Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Aisee umenikumbusha sana , kipindi hicho nilikua hata sijui wazee wana fanya kazi gani hapa ndio nina shangaa kumbe waze walikua na nafasi hizo , hata Mzee wangu ilikua late sana kuja kujua ana fanya kazi gani , sijui kwanini nilikua sina time ya kujua hilo.
KIna Saraita demu pekee alikua ana drive magari ya maana. Hapo jirani na kwa Sapi kulikua na mshkaji wangu moja nime msahau jina , alikua mshkaji wangu sana , halafu kwao kulikua na Tausi wengi sana ( Eneo hilo pia Tausi ako sana sijui sababu ya Ikulu ya pale Mwinyi na kwa Sapi ) , yule jamaa nasikia walihama hapo kuhamia mkoa , kitu kama hiccho , una weza mtambua aliitwa nani ?
Lete hiyo story ya demu wa Ki Indonesia , hatuta sema , tuta tunza siri .lol
Nasindikiza na kapicha
Tunaipanda kilima nyege hapa

Ova
20230703_114537.jpg
 
Ndugu zake ambao nawafahamu ambao wapo hai hadi Leo, ni huyo sister yao Juddy, Rose, Vicky na kaka zao wengine sijajui vizuri

Mama yao ndio anakaa hapo Mwenge hata juzi Jumamosi nilipita kuwasalimia

Halafu Mapinduzi alifariki kama utani, alitoka tu kwenye sherehe jioni akarudi nyumbani bahati mbaya mke wake ambaye ni Shangazi yangu alikuwa hayupo, so nyumbani alikuwa Dada wa kazi tu

Sasa alivyorudi home baada ya muda kidogo akaanza kukohoa Damu, hali ilivyozidi kuwa mbaya Dada wa kazi akachukua simu na kuwapigia ndugu zake, kaka zake wakafika na kumuwahisha hospitalini, Kwa bahati mbaya mgonjwa akakata moto njiani[emoji22]

Kifo chake nae kilikuwa Cha kutatanisha sijui hata alikula nini, maana ilikuwa ghafla Yani katoka kuongea na mkewe muda sio mrefu Dakika tano nyingi tunaambiwa mtu kafariki
Ninashukuru sana , sikuwajua ndugu zake wengine kumbe walikua na brothers , nilimjua JUdy na Mapinduzi .
 
Waliokaa pembeni ya Oysterbay Primary ni akina Bakirane, sio bakilana. Akina Bakilana walikaa kule karibu na lilipoanzia daraja la Tanzanite.

Kwa kina Bakirane walikua wanafuga Ng'ombe pale kwao na ile Isuzu KB double cabin tulienda nayo sana kuchukua majani shamba.

Enzi hizo huwezi ishi au pita pita mitaa ile usiwajie akina Kafipa, Apson, Kejo, Kitomari, Mtui, Cathless, Faraji, Kamuzora, Warioba, Mengi, Kihampa, Ngamilo, Ngalawa, Malecela, Bakilana, Bakirane, Ligate, Usungu, Mtui, Kotta, Mpembe, Maliti, Ntukamazina, Mahiga, na wengineo, akina Malocho na Mang'enya waliishi Chole road huko na Akina Typhon Maji. Majina ni mengi sana ngoja niachie hapo.
Ligate ndio yule jamaa yuko USA sijui promota wa mziki?
 
Aisee umenikumbusha sana , kipindi hicho nilikua hata sijui wazee wana fanya kazi gani hapa ndio nina shangaa kumbe waze walikua na nafasi hizo , hata Mzee wangu ilikua late sana kuja kujua ana fanya kazi gani , sijui kwanini nilikua sina time ya kujua hilo.
KIna Saraita demu pekee alikua ana drive magari ya maana. Hapo jirani na kwa Sapi kulikua na mshkaji wangu moja nime msahau jina , alikua mshkaji wangu sana , halafu kwao kulikua na Tausi wengi sana ( Eneo hilo pia Tausi ako sana sijui sababu ya Ikulu ya pale Mwinyi na kwa Sapi ) , yule jamaa nasikia walihama hapo kuhamia mkoa , kitu kama hiccho , una weza mtambua aliitwa nani ?
Lete hiyo story ya demu wa Ki Indonesia , hatuta sema , tuta tunza siri .lol
Wazee zamani walikuwa hawajitangazi,sasa siku hizi watu kutwa kutembea na vitambulisho vyao vinaninginia shingoni
Nlikuwaga na watoto wa mosha wale twins wa kiume,forodhani
Mzee wao alifarikigi basi msiba ulikuwa mkubwa kweli

Ova
 
Hatari.

Let me remember all the girls. The streets, the homies, the stories. From my times.

Kuna dada mmoja alikuwa anakaa karibu na lighthouse kule Toure Drive, kwa Jaji Nyalali, alisumbua sana.

