Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Nasindikiza na kapicha
Tunaipanda kilima nyege hapa

Ova
 
Ninashukuru sana , sikuwajua ndugu zake wengine kumbe walikua na brothers , nilimjua JUdy na Mapinduzi .
 
Ligate ndio yule jamaa yuko USA sijui promota wa mziki?
 
Wazee zamani walikuwa hawajitangazi,sasa siku hizi watu kutwa kutembea na vitambulisho vyao vinaninginia shingoni
Nlikuwaga na watoto wa mosha wale twins wa kiume,forodhani
Mzee wao alifarikigi basi msiba ulikuwa mkubwa kweli

Ova
 
Maliza kaka[emoji16]
 
Wiki iliyopita nimewaza sana hilo!! Nitakutafuta nikwambie nimetekeleza mkuu.
 
Hao watoto walikua wakali kinoma , Halima na mdogo wake Hamida, last time niliona kama Hamida kaolewa ni GA or FL , Lulu demu mmoja poa sana asiee, naona aliolewa na Mwarabu wa Qatar . wanaishi Qutar now
Dah, ndiyo hao hao Halima na Hamida.

Waarabu wamemchukua Lulu, halafu wanakuja kuchukua mpaka bandari [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Sijaona mnawazungumzia watoto wa Benjamin Mkapa au hawakuwa sehemu ya wana osterbay miaka hiyo?.
Watoto wa Mkapa hawakukaa Oysterbay, walikaa sana Canada, US, briefly Nigeria baba yao alivyokuwa balozi, halafu Upanga / Sea View.

Utotoni tulikuwa tunaenda kwenye birthday parties zao, walikuwa wanalalamika sana mshua wao alikuwa anawakataza kunywa maji kabla ya kumaliza chakula. Walikuwa hawapendi sana.

Kuna siku moja tulikuwa tumekaa maskani Upanga.

Mara tukaona polisi kama ishirini wanakuja wamebeba marungu na bunduki.

Basi mimi nikawaambia madogo maskani, kama hujiamini, ondoka kabisa, hapa tunakuja kupewa dhahama na hawa polisi.

Basi, polisi wakafika maskani.

Mmoja akasema "Aisee, mnafanya nini hapa?"

Jamaa mmoja akawajibu "Afande, kwani hivyo ndivyo mlivyofundishwa kusalimu watu?"

Polisi akanywea, akawa kama anashangaa, huyu dogo anajiamini vipi kuniuliza hivi?

Basi mkuu wao akaanza kutuuliza, mmoja mmoja, wewe unakaa wapi? Basi mtu anamuonesha pale, mwingine anaulizwa hivyo hivyo, anaonesha pale.

Wakamfikia mchizi mmoja, wakamuuliza, wewe unakaa wapi? Akajibu "Kwa Benjamin".

Sasa yule polisi akawa kashangaa, akauliza kwa Benjamin, Benjamin gani?

Jamaa akamwambia "Benjamin huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani kuna nani mwingine"?

Yule polisi akawa kama hajaamini, lakini kuna wenzake walikuwa wanamjua jamaa, wakamwambia ni kweli huyu huwa tunamuona kwa Mkapa tukienda kulinda.

Basi hapo hapo tukaona polisi wanabadilika kabisa. Yule kiongozi wao akasema "Aah, unajua wazee tunatambuana tu, hakuna tatizo, tunafahamiana tu".

Baadaye nasikia kile kijiwe walikipigia X kwenye ramani yao kituoni, wakimaanisha msiguse kijiwe hiki wanakaa watoto wa Mkapa hapa.

Nilifikiria sana kama kijiwe kingekuwa cha hohehahe wangetupa msala gani siku ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…