Vifo vya watoto mashuleni vinavyotokana na kufanya usafi kwenye ghala za kuhifadhia mahindi

totoadela

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
369
Reaction score
1,106
Habari ndugu zanguni,
Naomba tushauriane na tutoe ya moyoni kuhusu shule zinazowaingiza watoto kufanya usafi kwenye maghala ya kuhifadhi mahindi hizi ishu naona isipoziwa sauti itakuwa sugu kwa sasa. Jana nimeona watoto Watatu wa Form 3 wamefariki Dunia baada ya mwalimu kuwachukua watoto sita kwa ajili ya kufanya usafi hatimaye watoto watatu wamefariki Dunia 😭😭.

Inahuzunisha sana nikiwa kama mzazi kwa sababu hizo ghala ni hatari kwa maisha ya watoto wetu ambao wanaishi shule za kulala, mtoto ameondoka mzima wa afya kwenda shule kusoma unarudishiwa nyumbani mtoto amelala inaumiza mnoo..

Mwaka jana hii ishu ilitokea katika shule mbili tofauti na jana tarehe 2/5 nimeona imetokea tena.. Ndugu zanguni najua humu viongozi mbalimbali wapo ikiwemo mama yetu Gwajima Atusaidie kupaza sauti kwa walimu katika hizi shule za Sekondari watoto wa bweni..

Haya matukio yanaumiza mno ndugu zanguni.

Pia, soma=> Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai
 
Wadau wa Occupation Safety, inabidi hii mada waifanyie kazi. Mafundi walotengeneza wawe wanatoa user guide

Muda wa kuingia kwenye tank ni saa tisa asubuhi hadi saa mbili asubuhi.
 
A

kabisa ndugu yangu,
Usiku nimelala nasisimka
Moyo umeniuma sana
 
Wadau wa Occupation Safety, inabidi hii mada waifanyie kazi. Mafundi walotengeneza wawe wanatoa user guide

Muda wa kuingia kwenye tank ni saa tisa asubuhi hadi saa mbili asubuhi.
Kwa nini muda huo. Inabidi wasiingie kabisa ama kama mtu anaingia awe mtu mzima siyo watoto wa watu, inaumiza sana.
 
Kwa hio stoo ya mahindi ya shule inabidi ifagiwe na waalimu? Au shule ikodi vibarua wa kufagia stoo ya chakula cha wanafunzi wa sekondari?
Sio kazi ya watoto/wanafunzi kuwe na watu maalum wa shughuli hiyo...
Kwa hiyo unafurahia kuona vifo vya wanafunzi vinavyotokea!!!!🤔🤔🤔
Shule zinatakiwa ziwe na watu wao wanaofanya hiyo shuguli na sio wanafunzi
 
Ndo maana sijawahi kuamini akili za waalimu hata siku moja
Wana roho za kikatili sana 😪😪, utampaje mwanafunzi kazi ambayo inahitajika mtu mzima alieajiriwa kwa shughuli hiyo
 
Kwa hio stoo ya mahindi ya shule inabidi ifagiwe na waalimu? Au shule ikodi vibarua wa kufagia stoo ya chakula cha wanafunzi wa sekondari?
SIYO STOO ni kitu kama Tank la maji hivi ambalo limezibwa pande zote kwa nia ya kutoingiza hewa ili wadudu wasiingie na kuharibu mahindi, Sehemu isiyo na hewa ni hatari hivyo inatakiwa kuingia kwa uangalifu mkubwa hewa ni ndogo kuweka watoto sita kwa wakati mmoja ni kuwauwa. Inabidi vitumike vifaa maalum (Mifagio yenye mishikio mirefu sana) kufanya usafi huko siyo watoto wa watu.

Mwaka jana ama juzi ilitokea MOSHI. Ilibidi watu wajifunze hapa siyo kurudia kitu hicho hicho jamani ni mbaya sana hii lazima ikomeshwe haraka.

Wizara ya Elimu itoe Waraka kuzuia hiki kitu maana nchi nyingine WAZIRI angejiuzulu kabisa kama kweli imetokea tena maana mimi sijaiona kwenye vyombo vya habari, ilitakiwa aeleze ilipotokea Moshi alitoa maelekezo gani hasa. Siyo wanakaa kwenye V8 na kuhudhuria "Endless and Useless Meetings / Seminars " bila kujua dhamana waliyopewa juu ya watoto wetu.
 
Habari ndugu zanguni,
Naomba tushauriane na tutoe ya moyoni kuhusu shule zinazowaingiza watoto kufanya usafi kwenye maghala ya kuhifadhi mahindi hizi ishu naona isipoziwa sauti itakuwa sugu kwa sasa. Jana nimeona watoto Watatu wa Form 3 wamefariki Dunia baada ya mwalimu kuwachukua watoto sita kwa ajili ya kufanya usafi hatimaye watoto watatu wamefariki Dunia 😭😭.

Inahuzunisha sana nikiwa kama mzazi kwa sababu hizo ghala ni hatari kwa maisha ya watoto wetu ambao wanaishi shule za kulala, mtoto ameondoka mzima wa afya kwenda shule kusoma unarudishiwa nyumbani mtoto amelala inaumiza mnoo..

Mwaka jana hii ishu ilitokea katika shule mbili tofauti na jana tarehe 2/5 nimeona imetokea tena.. Ndugu zanguni najua humu viongozi mbalimbali wapo ikiwemo mama yetu Gwajima Atusaidie kupaza sauti kwa walimu katika hizi shule za Sekondari watoto wa bweni..

Haya matukio yanaumiza mno ndugu zanguni.

Pia, soma=> Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai
Mtu amepeleka mtoto akafundishwe yeye anampeleka kuzama kihengeni
 
Humu watakuja wathenge kukwambia siku zao zilifika au kaa na wanao nyumbani usiwapeleke shule
 
shule nyingi za bording kwa ufupi ukiangalia form zake zinaonesha wafanyaki wa mambo mengine si waajiliwa bali ni wanafunzi.
zipo shule zinatabia ya kulimisha wanafunzi mahindi ndiyo yatumike shuleni wakati wameandika pesa ya chakula.
miaka ya nyuma sema ndio mitandao ilikuwa hakuna.
swala la mashule wanafunzi kuwa wafanyakazi lipigwe marufuku jiulize mashule kuungua moto sababu wanafunzi wanageuzwa mafundi umeme,mafundi bomba,wakulima na kama kilichotokea hapo unaweza kuwafunga au kulipwa pesa nzuri sababu form ijasema mwanafunzi anatakiwa kuwa mfanyakazi wa stoo
 
Back
Top Bottom