kwahiyo tuishi kwa kudra?Ukishaishi kwa kuamini kudra za Mwenyezi Mungu utajenga popote pale.
After all, unaweza kuacha kujenga milimani ukajenga sehemu tambarare, lakini kwa kudra tu ukapigwa radi vilevile.
Hii mentality ya kuishi kwa kudra ndiyo inatugharimu.
Sasa, wingi au uchache wa watu hauwezi kujadiliwa nje ya muktadha wa sera za uchumi, teknolojia na mipango ya nchi.Kule kwetu tulizaliwa wengi, watoto 20 kwa wanawake 3 wa baba, lakini wote tulikwenda shule kwakuwa watoto wote tulikuwa na kazi za kufanya kule shambani, kwenye mifugo, kwenye mizinga ya baba na dukani. Tulikuwa tunalima sana, kuchunga sana, kukamua sana, kulisha kuku sana, kulinda tumbili sana, kurina asali sana na kulisha kuku sana kiasi kwamba hatukuwa na shida ya chakula wala ada ya shule na chuo. Bro, ni sera tu mbovu.
Muishi kwa kudra mara ngapi tena?kwahiyo tuishi kwa kudra?
Overpopulation si kubanana ardhi tu.Tz kuja kufikia kubanana hy bado sana, hata tukiwa 150M bado ardhi ipo kubwa sana tuu labla useme kubanana kwenye majiji na sio Tz nzima
Asante kwa video mkuu.
Inabidi kukubaliana nawe; maana tumeona jinsi mkasa huu ulivyotumika na wahusika kuutumia kuwa mtaji.majanga haya ni mitaji
Usichanganye volcano na landslide (Maporomoko ya ardhi). Mlima Hanang umekumbwa na landslide na Oldonyo Lengai ni volcano!OLDONYO LENGAI ni hatari zaidi kwasababu ni hai na kuna wakati huwa inatoa moshi mweusii
Halafu kuna jibu hapa:Nitakuwa kinyume na wewe.Mimi naona nchi zenye idadi kubwa ya watu ndiyo zenye maendeleo (kiuchumi) makubwa hapa duniani.
Maendeleo hayaji kwa idadi kubwa ya watu, maendeleo yanakuja kutokana na kujua kutumia watu na kupanga uchumi vizuri kulingana na idadi ya watu.
Very true.Hata maeneo yaliyoachwa wazi ili kuhifadhi watu wakati wa majanga yote sasa hivi ni mali ya chama, ni maegesho ya magari au ni baa au yameuzwa.
Ni huo pekee . Hakuna mwingine.Sasa milima kama ya Hanang iko mingapi ili walioko kwenye milima hiyo wasisubiri kujifunza kwa makosa yao wenyewe? watumie darasa hili hili la katesh.
Status ya visiwa vya bahari ya Hindi ikoje, hasa visiwa vyetu pendwaKuna visiwa vya kwenye bahari ya Pacific vinaelekea kuzama chini ya bahari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na usawa wa bahari kupanda.
Kwa hiyo, vinapanga kuendelea kama nchi mtandaoni tu baada ya kuzama baharini.
Usije kushangaa visiwa hivi vikapata maendeleo kama nchi za mtandaoni, bila ya kuwa na radhi, wakati sisi tuna ardhi lakini hatuna maendeleo.
Kusombwa kwa nyumba nyingi ni ushahidi mwingine wa uholela kwenye sekta ya ujenzi na makazi nchini. Hazikuwa nyumba bali matope TU (matembe). Ndio maana watu wanashangaa kuona nyumba za ibada kanisa na msikiti zimebakizwa bila kusombwa. Ukweli sio miujiza kubaki bali zilikuwa imara, zimejengwa vizuri kuliko nyumba zilizozolewa. Uholela huu kwenye wizara ya ujenzi unasababisha vifo vingi sana na hasara kwa wananchi na serikali pia. Waziri wa ujenzi ajiuzulu.Asante kwa video mkuu.
Inasikitisha sana.
Pole nyingi kwa wote waliopatwa na janga hili.
