Bei chee itategemea na eneo ambalo upo.
Kama upo DSM maeneo ya Sinza, Masaki, Mbezi, Kawe nk. Huko kuna Fiber ambazo vifurushi vyao ni kuanzia 70K na installation haizidi 200,000
Maeneo hayo pia hata TTCL wapo na wana package za 55K ila sijawaweka kipaumbele kwasababu ni miyeyusho. Hawaaminiki.
Tofauti na hapo hakuna kifurushi cha unlimited unachoweza kupata below 70K
Kama ni ushauri ni bora ukatafuta 110K uchukue Router ya Airtel yenye 30Mbps ambapo baada ya mwezi utaweza kununua package ya 70K kama 110K inakuwa ngumu ku afford.
Ila kama ukiwa maeneo ya biashara una ofisi yako basi unaweza ku share na majirani zako wakawa wanakulipa buku buku ambazo utakuwa unalipia kifurushi mwisho wa mwezi.