Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Yap Voda wana Supakasi za aina mbili.

4G na 5G

In case haupo kwenye location inayo support 5G basi utapewa hiyo ya 115K ambayo ni 20Mbps
Sizani mbona kwenye simu Voda inashika 5g Ili eneo langu au Kuna utofauti wa simu na router?

Na hicho kifurushi Cha 5g kinaanzia bei gan?
 
Sizani mbona kwenye simu Voda inashika 5g Ili eneo langu au Kuna utofauti wa simu na router?

Na hicho kifurushi Cha 5g kinaanzia bei gan?
Inawezekana maeneo yako kuna 5G access ya voda

Airtel bado hawajafika
 
Inawezekana maeneo yako kuna 5G access ya voda

Airtel bado hawajafika
Mkuu hao Voda nao jau nimeongea nao huduma Yao Kila mwisho wa mwezi unatakiwa kulipia yhn hawana huduma ya free pain ni postpaid bado changamoto sanaa kama ikitokea tharura mwez huu hulipi basi unawapigia simu unawaambia Tena iwe issue ya maana ndio wanaweza kukuelewa[emoji1751]
 
Unataka siku usipoamua kulipia kusiwe na maswala ya kutoa taarifa na siku ukilipia kusiwe na charges kufidia siku ambazo haujalipia?

Kama ni hilo hata mimi nakusapoti maana sielewi hata sababu ya wao kuset mfumo huo ni nini haswa.

Ni kama wanatulazimisha hivi kusiwe na exit door yani tusalie kwenye huduma zao tu.

Wangeweka mfumo simple kama huu tunaotumia kwenye laini zetu za kawaida tunavyonunua bundle ingekuwa fresh.

Mtu anaamua kununua kifurushi muda wowote anaitoka na hata akikaa mwaka bila kuweka hakutakuwa na faini siku atayoweka, kwasababu kile kipindi ambacho hajaweka vocha hakuwa anapata hiyo huduma.
 
Mkuu Scars yule dada kanicheki leo, ananiambia eti maeneo nilipo inawezekana kuna 5g, hivyo kesho surveyor atakuja kucheki network kama kuna 5g...

Inavyoonekana wanahitaji wateja sana, shida wameshindwa kujua soko kubwa kwa sasa liko wapi...

Hivyo vifaa vyao vya 5g walivyofunga bunju,kunduchi,kawe nk wangevileta maeneo mengine kama kimara,ubungo,mbezi mwisho na kibamba wangepata wateja wengi sana....

Tuendelee kiwashauri waache kukimbilia maeneo yaleyale ambayo yameshakamatiwa tayari..
 
Hilo hata mimi nimeligundua

Mi juzi hapo alinipigia yule Dada akinisisitiza kuwa nimsaidie kutafuta wateja.

Akaniambia "atayeonesha nia ya kutaka huduma mwambie akupe namba yake halafu unitumie mimi"

Hapo nikagundua kwamba wanapambana sana kutafuta wateja, yani amefikia hatua anaanza kuhisi pengine watu naowapa namba zake hawamtafuti

Labda kwasababu ya ubize wa mambo mengi na hivyo anataka yeye ndio abebe jukumu la kuwapigia simu nikimpa namba zao.

Inaonesha dhahiri kuwa wana njaa na wateja ila wao wenyewe ni kama bado wanashindwa kujua sababu za wao kukwama zinatokana na wao wenyewe.
 
Changamoto sanaa kaka
 
Na wakijichanganya voda wakaleta vifurushi vya bei tofauti tofauti baasi wameisha..

BTW huku mtaani niliko voda wametandaza waya wa fiber kuelekea taasisi moja hivi ya serikali, nilimuuliza mwamba mmoja akasema mtu binafsi wanampelekea pia..

That means inawezekana mwakani soon fiber itakuwa siyo habari za kufikirika tena..
 
Changamoto sanaa kaka
Hii mitandao miyeyusho sometimes

Wanataka kutuweka katika system ya uteja tuwe watumwa wao.

Sijaona mantiki ya wao kutaka malipo ya aina hiyo.

Unaweza ukasema labda kwasababu unapewa kifaa chao bure.

Lakini haipo hivyo hata kama utaamua kutoa 850K ili kifaa kiwe mali yako uwe huru

Lakini ukishaingiza mguu kwenye packages zao basi utashurutika kuingia kwenye kausha damu yao ya kulipia kila mwezi, na uki skip basi mwezi unaotaka kulipia italazimika kulipia na ile miezi ambayo ilikuwa hujalipia na huduma ulikuwa hupati.
 
Kama umbali gani kutoka hizo nyaya za fiber zilipo mpaka wewe ulipo?

Halotel nao wanazo ila walinitajia madola mengi yakunikomoa.

Ulizia bei kwanza za installation pamoja na packages zao kama zipo friendly
 
Kama umbali gani kutoka hizo nyaya za fiber zilipo mpaka wewe ulipo?

Halotel nao wanazo ila walinitajia madola mengi yakunikomoa.

Ulizia bei kwanza za installation pamoja na packages zao kama zipo friendly
Mimi binafsi najua siwezi gusa maana niko mbali.... Ila kwa walio mita kadhaa najua wataunganishwa kwa bei chee kabisa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…