya? Kuna vitu umesimuliwa lakini huvielewi unaishia kujichanganya! Mlima Hanang ni wa volcano na kwa sasa imesinzia (extinct) kwa hiyo haihusiki na landslide iliyotokea.

Kilichosababisha landslide hapo Hanang ni aina ya mwamba au udongo uliopo ambao una uwezo wa kuhifadhi maji, mwinuko wa mlima na mvua za muda mrefu na nguvu ya gravity ambayo ndiyo hasa imesukuma hiyo miamba ikabomoka.
 
Jidanganye tu aisei, hali ya hewa ya sasa na zamani ni tofauti sana, mazingira yamechafuliwa sana, huwezi kuongea kauli jumuishi kama hizo za kutoa false hope. Leo hii watu wa katesh wakiona wingu zito sana limetanda na kusikia mngurumo upande ulioko mlima hanang wanakurupuka kutoka kwenye nyumba zao. Unadhani kuna mtu anatamani kujenga upya nyumba palepale ilipozolewa ile ya kwanza?
 
Pia kwa kasi yetu ya kuzaana, wakati nchi haiongezeki, huko mbele watu watazidi kubanana tu.

Hivyo tunahitaji kupangilia vizuri sana both land use na family planning.

Enzi za kuzaana zaana ovyo tu na kuishi kwa kujua nchi kubwa tu hii zinaisha.
Tz kuja kufikia kubanana hy bado sana, hata tukiwa 150M bado ardhi ipo kubwa sana tuu labla useme kubanana kwenye majiji na sio Tz nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…