Tulikuwa tunakwenda karibu na club ya Wamarekani walikuwa wanakwenda sana kuangalia movies.

Kuna siku nyumba yao ilipigwa na radi, I wonder if it was because of the lighthouse.

I think it was Lulu.

Nilikuwa naenda na mshua nilikuwa mdogo sana. Mshua alikuwa anakaa na Judge Bomani, Judge Nyalali na washua wengine wanakata issues ambazo mimi hata sizielewi wakati huo.

Halafu kulikuwa na Mary Mosha hapa karibu na ubalozi wa Marekani wa Laibon. Alikuwa anasoma Forodhani. Baba yake alikuwa DG wa TANESCO, Mzee Mosha akaamua kuhama pale kwa sababu alisema ubalozi wa Marekani ulikuwa unawaangalia mpaka ndani.

Halafu kulikuwa na the Abebe sisters, Salaita na yule mwingine mdogo wake nafikiri yupo Las Vegas siku hizi. Anaitwa Maisara.

Halafu down the road Laibon kulikuwa na Arthur Lema na mdogo wake Brenda, baba yao likuwa DG breweries. Brenda was hot, but she was like a little sister to me.

Baba yao alivyotoka Breweries alienda kufanya kazi Nairobi for six month akarudi na a flashy red car. Akaenda kuwa DG wa Tanganyika Packers.

Arthur alipelekwa shule Ireland akanywa school fees zote, baba yake akampeleka Los Angeles California. Akasoma akarudi Tanzania kuendeleza mashamba yao.

Ule mtaa wa Laibon kulikuwa kuna nyumba ya Mwinyi, basi siku nyingine tukitoka shule tunakaa kuna kijiwe kona ya Kaunda, tunauona msafara wa Mwinyi anarudi nyumbani, anatupungia mkono.Mwinyi was cool to the kids on the corner.

Siku nyingine Mzee Mwinyi anaalika jirani kwenda kucheza naye bao, kuna mzee mmoja alikuwa anakaa nyuma ya nyumba yake alikuwa CEO wa NBC, karibu na kwa Speaker Adam Sapi Mkwawa, mtoto wake alikuwa rafiki yangu, walikuwa wanaitwa sana kwa Mwinyi kula kashata na kunywa kahawa.

Kuna siku Salama Mwinyi alikuwa ananiringishia sarafu mpya ina picha ya baba yake, nikapiga kofi, a message kwamba I don't care that your father is the president. Akataka kwenda kunisemea, lakini rafiki yake akamwambia huyo Kiranga ni kichaa, ukimsemea ndiyo utazidisha ugomvi. That is how I got away with slapping the president's daughter in the face. I am not proud of that, especially since my philosophy of not hitting women now.

Siku moja nikaamua kuwachemsha tu ubalozi wa Marekani. Nilitaka tu kuingia ubalozi wa Marekani na kuwauliza maswali.

Nikaingia. Kufika getini, yule Marine akaniomba ID, nilikuwa na wallet ina picha ya paka. Akaiangalia, akasema huyu ni paka wako? Nikasema ndiyo. Akafurahi sana. Apparently he was a cat person. Huyo paka hata hakuwa paka wangu, it was a stock photo.

Nilikuwa na documebts za watu wa kampuni za Marekani wanataka watu kutoka nchi za nje waende kufanya kazi Marekani. Nikawa nawaluliza wale watu wa Ubalozi, hawa Wamarekani tutawajuaje kama ni watu genuine au matapeli? Yule Consular wa Ublozi wa Marekani hakuwa na jibu. Kwanza aliniangalia kama haamini nauliza swali lile, inaonekana alikuw ahajapata kuulizwa swali lile na hakuelewa kama nimetumwa na serikali au vipi. Akaniambia atanipa mtu wa kunisaidia. Yule mtu alinizungusha ule ubalozi wa Marekani Laibon mpaka nikajua huyu ananizungusha makusudi nisijue ramani ya jengo. Mwisho wakanifikisha kwa mtu aliyeniambia kwamba Ubalozi wa Marekani Tanzania ni mdogo sana na hauna labor attache, kwa maswali yangu walihitaji nipate majibu kutoka kwa labor attache wa ubalozi wa Marekani Nairobi Kenya, nikapata mambo mengine nikaacha kufuatilia.

Mtaa huo pia walikuwa wanakaa kina Said, Idi, na wakina Janguo wengine.

Idi alikuwa na shobo sana, lakini siku moja alinionesha a very human side of him. Deereva wetu alikuja kunichukua shule, Muhimbili Primary (nilianza Muhimbili kwa sababu ya kukaa Upanga) halafu darasani mwalimu alikuwa katuchelewesha kutoka, yule derava hakujua la kufanya, Idi akajipa jukumu la kuja darasani na kumwambia mwalimu kwamba kuna dereva ananisubiri ameshangaa hatujaachiwa kuondoka darasani, mwalimu akaturuhusu kutoka, kutoka siku hiyo Idi Janguo akawa rafiki yangu.

