Kinachokusumbua ni ujinga tu.
Hivi unawezaje kuchukua tahadhari kwa ugonjwa unaoenea kwa njia ya hewa?Najua huwezi hata kufikiria,ila kama ungekuwa unafikiria,ungejiuliza maswali mengi na usingepata majibu yake kuhusu ugonjwa huu.
1. Vimelea vya ugonjwa vina uwezo wa kukaa hewani zaidi masaa manne.Hata watu wote wakivaa barakoa,unawezaje kuwazuia wasiteme mate,big G,makohozi ama kupenga makamasi?Ukikanyaga makohozi ukapanda kwenye gari yako,unapuliza dawa kwenye gari?Wanao hawagusi viatu ama carpet la gari?
2. Barakoa za vitenge hazikukingi kupata vimelea vya ugonjwa bali zinakudhibiti usieneze kirahisi kwa kutema mate n.k je kiuhalisia hicho kinafanyika?
3. Matumizi ya pesa taslimu,note na coins,unadhibiti viti visitumike kueneza ugonjwa?Je unadhani tuna uwezo hasa vijijini kutumia mitandao kufanya manunuzi?
4. Unadhani ni rahisi kuwakinga watumishi wote wa afya ambao wanakutana na mgonjwa kuanzia yule anayefungua faili hospitali hadi muhudumu wa mwisho anayekupa dawa ukatumie?Unajua bei ya barakoa moja N.95?Ilikuwa inauzwa sh.50,000 na unaivaa masaa manne tu!
Una utaratibu mzuri wa uthibiti wa taka zinazotokana na hivi vitu?
5. Unayafahamu maisha ya mtanzania wa kawaida au ndio nyie mliozaliwa mjini mnadhani nyanya zinalimwa kwenye friji?
6. Umewahi kufikiri kuhusu gharama za msingi pekee inazotumia serikali katika kutoa huduma za afya?
Unadhani tuna utajiri wa kukabiliana na huu ugonjwa?
7. Umewahi kujiuliza mortality rate ni kiasi gani kwa nchi kama Kenya na Uganda wanaochukua hatua kadhaa na kupima faida dhidi ya hasara ya kuifunga nchi?
Yako maswali mengi ila naamini tatizo ni kutaka kuiga wazungu kila kitu wakati mazingira yao ni tofauti sana na yetu.Jitahidi kufikiri vizuri utamuona JPM kama shujaa
Wewe wala si malaika. Wewe ni ibilisi mwenyewe. Haikufikirishi watu kufa. Uko kama una maslahi na kila kifo.
Kwanini nia yenu ni kupotosha tu kuwa kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huu ni kufungia watu ndani au kufunga mashule?
Kwanini ni nia yenu kupotosha kuwa serikali haziwajibiki kwa maisha ya watu kwenye dharura kama hizi. Serikali zisizowafaa wananchi wake wakati wa dhiki zitakuwa na umuhimu gani basi?
Mna maslahi gani na upotoshaji kama huu wakati maisha ya watu yanapotea kama hivi?