Nyumba zao zilikuwa duni sana ndio maana zilisombwa kirahisi, ni matope yaliyokutana na matope mengine kutoka mlimani. Sekta ya ujenzi Ina matatizo pia, watu wanajijengea nyumba kiholela kujenga msingi, kutana na mapaa hafifu mno.Inabidi kukubaliana nawe; maana tumeona jinsi mkasa huu ulivyotumika na wahusika kuutumia kuwa mtaji.
Lakini kinacho sikitisha ni kwa hao waliopatwa na mkasa kutotambua kwamba wanatumika kama mtaji.
Mwenye akili timamu ni yule anaejiuliza mwenyewe maswali kuhusu "ni kwanini tuko hivi na kwa nini tumebaki hivi tulivyo kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuzazi,.......?". Ataendelea kujiuliza mwenyewe "Ni kwanini Afrika yote inafanana fanana kimaendeleo na mambo Yao mengine yote?" Ataendelea kujiuliza "ni kwanini hata nchi zilizobadilisha vyama vyao tawala kama vile Zambia, Malawi, Kenya, Liberia, DR Congo, Uganda, nk hata wao bado hali Yao kiuchumi Iko vilevile TU?"Halafu kuna jibu hapa:
Sasa sijui kama kuna elimu ya kutosha iliyobadishwana hapa kufikia mwafaka.
Mmoja ni "BabuMkubwa", ambaye nachukulia kuwa ni mtu wa makamo ya kutosha na kuwa na upeo stahiki kutokana na uzoefu wa maisha, na uzoefu wa kimazingira kumwezesha kuwa na ufahamu wa uhusiano kati ya wingi wa watu na uwepo wa maendeleo miongoni mwa watu hao.
Sitamzungumzia wa pili, kwa sababu anajulikana vizuri miongoni mwa washiriki katika jukwaa hili.
Nimevutiwa na mabadilishano ya mawazo kati ya hawa wawili, kwa sababu moja tu; kwamba pamoja na kuwa nchi huru miaka zaidi ya 60, na kuwa na mamlaka yetu wenyewe juu ya elimu ya watu wetu; bado inaonekana kuwepo upungufu mkubwa sana katika jamii yetu, kuweza kutambua maswala ambayo ni rahisi kabisa kuhusu hali yetu duni kimaendeleo.
Kuna nyakati tunajifikiria tumepiga hatua mbele zaidi kimaendeleo kuliko wakati mwingie wowote tokea uhuru. Lakini unapokutana na maswala ya aina hii, na kujua kuwa ndani ya jamii bado kuna upungufu mkubwa wa uelewa juu ya maswala ya msingi kabisa kama hili; halafu unakumbana tena na wengine wakijitangaza kuwa "chawa" juu ya viongozi wetu wanaoshindwa kutufumbua macho kielimu, inabidi kujiuliza maswali mengi kama kweli safari yetu ya maendeleo inakwenda mbele au inarudi kinyumenyume.
Ni mawazo tu, yaliyo niijia akilini baada ya kusoma mabadilishano kati ya hawa wawili.
Mkuu,Mwenye akili timamu ni yule anaejiuliza mwenyewe maswali kuhusu "ni kwanini tuko hivi na kwa nini tumebaki hivi tulivyo kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuzazi,.......?". Ataendelea kujiuliza mwenyewe "Ni kwanini Afrika yote inafanana fanana kimaendeleo na mambo Yao mengine yote?" Ataendelea kujiuliza "ni kwanini hata nchi zilizobadilisha vyama vyao tawala kama vile Zambia, Malawi, Kenya, Liberia, DR Congo, Uganda, nk hata wao bado hali Yao kiuchumi Iko vilevile TU?"
Ukishapata majibu ya maswali hayo ndiyo uje na majibu ya mjadala kati ya uhusiano kati ya idadi ya watu na maendeleo.
Maendeleo hayaji kwa idadi kubwa ya watu, maendeleo yanakuja kutokana na kujua kutumia watu na kupanga uchumi vizuri kulingana na idadi ya watu.
Unaweza kuwa na watu wengi, lakini hujajipanga, unaongeza njaa tu.
Ingekuwa maendeleo yanatokana na wingi wa watu, India ingekuwa imeendelea kuliko Marekani na Nigeria ingekuwa imeendelea kuliko Italy.