Hii ni thread ya vifurushi ambavyo sio rasmi kama vya chuo au vifurushi maalum ambavyo vinatoa kiasi kikubwa cha internet, nitalist vifurushi ninavyovifahamu kama kuna wanaojua vyengine watasaidia
Tigo
Kwa Tigo bonyeza *147*00# kisha chagua size yako, unaweza kupata vifurushi vizuri, Ila njia hii sio reliable kwani vifurushi hivyo hubadilika kila Mara.
Vodacom
Vodacom angalia kwenye ya kwako tu, piga *149*03# kuangalia ofa.
Airtel
[
Halotel
-Royal bundles pengine kifurushi kizuri zaidi kwa Sasa kinakupa dakika takriban 200 na Internet unlimited kwa 0.5mbps kwa mwezi mzima. Ni vyema kwenda ofisi za Halotel na kununua line ya Royal bundle, pia unaweza kukuunga kwa kubonyeza menu yao ya *148*66#
-Mega bundle kwa shilingi 10,000 Unapata GB 15 ambazo unatumia mb 500 kila siku kwa mwezi, kujiunga ni *150*88#, unakiunga na salio la halopesa.
-Kifurushi Cha usiku kwa 1000 unapata Internet unlimited, kizuri kwa ajili ya kudownload files kubwa Kama games na movies. Kujiunga *148*66# kisha vifurushi maalum (ya kwako tu)
TTCL
-bandika bandua ni vifurushi vizuri kwa matumizi makubwa Kama kuangalia Netflix, zipo option Kama
-1000 GB 4 kwa siku (Mb 500 mchana 3.5GB usiku)
-2500 GB 10 kwa siku
-5000 GB 8 kwa wiki (3gb mchana na 5GB usiku)
Uzuri wake ni kwamba GB za usiku zinaanza saa 2 usiku muda mzuri ambao watu wanaangalia movies baada ya kutoka makazini.
-Toboa Night navyo ni vifurushi vizuri vya usiku in case Halotel kwako inasumbua ama Haina speed, kwa 500 unapata GB 2 na 1000 unapata GB 10.
Vyote toboa na bandika bandua unajiunga kwa kubonyeza *148*30# kisha TTCL bundles.
-Ofa maalum, pia TTCL Wana ofa mbalimbali Kama vile za sabasaba, nanenane etc ambazo wanazieka kwenye option ya vifurushi maalum,
Remote[/B][/B][/B]