Najua wewe ni mgeni wa hii mitandao na huijui vizuri. Kuna watumiaji wa chini, kati na wajuu. Kutumia hiyo mb kwa masaa ni wewe lakini haibadilishi ukweli. Tigo ilikuwa ukiacha hela wanakuunganisha na hadithi bila wewe kujiunga na hii ishanitokea sana. Kuhusu kutotoboa siku tatu nilikuwa natumia matumizi ya kawaida ya kuperuzi jamii forum nayo ilikata na siyo mara mmoja zaidi ya mara 4. Mara zote 4 mb zinakata siku 3, Sasa huoni hapo kuna tatizo?. Hii mitandao nailewa sana. Tigo, Voda na halotel labda unidanganye kwenye mitandao mingine. Ya kwako tu, Size yako TIGO (Utapeli mtu). MB kadhaa facebok, Mb kadhaa Whatsapp. MB kadhaa mchana, mb kadha usiku ni utapeli mtupu. Kuna kifurushi cha Tigo cha Youtube ilikuwa unajiunga kwa 500 wiki lakini kilikuwa kinakata kwa siku 2 tu. Sasa hivi vifurushi vimekuwa dili vinapunguzwa kila siku
Kwenye matumizi ya internet wewe hata unafikii. kwa masaa 6 natumia GB 20 na zaidi na bado hazinitoshi. Hii mitandao ina kajanja sana labda kama wewe ni mfanyakazi wa Halotel. Kuna nyuzi humu watu wanalalamika sana kuhusu hii mitandao, vifurushi kila siku vinabadilishwa. Mpaka kuna mbunge fulani alikuwa analalamika bungeni vodacom wanaiba dk. Mimi siyo mgeni wa hii mtandao, nimetumia sana internet ya bure ya Airtel usiku, THE GRID ya vodacom nimeitumia sana. Ile internet ya Airtel, jamaa anakuunga kwa 1500 kwa siku 2 kwa GB 10. KIFURUSHI KILICHOBAKIA CHA USIKU NA NI BORA AMBACHO MITANDAO MINGINE HAWANA NI CHA HALOTEL CHA 1000 UNAPATA UNLIMETED INTERNET. Hii nayo utabisha
UZI WA CHIEF MKAWA WA MWANZO ULIKUWA UNAVUTIA SANA KWA KUPAMBWA NA VIFURUSHI WENYE GHARAMA NAFUU WENYE DK NYINGI, SMS NA GB ZA KUMWAGA LAKINI KWASASA UMEBAKI MIFUPA NA WALA HAUVUTII TENA KAMA MWAZO. HII MITANDAO IPO KWA AJILI YA KUPIGA PESA TU.