Mtaa huo wa Laibon nakumbuka kina Chambi Chachage, kina Humphrey Mbise, Salama Mwinyi alikuwa anakuja kwenye nyumba yao ya Laibon siku moja moja, lakini mara nyingi akikaa Ikulu.

Siku moja natoka shule nikakutana na Salim Ahmed Salim akitembea kufanya mazoezi, alikuwa na bodyguars wake wachache tu, akatupa hi kawaida tu..

Kuna binti mmoja wa Adel, I forgot her first name, alikuwa anasoma Jangwani, baba yake alikuwa Permanent Secretary kwenye one of the key ministries, nilikuwa naongea naye sana kwenye simu halafu hanijui mimi ni nani.

Kuna siku tumeenda Ubalozi wa Indonesia kwenye party, kule Coco Beach, nikatokea naongea na mtoto wa balozi anataka sana kujua Kiswahili, alikuwa anasema anataka sana kujifunza Kiswahili, kinafanana sana na lugha yao, kilichofuata hapo sitaki kuhadithia.

Those were the days.
Maliza kaka[emoji16]
 
Sasa mchizi wa JF nakupa idea nyingine, nunuwa ardhi uswahilini ambako bado Ardhi inauzwa kwa thamani ndogo jenga community swimming pool kubwa halafu ndani yake weka kapub kadogo na something like circus ya michezo ya Watoto, wekeza hii kitu kwenye community tofauti tofauti according to your research

Utapiga pesa mpaka basi, na hii ni permanent investment.

Bongo kuna tatizo la community kukosa maeneo yao ya kufurahia maisha zaidi ya watu kuwekeza bar tu kila corner.

Uzuri wa Bongo almost ni summer time mwaka mzima kwahiyo swimming pool ni biashara inayolipa sana.
Wiki iliyopita nimewaza sana hilo!! Nitakutafuta nikwambie nimetekeleza mkuu.
 
Hao watoto walikua wakali kinoma , Halima na mdogo wake Hamida, last time niliona kama Hamida kaolewa ni GA or FL , Lulu demu mmoja poa sana asiee, naona aliolewa na Mwarabu wa Qatar . wanaishi Qutar now
Dah, ndiyo hao hao Halima na Hamida.

Waarabu wamemchukua Lulu, halafu wanakuja kuchukua mpaka bandari [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Sijaona mnawazungumzia watoto wa Benjamin Mkapa au hawakuwa sehemu ya wana osterbay miaka hiyo?.
Watoto wa Mkapa hawakukaa Oysterbay, walikaa sana Canada, US, briefly Nigeria baba yao alivyokuwa balozi, halafu Upanga / Sea View.

Utotoni tulikuwa tunaenda kwenye birthday parties zao, walikuwa wanalalamika sana mshua wao alikuwa anawakataza kunywa maji kabla ya kumaliza chakula. Walikuwa hawapendi sana.

Kuna siku moja tulikuwa tumekaa maskani Upanga.

Mara tukaona polisi kama ishirini wanakuja wamebeba marungu na bunduki.

Basi mimi nikawaambia madogo maskani, kama hujiamini, ondoka kabisa, hapa tunakuja kupewa dhahama na hawa polisi.

Basi, polisi wakafika maskani.

Mmoja akasema "Aisee, mnafanya nini hapa?"

Jamaa mmoja akawajibu "Afande, kwani hivyo ndivyo mlivyofundishwa kusalimu watu?"

Polisi akanywea, akawa kama anashangaa, huyu dogo anajiamini vipi kuniuliza hivi?

Basi mkuu wao akaanza kutuuliza, mmoja mmoja, wewe unakaa wapi? Basi mtu anamuonesha pale, mwingine anaulizwa hivyo hivyo, anaonesha pale.

Wakamfikia mchizi mmoja, wakamuuliza, wewe unakaa wapi? Akajibu "Kwa Benjamin".

Sasa yule polisi akawa kashangaa, akauliza kwa Benjamin, Benjamin gani?

Jamaa akamwambia "Benjamin huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani kuna nani mwingine"?

Yule polisi akawa kama hajaamini, lakini kuna wenzake walikuwa wanamjua jamaa, wakamwambia ni kweli huyu huwa tunamuona kwa Mkapa tukienda kulinda.

Basi hapo hapo tukaona polisi wanabadilika kabisa. Yule kiongozi wao akasema "Aah, unajua wazee tunatambuana tu, hakuna tatizo, tunafahamiana tu".

Baadaye nasikia kile kijiwe walikipigia X kwenye ramani yao kituoni, wakimaanisha msiguse kijiwe hiki wanakaa watoto wa Mkapa hapa.

Nilifikiria sana kama kijiwe kingekuwa cha hohehahe wangetupa msala gani siku ile.
 
Back
Top Bottom