Vifo vya watoto mashuleni vinavyotokana na kufanya usafi kwenye ghala za kuhifadhia mahindi

Habari ndugu zanguni,
Naomba tushauriane na tutoe ya moyoni kuhusu shule zinazowaingiza watoto kufanya usafi kwenye maghala ya kuhifadhi mahindi hizi ishu naona isipoziwa sauti itakuwa sugu kwa sasa. Jana nimeona watoto Watatu wa Form 3 wamefariki Dunia baada ya mwalimu kuwachukua watoto sita kwa ajili ya kufanya usafi hatimaye watoto watatu wamefariki Dunia 😭😭.

Inahuzunisha sana nikiwa kama mzazi kwa sababu hizo ghala ni hatari kwa maisha ya watoto wetu ambao wanaishi shule za kulala, mtoto ameondoka mzima wa afya kwenda shule kusoma unarudishiwa nyumbani mtoto amelala inaumiza mnoo..

Mwaka jana hii ishu ilitokea katika shule mbili tofauti na jana tarehe 2/5 nimeona imetokea tena.. Ndugu zanguni najua humu viongozi mbalimbali wapo ikiwemo mama yetu Gwajima Atusaidie kupaza sauti kwa walimu katika hizi shule za Sekondari watoto wa bweni..

Haya matukio yanaumiza mno ndugu zanguni.

Pia, soma=> Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai
Wizara ya Elimu kupitia kwa Kamishina wa Elimu inapaswa kutoa Waraka Maalumu wa Mwongozo kuhusiana na masuala kama haya. Shule za Bweni Mimi ninavyojua huwa zinakuwa na Wafanyakazi wengine wasio Walimu kama vile Wapishi ambao huwa wanafanya kazi kama hizi chini ya miongozo maalumu ya kazi hizo.
 
shule nyingi za bording kwa ufupi ukiangalia form zake zinaonesha wafanyaki wa mambo mengine si waajiliwa bali ni wanafunzi.
zipo shule zinatabia ya kulimisha wanafunzi mahindi ndiyo yatumike shuleni wakati wameandika pesa ya chakula.
miaka ya nyuma sema ndio mitandao ilikuwa hakuna.
swala la mashule wanafunzi kuwa wafanyakazi lipigwe marufuku jiulize mashule kuungua moto sababu wanafunzi wanageuzwa mafundi umeme,mafundi bomba,wakulima na kama kilichotokea hapo unaweza kuwafunga au kulipwa pesa nzuri sababu form ijasema mwanafunzi anatakiwa kuwa mfanyakazi wa stoo
Nafikiri hii haiko sawa sawa, zipo kazi ambazo zinapaswa kufanywa na Wanafunzi, lakini pia zipo kazi ambazo hazitakuwi kufanywa na Wanafunzi ikiwamo na hii ya kusafisha vihenge. Kwa mtazamo wangu kazi kama hii inapaswa kufanywa na Wafanyakazi wengine maalumu ambao wameajiriwa na Shule. Hebu jiulize: Je, wanafunzi hao huko shuleni walikuwa wanajipikia wao wenyewe chakula Chao Cha kila siku??
 
Tahadhari ni muhimu, tujifunze kuchukua hatua kuzuia matukio kama haya.
 
Sijui Kama govt inafuatilia haya matukio..😕 naona yanajirudia.
 
Habari ndugu zanguni,
Naomba tushauriane na tutoe ya moyoni kuhusu shule zinazowaingiza watoto kufanya usafi kwenye maghala ya kuhifadhi mahindi hizi ishu naona isipoziwa sauti itakuwa sugu kwa sasa. Jana nimeona watoto Watatu wa Form 3 wamefariki Dunia baada ya mwalimu kuwachukua watoto sita kwa ajili ya kufanya usafi hatimaye watoto watatu wamefariki Dunia [emoji24][emoji24].

Inahuzunisha sana nikiwa kama mzazi kwa sababu hizo ghala ni hatari kwa maisha ya watoto wetu ambao wanaishi shule za kulala, mtoto ameondoka mzima wa afya kwenda shule kusoma unarudishiwa nyumbani mtoto amelala inaumiza mnoo..

Mwaka jana hii ishu ilitokea katika shule mbili tofauti na jana tarehe 2/5 nimeona imetokea tena.. Ndugu zanguni najua humu viongozi mbalimbali wapo ikiwemo mama yetu Gwajima Atusaidie kupaza sauti kwa walimu katika hizi shule za Sekondari watoto wa bweni..

Haya matukio yanaumiza mno ndugu zanguni.

Pia, soma=> Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai
Unapoleta habari inayogusa kama hii uwe na facts, sio kujiandikia tu kimhemko. Ama unaandika kishabiki au una chuki na shule husika.

Tukio unalo-site halikutokea tarehe 2 bali 1 Mei. Na pia hapakuwa na kazi ya kusafisha ghala kama unavyoeleza hapa
 
Wadau wa Occupation Safety, inabidi hii mada waifanyie kazi. Mafundi walotengeneza wawe wanatoa user guide

Muda wa kuingia kwenye tank ni saa tisa asubuhi hadi saa mbili asubuhi.
Hata wakiifanyia kazi madogo walipangiwa watakufa hivyo Pindi tu walipozaliwa.
 
Ndo maana sijawahi kuamini akili za waalimu hata siku moja
We ni fala usiyejielewa. Akili hizo mbaya za walimu ndizo zilizokupa wewe uwezo wa kuweza kuharisha namna hii kwenye keyboard. Uwe na shukrani nyang'au weeee!!
 
Wizara ya Elimu kupitia kwa Kamishina wa Elimu inapaswa kutoa Waraka Maalumu wa Mwongozo kuhusiana na masuala kama haya. Shule za Bweni Mimi ninavyojua huwa zinakuwa na Wafanyakazi wengine wasio Walimu kama vile Wapishi ambao huwa wanafanya kazi kama hizi chini ya miongozo maalumu ya kazi hizo.
Haswaa
 
We ni fala usiyejielewa. Akili hizo mbaya za walimu ndizo zilizokupa wewe uwezo wa kuweza kuharisha namna hii kwenye keyboard. Uwe na shukrani nyang'au weeee!!
suala la walimu naona limekugusa pole sana Mwal. Mu7
Ila akili zenu kisoda wakati mwingine
 
Sasa mtu adi unakosa hewa bado unabung'aa tu ndani ya ghala, au mwalimu aliwafungia kwa nje. Mbona haimeki sensi kwa hao pupils ad nguvu inakuishia yote inakuaje apo
 
Hii inaonesha walimu wetu Wana elimu ya hovyo kabisa.elimu zao hazistahili kuwapa watoto wetu.wewe inajua kabisa kazi ya kihenge ni kuzuia uingiaji wa hewa lakini unawaingiza tu wanafunzi.inauma sana kusikia mtoto wako kufariki Kwa uzembe kiasi hiko
 
Siku nikisikia mtoto wangu anafanyishwa ushenzi wa aina hio shuleni lazma nilale mbele na hao walimu. Kama wanaona sahihi wafanye wao hio kazi.
 
Sasa mtu adi unakosa hewa bado unabung'aa tu ndani ya ghala, au mwalimu aliwafungia kwa nje. Mbona haimeki sensi kwa hao pupils ad nguvu inakuishia yote inakuaje apo
Mwilia unategemea oxygen kufanya movement. Ukiwa suffocated huwezi sogeza hata kidole.
 
shule nyingi za bording kwa ufupi ukiangalia form zake zinaonesha wafanyaki wa mambo mengine si waajiliwa bali ni wanafunzi.
zipo shule zinatabia ya kulimisha wanafunzi mahindi ndiyo yatumike shuleni wakati wameandika pesa ya chakula.
miaka ya nyuma sema ndio mitandao ilikuwa hakuna.
swala la mashule wanafunzi kuwa wafanyakazi lipigwe marufuku jiulize mashule kuungua moto sababu wanafunzi wanageuzwa mafundi umeme,mafundi bomba,wakulima na kama kilichotokea hapo unaweza kuwafunga au kulipwa pesa nzuri sababu form ijasema mwanafunzi anatakiwa kuwa mfanyakazi wa stoo
kilimo mashuleni si jambo baya ndugu

kazi za mikono ni muhimu mashuleni tena ikibidi shule ziwe na miradi ya ufugaji na kilimo kwa wingi sanjari na ufundi
 
Sasa mtu adi unakosa hewa bado unabung'aa tu ndani ya ghala, au mwalimu aliwafungia kwa nje. Mbona haimeki sensi kwa hao pupils ad nguvu inakuishia yote inakuaje apo
Daaah!
Je, umewahi kusoma somo la Chemistry angalau kwa basic knowledge tu??
Na somo la Biology nalo ulisoma kidogo? Hususani kuhusiana na mada ya Respiratory System?
 
Back
Top Bottom